Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Man City wana academy bora kwa kigezo gani mzee

Nitajie senior players 5 wanaowika Ulaya waliopikwa City academy
Kwani tangu aondoke Fergie kuna senior players wangapi wanawika ulaya from MUFC academy?
 
Timu imejengwa kwa miaka 26 wafanyabiashara wanakuja kuiua kwa miaka 6 tu.......
 
Kwani tangu aondoke Fergie kuna senior players wangapi wanawika ulaya from MUFC academy?
Paul pogba, Pique, Lingard, Rashford, Mc tominay, Rossi, Tim Heaton, Spector, simpson, drink water, de laet, Phil bradsley, Joshua king, cathcart, Michael Kean, Robbie Brady, Tuanzebe, fosu mensah, perreira, welbeck, januzaj, Morrison, Pereira (kipa), Johnstone etc

Leicester wanachukua ubingwa na wachezaji 5 toka academy ya man U,

Kwa Uingereza man city Ni academy ya 5 list ipo Kama Hivi

1. Man UTD
2. Totenham
3. Southampton
4.chelsea
5. Man city.

Wamezirank kwa dakika ambazo academy graduates wamecheza. Man utd Ni zaidi ya mara mbili ya city.
 
Luiz sio key player. Hazard, Kante Ngolo, Kepa, Rudiger, Willian, na n.k ndo key player. modogo kama akina Odoi, Mount, na n.k ni upcoming key player. .
 
Vizuri sana mkuu, wewe ndo fan wa mpira.
 
Mimi nadhani tuwape nafasi makinda wanaweza kutusogeza mbele kidogo kuliko kutegemea wachezaji kama Dyabala ambao hawako tayari kupigania team.

Ole kajitahidi kusajili sehemu zenye mapungufu hasa eneo la ulinzi,bado kiungo na mshambuliaji wa kulia.Pia tukumbuke usajili ulikuwa mgumu kweli kweli hasa bei za wachezaji zipo juu sana.

Tumefanikiwa kuziba pengo mlinzi wa pembeni kulia na baki wa kati,naamini Fred,Pereira,Fosu Mensah na McTominary wana uwezo wa kuziba pengo la Hereira na Manywele.Sehemu pekee bado tutaumiza kichwa ni mshambuliaji wa kulia.

Lukaku sidhani kama kaacha pengo kubwa kinda Mason ana uwezo mkubwa kuliko kubwajinga Lukaku.Sijui kwanini mpaka sasa naamini Sanchez anaweza kutusaidia msimu huu.

Tupe team yetu moyo badala ya kulalama.
 
Mkuu I feel your pain, but I also try to understand the fact

Kwa upande wa beki ni ukweli usiopingika tumejiimarisha msimu huu, ni kweli tulitamani Shaw awe na compitition na back up pindi akiumia lakini huwezi kusajili timu nzima katika msimu mmoja.

Back four ya Wan Bissaka/Dalot, Tuanzebe/Lindelof, Maguire, na Shaw sio mbaya kama baadhi ya watu wanavyotaka kutuaminisha. Ni timu ngapi zenye subs za beki kama Smalling, Bailly na Rojo aliye mzima bila majeraha? Ni chache sana.

Lingard. Kabla hatujamuhukumu, tunapaswa kujiuliza kwanini pale Three Lions lazima apate namba piga uwa. Hiyo ni ishara kuwa ana kitu flani. Lakini nikukumbushe kwa United hana uhakika wa namba.

Tatizo kwa usajili wa msimu huu ninaloliona ni kuongeza angalau mid fielders wawili, defensive 1 na creative 1. Pia tulipaswa ku replace magoli ya Lukaku kwani Rashford hana uwezo, ila Sanchez mzima anaweza kutufungia magoli kama false number 9 na Martial akiaminiwa (kama ilivyokuwa msimu wake wa kwanza United) anaweza kufunga magoli. Namuunga mkono Lukaku kuondoa, United fans hatukumuonesha upendo kabisa.

Kwa mtazamo wangu hata Lukaku angebaki bado asingetusaidia kwani kocha hampi nafasi. Hivyo ni bora tu alivyoondoka. Angebaki ni wale watoto wangeendelea kuanza, ameondoka bado ni hao watoto wataendelea kupata namba, kwa hiyo mbadala au bila mbadala ninaona ni yale yale

Kuna watu walitamani tuwaondoe wachezaji wote tusiowataka. Rojo, Jones, Lingard, Sanchez, Smalling, Young, Mata, Lukaku, Matic na wengine,wote waondoke. Je tungesafisha timu nzima?Je tungepata wanunuzi kwa bei tunayotaka? Kumbuka mashabiki huwa tunataka quick fix, je unajua wamiliki nao wanataka hela? Hata ungekuwa wewe ndio mmiliki ungewaondoa tu ili uwaondoe bila kujali hasara?

Je kwa soko la sasa hao wachezaji wote unawa replace vipi? Muda unao wa kuwa replace dirisha lenyewe ni fupi, tuchukulie una muda. Kwa soko la sasa una hela ya kuwa replace hao wachezaji?

Utasema hela ya kuwauza akina Lingard, sasa ukiwa desperate utawauza kwa hasara je hela ya kuwauza wote hao utapata hela ya kununua hata wachezaji wawili wenye kiwango ukitakacho? Na kumbuka hapa utatakiwa ununue wachezaji wa kujaza squad sio unaondoa 8 unaleta wawili au watatu.

Kuna maswali mengi kuliko majibu. Nakubaliana na wewe kuna shida kwenye hierarchy ya United, lakini kuna mambo tunayakuza sana.

Mfano, kuna baadhi yetu tunamlaumu OGS kwenye usajili, je ni kweli OGS hakumtaka BF au hakumtaka winger wa kulia. Tunapenda sana kulaumu.

Ed Woodward ni shida, hilo halina ubishi, Glazers ni shida, hilo halina ubishi, Board ni shida hilo halina ubishi. Wote hao wanaangaalia zaidi commercial aspect pale klabuni kuliko football aspect.

Angalau tukipata Sporting Director tunaweza kufanya vizuri zaidi kwenye madirisha ya usajili yajayo.
 
Kwani tangu aondoke Fergie kuna senior players wangapi wanawika ulaya from MUFC academy?
Kwani academy ya United imeanzishwa Fergie alipoondoka?

Haya embu niambie kuna senior players wangapi wanaowika Ulaya pale Man City tangu timu iundwe (achilia mbali, tangu 2013 Fergie alipoondoka, maana hicho si ndio kipimo chako)

Vipi kuhusu Barcelona wapo wangapi wanaowika tangu 2013?

Nirudi kwenye swali lako, kwa uchache hao ndio wanaowika Ulaya tangu SAF aondoke United kutoka United Academy

Rashford Three Lions

Scot Tominay Scotland

Tuanzebe Three Lions

Henderson Goalkeeper - Shefield Wednesday - Three Lions

Pereira - kaitwa Selecao mara moja
 
Akirudi uni tag mkuu
 
Hao ndio wanawika Ulaya saiv? Yaani hao uliowataja ndio wanatikisa Ulaya ni tishio kweli kweli? Duh!
 
Hao ndio wanawika Ulaya saiv? Yaani hao uliowataja ndio wanatikisa Ulaya ni tishio kweli kweli? Duh!
Tunacompare Man UTD na man city,

Hebu nitajie man city toka club ianzishwe mchezaji mmoja tu Kama Pogba au pique ama Rossi.

Pique Moja ya beki Bora duniani,

Pogba Moja ya midfield Bora duniani

Rossi Moja ya striker Bora duniani (top scorer Serie A na la Liga Mara kibao Kasumbuana na Kina Ronaldo na Messi). Sema Majeruhi tu yameharibu career yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…