sifa ya klabu tajiri inayotaka kurudi kwenye ubora wake.
- itambakisha romelu lukaku huku ikiendelea na jitihada za kumtafutia wachezaji watakaompa huduma bora.
- itatoa cash kwa ajili ya usajili wa paul dyabala ili aongeze nguvu kwenye safu ya ushambuliaji na si kufanya dili la kubadilishana wachezaji
- kama humuhitaji romelu lukaku basi tafuta mshambuliaji mwengine mfano wa piatek kutoka ac milan, kufanya hivyo ndio utakuwa umeziba pengo lake.
Rashford, Martial, Greenwood, Sanchez hawa wote hakuna hata mmoja anayekupa matumaini ya kufanya vizuri kwa mechi zote 38 za ligi kuu ukiongezea na mechi za michuano mengineo.
msimu huu tunakwenda kudhalilika tena endapo tutafanya maamuzi ya kumuondoa romelu lukaku bila ya kutafuta mshambuliaji mwengine, hivi tunamuondoaje mwanadamu mwenye uhakika wa kutupa magoli 20 kwa msimu kwa kumtegemea rashford na sanchez?
tusidanganyane hawa vijana wetu akiwemo greenwood, tahit chong, gomez na wengineo hawatafikisha hata mechi 15 za kucheza msimu huu hivyo basi tulipaswa kuiongezea makali safu yetu ya ushambuliaji bila ya kumuondoa mchezaji yeyote muhimu.
tatizo jengine ninaloliona kwenye timu yetu ni lile la kuendelea kutegemea miujiza kupitia upande wetu wa kushoto, ok tumemsajili wan bissaka lakini jamaa uwezo wa kushambulia ni mdogo. Hata ukiangalia hao winga wetu wanaotokea upande wa kulia ndio wale wale tuliowazoea.
Si ajabu kushuhudia tena msimu huu tunamtumia diogo dalot nafasi ya winga wa kulia kana kwamba dirisha la usajili halijatufikia wakati kumbe tumelipuuzia utadhani tuna wachezaji mfano wa sterling, sane na mahrez.
tungelifanya jambo la maana sana kama tungelitafuta mshambuliaji machachari anayetumia mguu wa kushoto au yote miwili akawa ana cut inside kama wanavyofanya jamii ya wachezaji mfano wa arjen robben, mchezaji pekee ambaye nilimuona atatusaidia kuwa na safu ya ushambuliaji ilio na balance pande zote mbili ni kijana wa ivory coast anayeitwa
nicolas pepe ambaye huenda akasajiliwa na arsenal muda wowote.
aubameyang + pepe + lacazette + mesut ozil + mkhitaryan + iwobi
akitokezea mwanadamu anahutubia mbele ya hadhara huku akijisifu ya kwamba manchester united ndio klabu ya pili kwa utajiri duniani basi mkatalie hata kama ni mzee wako haijalishi huna hoja za msingi za kiutetezi.