Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Dybala requested 10m€ net per year to Manchester United, but not accepting 25% cut clause if no Champions League spot that Mufc impose on whole squad.

Dybala playing difficult, Lukaku-Juventus on hold.

Few days ago Dybala rejected Inter.

Meanwhile, Cavani too rejected Inter
 
Shida inakuja united haina striker zaidi ya Rashford na Lukaku,so hapo huwezi kumtoa striker ambaye una uhakika wa kupata magoli mengi zaidi kutoka kwake kwa usajili wa free role player..
Tusimdharau hivyo dybala,binafsi naamini uwepo wa ronaldo ndo umefanya akawa hana msimu mzuri binafsi.na huu mbadilishano nahisi kama Man u ndo anafaidika zaidi kulingana na ubora wa wachezaji hao wawili.
 

Ww jamaa jukwaa lako limekushinda nn
 
Inavyoonekana,
Mfumo ambao OLE anataka kuutumia hauhitaji in-and out striker.

Tofauti na hivyo hakuna haja ya kumuuza Lukaku.
 
Hata Juve watafaidika mkuu, in short ni win win situation,

Sisi tunabadili mfumo tunataka mtu wa kulink up play na Dybala ni perfect.

Juve nao wamebadili mfumo, majority ya Magoli ya Ronaldo msimu uliopita ni ya Vichwa, msimu uliopita Juve wamepiga cross zaidi ya 700, so timu inayopiga cross 20 Mpaka 30 kwa match moja kwa Lukaku ni Dodo limemdondokea mlangoni.
 
Huyo Dyabla hana uwezo wake na uchezaji wake hana tofauti na Juan Mata .. Hana anachomzidi Mata .. Mimi nafuatilia sana Seria A tangu nimeanza kumuona anavyocheza huwa napata picha ya Juan Mata ..


Sasa kwanini tuongeze player Mwenye uwezo sawa na waliopo ?? Hilo ndio suluhisho la matatizo yetu ?
 
This is not Win-Win Deal..


Ni uwazi tumepigwa .. Narudia tena tumepigwa.. Huyo Dybala hataweza kutusua EPL . Tunza haya maneno Yangu ..
 
Watu wanaosema tunanunua wachezaji ambao wa aina yao tunao wananishangaza sana, hivi hawaoni kitu Pep anafanya?

Aliumia Fernandinho, kama Pep asingekuwa na wachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza eneo moja ubingwa ungekuwa ndoto kwake.

Huwezi kuwa na timu ya kutegemea kushindania ubingwa halafu unakuwa na mchezaji mmoja bora katika eneo fulani halafu wengine wote ni vimeo.
 
Mimi ndio Ninasema hivyo naomba unitag ..


Nilijua tu utamtolea mfano Pep ili ujiBack Up..

Kwanza kabisa huyo Dybala hakuwa kwenye Mpango kazi wa Ole , how umlinganishe na Pep anaesajili kwa kufuata mpango kazi wake ?? Acha linganisha Pep na Uchafu au takataka zinazofanyika pale united ..


Mimi sipingi namba moja kuwa na wachezaji hata sita , ninachomaanisha Mimi ni je , huo isajili ni moja ya matatizo ya msingi kwa united kWa sasa ?? .. It's absolutely NO NO NO... Matatizo yetu yanafahamika na kuonekana ..

Hatuna strikers na Mabeki wa kati wa maana .. Hiyo namba 10 pale united tuna wachezaji wenye uwezo wa kucheza ile namba vizuri mno (Mata na Pareira).. Ni suala la kocha kuwapa muda tu wa kutosha dimbani .. Kuliko kufanya Gambling kwa mchezaji ambae kuja Ligi ya EPL ni kama kurusha sarafu hewani .. Tunabeti ...



United ishughulikie matatizo yake ya msingi ya safu ya ushambuliaji na mabeki wa kati .. Hatuwezi kuanza ligi tuna Prone Injury players kama Roho na Baily halafu tutegemee Jones na Smalling .. Nilitegemea mpaka sasa tuwe tumevunja bank na kusajili walau mabeki Wawili wa kati ..


United ya msimu ujao inaweza kufanya vyema kwa kuwa na striker mzuri bila huyo dybla .. Ila tunaweza kuboronga tukiwa na Dybala bila kuwa na striker mzuri .. Maana yake ni nini ?? Ni kwamba kama akisajiliwa Good striker kazi ya Dybala inaweza kufanya na wachezaji wengi tu na tutafanya vizuri ..



So issue sio kusajili rundo la wachezaji kwenye namba moja , issue ni sajili tufanye kwenye maeneo yenye changamoto
 
Halafu kusema kwamba Rashford ndio kamuondoa Lukaku, sio sahihi.

kuondoka Lukaku, ni kwa sababu OLE anataka attackers wawe dynamic/fluid, sio striker anasubili mpira umfikie mguuni, ndio aonekane.

sifa ya klabu tajiri inayotaka kurudi kwenye ubora wake.
  • itambakisha romelu lukaku huku ikiendelea na jitihada za kumtafutia wachezaji watakaompa huduma bora.
  • itatoa cash kwa ajili ya usajili wa paul dyabala ili aongeze nguvu kwenye safu ya ushambuliaji na si kufanya dili la kubadilishana wachezaji
  • kama humuhitaji romelu lukaku basi tafuta mshambuliaji mwengine mfano wa piatek kutoka ac milan, kufanya hivyo ndio utakuwa umeziba pengo lake.
Rashford, Martial, Greenwood, Sanchez hawa wote hakuna hata mmoja anayekupa matumaini ya kufanya vizuri kwa mechi zote 38 za ligi kuu ukiongezea na mechi za michuano mengineo.

msimu huu tunakwenda kudhalilika tena endapo tutafanya maamuzi ya kumuondoa romelu lukaku bila ya kutafuta mshambuliaji mwengine, hivi tunamuondoaje mwanadamu mwenye uhakika wa kutupa magoli 20 kwa msimu kwa kumtegemea rashford na sanchez?
tusidanganyane hawa vijana wetu akiwemo greenwood, tahit chong, gomez na wengineo hawatafikisha hata mechi 15 za kucheza msimu huu hivyo basi tulipaswa kuiongezea makali safu yetu ya ushambuliaji bila ya kumuondoa mchezaji yeyote muhimu.

tatizo jengine ninaloliona kwenye timu yetu ni lile la kuendelea kutegemea miujiza kupitia upande wetu wa kushoto, ok tumemsajili wan bissaka lakini jamaa uwezo wa kushambulia ni mdogo. Hata ukiangalia hao winga wetu wanaotokea upande wa kulia ndio wale wale tuliowazoea.

Si ajabu kushuhudia tena msimu huu tunamtumia diogo dalot nafasi ya winga wa kulia kana kwamba dirisha la usajili halijatufikia wakati kumbe tumelipuuzia utadhani tuna wachezaji mfano wa sterling, sane na mahrez.

tungelifanya jambo la maana sana kama tungelitafuta mshambuliaji machachari anayetumia mguu wa kushoto au yote miwili akawa ana cut inside kama wanavyofanya jamii ya wachezaji mfano wa arjen robben, mchezaji pekee ambaye nilimuona atatusaidia kuwa na safu ya ushambuliaji ilio na balance pande zote mbili ni kijana wa ivory coast anayeitwa nicolas pepe ambaye huenda akasajiliwa na arsenal muda wowote.

aubameyang + pepe + lacazette + mesut ozil + mkhitaryan + iwobi​

akitokezea mwanadamu anahutubia mbele ya hadhara huku akijisifu ya kwamba manchester united ndio klabu ya pili kwa utajiri duniani basi mkatalie hata kama ni mzee wako haijalishi huna hoja za msingi za kiutetezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…