Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Koulibally ni habari nyingine asee. Ana kila kitu anachopaswa awe nacho defender Wa kati
 
Hapo ndo na Mimi ninapoahangaa huyu ole hawa watoto anaonunua atabadili na mfumo Wa kiuchezaji au ni huu huu? Mana mtu kama DJ hata Bruno ni wazuri na wanaweza onyesha potential zao vema kama timu itacheza pressing style
 
Hapo ndo na Mimi ninapoahangaa huyu ole hawa watoto anaonunua atabadili na mfumo Wa kiuchezaji au ni huu huu? Mana mtu kama DJ hata Bruno ni wazuri na wanaweza onyesha potential zao vema kama timu itacheza pressing style
mara nyingi ole amesikika akisema ya kwamba anavutiwa na style anayofundisha jurgen klopp na anapenda kuona man utd tunacheza mpira wa kasi msimu huu, sielewi kama malengo hayo bado yapo kwenye fikra za OGS.


lakini kama kweli ole ni muumini wa pressing kwa nini ameshindwa kuingiza style hiyo kati kati ya msimu baada ya kupewa mkataba wa kuifundisha klabu?

ukiangalia wachezaji tulionao msimu huu ndio wale wale tuliomaliza nao msimu uliopita tofauti na klabu ya real madrid ambayo imeingiza wachezaji watano na wanaelekea kutoa wachezaji sita,

ole alipaswa kuimplement style mpya ya uchezaji tokea msimu uliopita ili apate kufanya uchambuzi wa kina kwa kila mchezaji amfahamu ubora wake na udhaifu wake.
 
Unanikosha na makala zako mkuu Daemusin
 
Mata siyo kilaza bro. Vilaza ni hao wengine
 
utamaduni: United yenye mafanikio haijawahi kusajili established wingers, wingers wetu wote bora walikua wakawaida sana kabla ya kufika united.
 
Hata Leceister city imechukua Premier League huku Spurs ikishindwa kufanya ivo.

Hizo timu ulizozitaja zote, tukianza na huyo Atletico Madrid, ana mafanikio gani ndani ya miaka sita dhidi ya Real Madrid? Usifananishe MUFC na timu kama Atletico, huyo mfananishe na spurs. Mi ntakwambia PSG ina mafanikio zaid kuliko MUFC vile vile ndani ya hio miaka sita na ina mastar kibao ndani na wana perform vizuri tu. Hapa tunachozungumza ni MUFC kushindana na European Giants, tunataka kuchukua UEFA champions League, tuwe na timu ya kushindana na Real madrid, Barca, Juve n.k sio tuwe tunatizama mbona spurs kafika final bila star? na ndio maana nkasema kuwa hata Leceister amechukua EPL bila ya star hata mmoja, hizo ni flukes tu. Tunataka kushindana na Liverpool na Man city kuchukua EPL, basi tuwatizame wenzetu je wanakuza vipaji au wanaleta ready made machines? Kama wanakuza vipaji, basi hakuna tatizo kukuza kipaji na sisi, ila kama wanaleta ready made machines, muda wa kukuza vipaji hamna, unaweka experienced players, wa kukuza vipaji unapeleka kwa mkopo kwengine.

Mnaoishi 2013 ni nyie mnaoamini kama we still need inexperienced players kuwakuza wakati wenzetu wanatwaa ubingwa! mambo ya zamani hayo saivi football is changed, every top manager is hungry for titles and got little or no time to develop a player.

Na hao Star ambao wamenunuliwa MUFC kwanini wame under perform? Mbona Real madrid wanadai hela ndefu na wanapewa na wana perform vizuri?
 
Kwenye la liga miaka 6 iliopita.


Miaka 6 iliopita kwenye la liga Madrid kachukua mara 1 na Atletico mara 1, na wote wawili wameshika nafasi ya pili mara 2 hivyo kwenye ligi ya uhispania miaka 6 iliopita Madrid Hana chochote Cha kujivunia mbele ya Atletico.

Na usisahau Madrid walikuwa wakibebwa na Ronaldo muda wote huo.

Toka Fergie astaafu hatujawahi Hata kufikia nusu fainali ya Uefa ila Atletico kaingia fainali mara mbili, Monaco kaingia nusu, Ajax nusu etc hio ndio reality.

Na hizo machine unazozisema wewe si zimekuja kibao tu?

1. Di Maria anakuja man U Kama top Assist wa ulaya Nzima
2. Mkhitariyan same top Assist ulaya Nzima
3. Ibrahimovic anakuja akiwa kapitwa Goli 1 tu na Messi
4. Pogba Wonder kid
5. Falcao alievunja rekodi ya magoli mashindano ya Ulaya
6. Shaw Wonderkid mwengine na most expensive teeneger wakati wake.
7. Martial Golden boy etc

Wametusaidia nini mkuu?

Mjinga ni yule anaerudia kitu like kile Kila siku na hakifanikiwi.

Na hao Leicester walifanikiwa sababu walijenga kikosi Cha ushindi na Sasa hawana mafanikio sio sababu kwamba walibahatisha, Bali hawana hela na kikosi Chao kimebomolewa, Leo Ngolo kante tunajua alichofanywa World cup na Chelsea, Mahrez tunamjua, Vardy tunamjua etc. Wangekuwa na hela wasiwauze pamoja na kuimprove still wangesumbua top 6.
 
Miaka 6 iliopita kwenye la liga Madrid kachukua mara 1 na Atletico mara 1, na wote wawili wameshika nafasi ya pili mara 2 hivyo kwenye ligi ya uhispania miaka 6 iliopita Madrid Hana chochote Cha kujivunia mbele ya Atletico.
Akachukua Champions League 3 na Atletico kachukua 3? Labda swali hili ndio litakwambia tofauti ya izo timu mbili.

Na usisahau Madrid walikuwa wakibebwa na Ronaldo muda wote huo.
Kwaio hapa tunaona Star ambae alikuwa akicheza kwa determination, na sio POGBA anaedai mishahara tu.

Toka Fergie astaafu hatujawahi Hata kufikia nusu fainali ya Uefa ila Atletico kaingia fainali mara mbili, Monaco kaingia nusu, Ajax nusu etc hio ndio reality.
Tatizo lilikuwa nini sisi kutokufika nusu final miaka sita hio?

Kwaio mashine zimekuja izo, hebu nambie tatizo lilikuwa nini hata tukose mafanikio? Kwanini mashine hizo zikienda kwengine zina perform fresh?
Fact is at that time, EPL big teams zilikuwa ovyo tu. Kama aliweza kujenga kikosi cha ushindi anashindwaje kutengeza chengine basi kama wao wanategemea kukuza wachezaji ndio watese England.
 
Tumeleta ready made Falcao, Di Maria, Depay, Bastian, Pogba, Zlatan, Fred, Sanchez, Rom & Co. Lakini tumepata nini cha maana (kwa standards za United na ubora wa hao tuliowaleta)?

Tumuache Spurs, Liverpool ameleta world class gani (usintajia the unknown Southmpton CD who turn out to be world class while he is at Liverpool), lakini kwa miaka 2/3 ameleta changamoto kwenye ligi na amefika mara 2 UCL na kwenye mojawapo amechukua kombe

Kwanza timu inayopata mafanikio kwa mfumo wa Galacticos ni moja tu duniani, that's Real Madrid.

Miaka yote Barca wamekuwa wakichanganya ma super stars na the potential unknown players whose later become world class players. Hivyo hivyo wamekuwa wakifanya Bayern na Man Utd wakati wa SAF.

PSG pia wanatumia mfumo wa Galacticos siku hizi lakini wanaambulia kushinda kila mwaka ligi yao ya Wakulima.

Pia, naona kuna watu wanapotosha. Sio kwamba United hataki kununua Wachezaji wenye majina tayari, NO. Mwaka huu umekuwa mgumu kwa kuwa timu haipo UCL hivyo haina pool factor kwa wachezaji wa kaliba ya akina Rabiot.

Kwa mfano nia ya kumtaka BF na Koullibaly ni ishara tosha kwamba club ipo tayari kununua Wachezaji ready made lakini wawe na right profile ambayo OGS anaitaka

Kwa sasa naunga mkono juhudi za kujenga mafanikio na si kununua mafanikio
 
Mkuu unaweza ukawa na kila aina ya mchezaji lakini wakawa hawataki kucheza MUFC, utafanikiwa?

Kwa mfano kama sasa ivi POGBA amekwisha weka wazi kuwa MUFC basi tena, wewe unamshikilia aendelee kubaki what do you expect? Hichi ndicho nnachozungumza mimi, mchezaji hata mtolee mbali asije akazamisha Jahazi! As a manager lazima uwaoneshe who is the Boss, ndio SAF alivokuwa. Mchezaji mapozi mengi, unamtoa nje!

Unamuongezea mkataba Ashley young halafu eti unataka kushindana na LFC au MCFC?

Nyinyi mnasema kuhusu ma star waliokuja not delivering, vipi na hao ambao potentials walio flop? what is the reason behind?
 
Mkuu pengine hii comment yangu ya mwisho kwako.

Tatizo kubwa la watanzania na Binadamu wengi huwa tunaangalia mafanikio pale yanapotokea na hatujishughulishi kujua yametokea vipi, nitakupa mfano mzuri man UTd ya 2008, moja ya kikosi Bora kupata kutokea. Baada ya mafanikio ya 1999 timu yetu ilidrop na ulaya tukawa tunafanya vibaya Sana na kuna muda Fergie alikuwa anazomewa, kipindi Fulani Arsenal Invicivble na Mou miaka 2 mfululizo anachukua ubingwa huku sisi Hata kuvuka makundi Uefa ni Tabu. Hadi mashabiki walikuwa wanazomea wanataka Fergie Afukuzwe.

Lakini at that time tulikuwa tunajenga kikosi upya walisajiliwa wachezaji Hawa
1. Rooney kitoto Cha Everton
2. Ronaldo kitoto chengine Toka Sporting
3. Nemanja vidic beki asiyejulikana Toka spartak Moscow
4. Patrice Evra
5. Ji sung park (Evra na park kidogo walikuwa wanajulikana lakini still huwezi kuwaita ma super star at that time)
6. Carrick etc

Hao wachezaji around 2004 mpaka 2006 walikuja plus watoto wengine waliokuwepo Kama Rio Ferdinand,

Strategy hio ilikuja baada ya strategy ya kununua ma super star kufeli, kabla ya hao tulinunua masuper star Kama
1. Juan Sebastian veron fundi wa Ki Argentine
2. Kleberson mshindi wa world cup 2002
3. RVN
4. Fabian bhartez
5. Laurent Blanc etc

Hivyo mkuu huo ni mfano halisi Toka Man United kwamba kununua machine hakujengi tu kirahisi timu Bali unatakiwa kuanzia na squad players kwanza.

Baada ya hao kina Evra na park na timu kukaa sawa tukai re enforce na masuper star akaja Tevez, Hargreaves, Anderson etc

Sio man U tu naweza kupa mifano ya Timu nyingi, Barcelona walivyopoteana alienda LVG pale decision alizofanya aliblock mauzo ya watoto Kama puyol, Valdez, xavi, iniesta etc hao walikuwa Hata hawajulikani, akawa anawapiga benchi kina Rivaldo, Leo ukiona Barcelona wanasajili Suarez ama coutinho unadhani Wana mafanikio sababu hio unasahau struggle walioipata miaka kadhaa iliopita.

Same kwa Bayern hicho hicho kilitokea.

Kama nilivyosema comments za juu Hata uwe na Ronaldo na Messi Kama hauna Backbone ya Timu haisaidii, unamuona Messi na Aguero Argentina? Si wazuri wale mbona wanaflop? Masuper star wanakuja baadae baada ya kutengeneza timu.

Wachezaji tuliosajili msimu huu ni wazuri na Kama tunapata hao ambao tetesi zinasema wanakuja Kama Bruno, Ben Yedder, Maguire etc wote ni squad players wazuri watatu improve.
 

Ukifanya analysis ya msimu uliopita ni wazi timu ilikuwa mbovu kwenye idara zote (ulinzi,kiungo & ushambuliaji) na usajili uliofanywa so far sijaona kama utaleta mabadiliko makubwa tofauti na msimu uliopita kibaya zaidi ni jinsi competitors wetu jinsi wanavyojiimarisha

Bado Rojo,Young,Smalling,Jones,Bailly,Darmian,Shaw ndio watacheza kwenye ulinzi tumemsajili Daniel James ambaye ni left winger while (Martial,Sanchez) wanacheza nafasi hiyo so bado tutaendelea kuwategemea kule academy kuna Chong,Gomes na Greenword why hawakuwa promoted ?

Rooney alikuwa na uwezo mkubwa sana kabla hajatua United I hope uliangalia ile Euro iliyofanyika Portugal kiwango alichoonyesha Rooney kabla hajaumia(kama asingeumia Wazza angekuwa top scorer) its unfair kulinganisha scenario za CR7 & Wazza na huyu Daniel James

Mata,Dalot na Lingard ndio watacheza kama right winger inakaribia miaka 10 hatuna winger wa kulia .Fellaini na Herrera wameondoka hatujapata replacement so far pre-season imeanza OGS alisema anataka timu ikianza pre-season wachezaji wawe wamesharipoti

Na kama tunataka kujenga backbone mpya tunapaswa kuwa na decision makers wengine(Woodward) hawa waliopo usitegemee makubwa na timu ina kocha ambaye hana uzoefu so alipaswa kupewa msaada mkubwa sana kwenye kutengeneza hiyo timu otherwise cycle itaendelea
 
Mkuu upo sahihi upande wa decision maker na pia ni kweli hatuwezi kutatua matatizo yote msimu mmoja ila atleast wachezaji ambao tupo linked nao wanaleta matumaini.
Na pia mkuu Tusimtumie Daniel James kudefine usajili wetu msimu huu jamaa bado Sana, chukulia mfano Kama AWB jamaa katop almost stats zote kwa full back msimu iliopita, hiyo ndio level tunayotakiwa ku aim. Same kwa Bruno ambaye amevunja rekodi/kutop stats nyingi za midfield msimu uliopita, potential wise wakati tunamsajili Evra na AWB unaweza kusema kabisa AWB ana potential zaidi.
Na pia Jambo jengine kubwa ambalo timu yetu Ina miss ni work rate, tuna wachezaji wavivu Sana, Kama zamani tulivyo discuss timu yetu ni ya tatu Toka mwisho kwenye kukimbia uwanjani, Hawa wote wanaokuja ni watu wa kujituma, wata raise work rate yetu na huwenda ikawa chachu pia kwa watu Kama martial na Shaw na wao wajitume.
Hili smile tulilimiss muda mrefu Sana
 
Kwenye hoja ya kwanza nipo na wewe 100%, ni ujinga kulazimisha mchezaji abaki na wakati yeye hataki kubaki, japo timu nyingine ni ving'ang'anizi mfano Klop aliwahi kulazimisha Lewandosk abaki pale Dortmund, Bayern wakaja wakamchukua bure

Kwenye suala la pili, ni kwamba ni kweli potential na proven players wamefeli pale United. Swali ni kwamba ni bora usajili mtu kwa £50mil+ halafu a flop au usajili kwa £12mil ili hata aki flop iwe hasara ya kawaida na atafutwe mchezaji mwingine?

Na point yangu ya msingi, United hawana utamaduni wa Galacticos, na tulivyo adopt huo utamaduni mambo ndio yakawa mabaya zaidi, kwanini tusiende back to our roots?
 

Sina tatizo na AWB ni usajili mzuri at least tumesajili natural RB baada ya kuwatumia mawinga kama RB (Young & Valencia) na ukiangalia AWB ni mzuri kwenye defence na sio mzuri kushambulia still timu inahitaji right winger (haya ni matatizo ya muda mrefu) otherwise Mata/Lingard wataendelea kucheza winga wa kulia.
Siwezi kumuongelea Fernandez mchezaji ambaye hajasajiliwa na United kama kama ni tetesi basi De Ligt,Varane,Koulibaly,Saul,Longstaff,Maquire wangekuwa wanachezea United

Wakati anasajiliwa Evra was miles better player than AWB (AWB ni mwingereza while Evra Mfaransa) ambaye amecheza msimu mmoja kumbuka Evra alikuwa ametoka kucheza fainali ya Champions league against Porto na alikuwa Vice-Captain wa Monaco akiwa na miaka 23

Kama unataka kuongeza work-rate tafuta kocha mkali umeona Klopp/Pep/Poch/Zizou/Conte wanavyo kabiliana na hizo situation then mpe power against wachezaji wavivu unlike Woodward alichofanya against Mourinho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…