Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mbona Rashford aliaminiwa hivyo hivyo ?
Mkuu Rashford aliaminiwa kutokana na kukosa options kwenye mechi yake ya kwanza

Kwanza hata hakuwa rated kiivyo pale academy (kama ilivyokuwa kwa Greenwood au yule dogo James Wilson)

Ile siku timu ilipata majeruhi wengi hivyo ikabidi dogo apewe majukumu out of necessity

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
fikria hata kikosi cha real madrid kilichobeba makombe mara tatu mfululizo msingi wake mkubwa ulianza kujengwa kuanzia mwaka 2009 chini ya raisi ramon calderon aliyewasajili ronaldo, alonso, benzema, kaka, raul albiol.
baadae wakaongezwa ozil, dimaria, khedira, carvalho, varane, coentrao, callejon, luka modric, kroos, bale n.k
hawa wote wametumikia klabu takribani miaka mitatu hadi nane mbona madrid wamefanikiwa?

ndio maana nikasema hoja ya kuwa na wachezaji 18 tokea mwaka 2015 ndio chanzo cha sisi kufanya vibaya ni dhaifu.
 
Mkuu unachosema ni kweli lakini yote yanawezekana, cha msingi kazi moja ianze na nyingine inafuata

Kwa United tuna uhakika Valencia anaondoka, Herrera anaondoka, big Fella alishakwenda. Damian ni mchezaji ambaye japo hatma yake haijulikani lakini, ni mchezaji ambaye ana chance kubwa sana ya kuondoka huku Inter, Juve na jana nimesikia Valencia nao wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili.

Pia sikumbuki kama tulisajili mbadala Baada ya kuuza Depay na Blind.

Sanchez inaripotiwa anahitajika Juve, Inter na sasa wanatajwa Atletico kama mziba pengo la Griezeman

Mfano Daniel James ni hitaji la mwaka jana kusajili winger pale United hivyo the space was there already

Rojo pia anatajwa kuuzwa endapo atapatikana mnunuaji (suala lake halipo wazi, zaidi ya sisi mashabiki kutaka aondoke)

Ukweli ambao ni michungu na tunajaribu kujisahaulisha ni kuendelea kuwa na Youngy, Jones, Smalling (japo ninamuamini kama back up central defender) na Rashford kama striker tunayemtegemea. Hili ndio tatizo kubwa.

Lakini imagine, aliondoka Sanchez, Valencia, Rojo, Darmian, Herrera (japo roho inauma) jumlisha na wachezaji walioondoka bila replacement kutakuwa na free space pale United



Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu mbona umeanza kumfharau mapema?


Hivi unayohabari kuwa huyo dogo ndiyo walewale Watoto wa Malkia?
hahahahaaaa wewe acha tu,
nimesikia no new signing upande wa winga teleza
kama namuona lingard anavyocheka muda huu kwa kuletewa kipimo sahihi 😛 😛 😛
 
Lakini imagine, aliondoka Sanchez, Valencia, Rojo, Darmian, Herrera (japo roho inauma) jumlisha na wachezaji walioondoka bila replacement kutakuwa na free space pale United
ndio tunavyo ombea yafanyike mabadiliko hayo, niko radhi tushindwe kusajili mchezaji yeyote kuliko kuendelea kuwapa nafasi vilaza wa kila siku.
 
Kuna na wachezaji 18 ambao ni
Underperfoming tokea 2015 hadi leo ni kosa kubwa sana..ikiwekwa hivi je mkuu??
 
Ili swala la kusema mchezaji fulan anakipaji wakati kipaji chake hakitusaidii ni upuuzii n muda wa MAN U kusajili wachezaji sahihi kwa nafasi sahihi tena bila kujali watu wenye majina makubwa tunahitaji mashinee za kupiga kazi na kuleta mafanikio...tangu nianze kusikia sijui flan anakipaji sijui nn...United inatakiwa irudi enzi za babu fergiii anasajili mtu kwa kazi na ushindi wale kina flechaa,carrick,Neville,brown,valencia hawakuwa na vipaji lakn walipiga kazi mwanzo mwisho tukanyakuwa vikombe kazawakaza....kipaji tupia Kuku akulee
 
True..

Tunaambiwa tu Martial ana kipaji..mchezaji hata kuvuka tu goli 15 per season ni kazi..hatuwezi kumove one kwa njia hii

Inabidi tusajili wachezaji sahihi kwenye eneo sahihi..
 
Yaani kwa upande wangu ni bora tuwaondoe;

√Ashley Young
√Sanchez
√Darmian
√Rojo
√Lingard
√Jones

Then tumrudishe Tuanzebe,na kuwapa nafasi Greenwood na Chong,kuliko kuwapa hawa vilanza chansi next season
wote hao ukiwaondoa hakuna hasara yoyote tunayoipata, uongozi wa man utd umejawa na uoga wa kipumbavu.

  1. smalling hapati majeruhi ovyo ana uwezo wa kuziba nafasi ya jones na rojo
  2. ashley young, valencia, darmian nafasi zao zitazibwa na usajili mmoja tu lakini awe na uwezo wa kutumia miguu yote miwili itapendeza zaidi kama alivyo diogo dalot, faida kubwa ya ashley young ni uwezo wake wa kuziba pande zote mbili tunapokuwa na majeruhi.
  3. list yako ina waingereza watatu, ukiwaondoa hao baadae ukamleta james maddison waingereza wataziba midomo yao. maddison yupo vizuri zaidi ya jesse lingard kwenye utengenezaji wa nafasi ambalo ndio tatizo letu kubwa sana.
 
Nimesikia atletico madrid wanamtaka Sanchez kama mrithi wa AG.
 
Tusubiri tuone
 
Yaani kwa upande wangu ni bora tuwaondoe;

√Ashley Young
√Sanchez
√Darmian
√Rojo
√Lingard
√Jones

Then tumrudishe Tuanzebe,na kuwapa nafasi Greenwood na Chong,kuliko kuwapa hawa vilaza chansi next season
Mkuu nakuomba kwa heshima zote umuondoe mtumishi wa wa Bwana "Marcus Rojo " katika hiyo orodha ya wahuni wa Tandika ..



Utakuwa umenifanya kuwa na sikukuu tamu kama ukimuondoa huyo mtu kwenye hicho kichaka..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…