Manchester United (Red Devils) | Special Thread

"If you don't know where you are going, you may think any road may take you there".
 

Ni vyema umewataja wachzaji aliosajili,sasa ebu niambie alisajili beki wawili wa kati,bado msimu uliofuata alitaka tena beki wa kati,hapo ndipo nilianza kuona mwenye tatizo ni Jose.Karibu usajili wote aliofanya Jose ulikuwa hovyo,fikiria kasajili wachezaji 11 niambie yupi wa kujivunia mpaka sasa.
 
Mbona unashindwa kutetea hoja zako,umesema alisajili wachezaji wazee now umeshabadilika alisajili wachezaji hovyo
 
I doubt hata kama unamfahamu Toby tunayemzungumzia,Toby anacheza Spurs na amecheza EPL kwa misimu 5 now
2015-2016 alikuwa kwenye PFA Team of the year sijui unaizungumzia kasi ipi na hawa wenye kasi Smalling,Jones,Rojo wamefanya nini cha ajabu

Ni beki wa kawaida sana kinachomsaidia ni mfumo wa team na viungo wazuri waliopo Spurs,nakuhakikishia kama Jose angefanikiwa kumsajili leo ungekuwa unazungumza maneno mengine.Smalling & Jones walikuwa wachezaji wa team ya taifa ya England na Rojo Argentina sidhani kama ni wabaya kiasi hicho unachosema naamini majerui na mifumo ya waalimu tofauti tofauti vimechangia kuporomosha kujiamini.Bado naamini Toby si jibu la uhakika la safu ya ulinzi ya Man,naamini mifumo imara hasa kuepuka kabadili waalimu mara kwa mara kumeendeleza tatizo.
 
Smalling na Jones hata wakiitwa timu ya taifa ni wachezaji wa benchi hawajawahi kuanza kikosi cha kwanza na wako kwenye timu karibia miaka 10 ,Smalling aliwahi kucheza vizuri msimu mmoja wakati wa LVG

Rojo & Jones ni wachezaji ambao hawawezi kucheza mechi 5 mfululizo bila kuumia na ni mabeki wanaofanya many individual mistakes.Makocha wataendelea kufukuzwa until the management watakapogundua tatizo ni nini kwa sasa bado hawajagundua
 
Mbona unashindwa kutetea hoja zako,umesema alisajili wachezaji wazee now umeshabadilika alisajili wachezaji hovyo

Zlatan 35 !,sijui kama mwalimu unategemea nini kwa mchezaji mzee wa kiwango hiki zaidi ya kuwazibia nafasi makinda.

Sanchez 29 kama kuna mchezaji majanga sijaona kama huyu,kwanza kaja kuharibu salary structure na sijaona anachokifanya zaidi ya kuanguka angua uwanjani na kulalamika kwa waamuzi.

Matic 29 alicheza mwaka 1 baada ya hapo hakuna kitu akiwa uwanjani ni kama team inacheza na wachezaji 10,yuko very slow hapa sasa ndio utajua umri ni suala muhimu sana.Kwa lugha rahisi Matic umri umemkamata kisawa sawa hana mchango wa maana katika team bora McTominay mara mia mbili.
 
Toby ni mzee..unazungumzua Stats za 2015-2016 wkt tupo 2019..bro hauko serious.

Aksante Baba unajua namkubali sana Belo lakini wakati mwingine anakuwa kama Ed yaani anakuwa nyuma ya wakati sana fikiri mchezaji wa miaka 29 miezi miwili mbele 30 unataka asajiliwe !.
 
Zlatan is the most succesfully player signed by Mourinho despite his age,Sio kila mchezaji anasajiliwa aje acheze timu miaka 5/10
Kuna wachezaji huwa wanasajiliwa kwa ajili ya muda mfupi Henrik Larsson huyu hakucheza hata mechi 20 but ni mmoja ya wachezaji waliokuwa na msaada sana ule msimu.Rodgers alimsajili Milner akiwa mchezaji mzee lakini ni mmoja ya wachezaji muhimu sana kwenye kikosi chao kwa sasa

Ed Woodward ndio anayenegotiate mishahara ya wachezaji,yeye ndio alikuwa ana uwezo wa kukataa kumsajili Sanchez kama alivyogoma kusajili defender last season but alikuwa mchezaji mzuri pia alikuwa anauza jezi
 

Zlatan alicheza vizuri msimu mmoja tu,msimu uliofuta alichemsha vibaya sana,again umri hasa EPL si suala la kubeza.Ukitazama League ya Italy aina mchezo unaweza kuwa accomodate wachezaji wazee lakini si EPL.Naamini Man inatakiwa kutazama mipango ya muda mrefu kuanzia Mwl na Wachezaji naamini katika usajili wa makinda ndio suluhu ya matatizo yetu ya muda mrefu.

itazame Ajax tuliyokutana nayo fainali ilijikita zaidi katika makinda sisi tulikimbilia fainal product matokeo yake ndio haya tunashindwa kuingia top 4.Uwekezaji wa kina Pogba.......unatuumiza sana kuanzia fedha zilizotumika na baya zaidi tabia zake mbovu za kujiangalia yeye mwenyewe kuliko team ni mwendelezo wa mifano mibaya kwa wachezaji chipukizi.
 
Inawezekana tunafuatilia timu tofauti but i know Zlatan aliumia na hata fainali ya Uropa alikuwa nje na magongo msimu uliofuatia alivyopona hakucheza mechi nyingi akaondoka
 
Inawezekana tunafuatilia timu tofauti but i know Zlatan aliumia na hata fainali ya Uropa alikuwa nje na magongo msimu uliofuatia alivyopona hakucheza mechi nyingi akaondoka

Zlatan akiumia si taabu,akiumia Rojo au Jones taabu kweli kweli.
 
Mpaka magazeti yamembrand jina la THE WALKING MATIC.
 
Usajili wa Jose karibu wote haujatick sema katika hali ambayo waliikuta team ilikuwa lazima ichukue muda sana kuibadilisha.
Van Gaal aliwanunua.
1 Sergio Romero
2 Matteo Darmian
4 Daley Blind
5 Angel Dimaria
6 Memphis Depay
7Morgan shenerndalin
8 Luke shaw
9 Ander Herera
10 Radamel Falcao
11 Anthony Martial
Kati ya hao wote ni wachezaji wanne tu walionyesha angalau usajili umelipa.

Moyes aliwasajili hawa.
1King Fella
2 Mata
Angalau walionekana kuwa na maana hasa Mata msimu wa Van gaal

Mourinho aliwasajili hawa.
1 zlatan
2 mikhtarian
4 Lindelof
5 Bailey
6 Fred
7Pogba
8 Lee grant
9 Dalot
Katika list yote hii hakuna waliokaa vizuri kwenye squad hata chini ya Mourinho mwenyewe
Jose katurejesha nyuma pakubwa.
 

Mbona mnaendelea kusubiri na huu ni mwaka wa 6 sasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…