hahahahaha yan mafanikio ya Liverpool yanauma sana ila ndo tujifunze....mdani ya 3 years nadeal kibao tutaanza kwenda kwa liver pia Hahahahahaha sisi wazee wa biashara na wachezaji matozi ngoja akili ukae sawa..... Tukumbuke kipindi tunataka kumsajili Mick tulikuwa tunataka tumuangalia na mane ila tukamchagua Mick.......tukumbuke shaqiri ametoka stoke, VVD ametoka Southampton....sisi tukomae na hao Matop class tuone tutafika wapi... Inaumiza sana hata usingizi hauwezi kuja ila ndo hvyo
Ni kweli mtuu timu ya ushindani ya muda mrefu yajengwi kwa kununua wachezaji wengi au wote ambao Ni world class,
*Bei zao Ni kubwa mno kwa soko la sasa hivi
*Wengi wako kimaslahi zaidi kuliko kujitoa kwa timu
*Wengi huja kujawa na majivuno(kujiona wakubwa kuliko club/kocha/wachezaji wenzao)
Hawa wanafaa unapokuwa upo desperate kushinda taji ndani muda mfupi(msimu au wa 2)
Timu zote zinazofanya vizuri kwa muda wa Kati/mrefu, wachezaji zilionao sio wote walinunuliwa wakiwa world class, Liverpool,City, Spurs, Bayern,Barca, Ajax(wanakuja vizuri), hizo zote zimejaaa wachezaji ambao ustaa wao wameupatia klabuni, japo kunawachache Sana Ni mastaa kwa kununuliwa..,...
Hehe..lakin liverpool wamedumu na kocha mmoja mda wote huo na wameenda naye taratibu. Ina mana Mou bas asingetimuliwa et mana yule ni kocha bora pia na ni mtu mweny mafanikio sana na akishika timu, lazima ktk misimu yake kombe abebe
Mou Ni kocha mzuri wa kuleta matokeo ya haraka/ndani ya muda mfupi, Hata Ed Woodward naaamini alimleta kwa malengo hayo kuipatia utd kombe kubwa(EPL/UEFA) ndani ya msimu au wa 2, na Mou kweli Ana rekodi nzuri Sana ya kufanya hivyo/kuchukua kombe ndani ya msimu au wa 2, hata utd kapiga kazi nzuri msimu wa kwanza Europa, wa2 utd was strong EPL title contender, wa 3 Kama kawaida akafukuzwa....
Why, huwa anapata makombe kwa kununua wachezaji waliova tayari kwenye timu zingine anawaunganisha anashinda kombe, shida kuwa wachezaji Hawa wengi huwa na viburi hivyo hugombana nao baada ya muda mfupi TU hivyo yeye kutimuliwa kwa timu kupata matokeo mabaya.....
Mtizamo wangu,
*utd walikuwa sahihi kumuajiri Mou, walifanya makosa kumuongeza kandarasi, pia walikuwa sahihi kumfukuza.....
*Utd itafute director of sport/football mzuri, pamoja na kocha mzuri..
*Utd ijipe msimu 2 ya kungeneza timu kwa kufanya mpango mzuri wa kusajili(kuachana na habari ya matop player kwa sasa) ijikite kwenye kununua potential talents, kidoooooogo baadae ndo inunue top/world class kuziba mapengo machache (
Kama walivyo fanya city na Liverpool, wamekuja kununua wachezaji wa Bei ghari kuziba mapengo machache TU,(liver beki na kipa)
Otherwise, kwa ubovu wa timu ya UTD sahivi hata ikitumia [emoji386] 350m, kwenye usajili huu kwa kusafaka top/world class itambulia wachezaji 3, ambao hawataleta mabadiliko makubwa kwenye kikosi kushindana na city na liver next season, hivyo kuishia kuleta mikwaruzano na kocha na wachezaji wengine, na kuomba kuondoka mwishoni mwa msimu, Hivyo tatizo linarudi pale pale pale, Bora itumie hata [emoji386] 250m kutafuta wachezaji ambao hawaanza kuwa mastaa ila wa vipaji na wanaweza endana na falsafa ya timu, tukipata Hawa 4/5, then mwakani ndo timu ingalie mapengo yapo wapi iliyazibwe na hao top class 2/3....