Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Nyie ongeeeni yote lakini Mimi hapa ubongo ni Kama umepiga ganzi siamini kabisa kinachoendelea!Man U wa kuililia nafasi ya nne kiasi hiki?really?tunaipigania kabisa nafasi ya nne Kama tunaipigania ubingwa?kuna jamaa zangu mashabiki wa arsenal nilikuwa nawatania balaa enzi za mzee Fegi jinsi mbio zao zilivyokuwa zinabadilika ikifika february-march na kuhamishia nguvu zote kupigania top four.Yaani walikuwa wanaanza ligi kwa mbwembwe nyingi lakini ikifika kipindi hicho matumaini yao ya ubingwa yanakuwa yamepotea wanabadili gia angani.sikuwahi kuimagine Kuwa Kuna siku Kama hizi zitakuja....tunalia kabisa tumekosa nafasi ya nne!!!!!!this is sh***t!yaani pale walipo Man City na Liverpool zile mbio sisi ndio tunapostahili na sio huku mavumbini!!!!!inauma Sana hasa kwa sisi wengine tunaougua ugonjwa wa soka,naumia Sana lakini ndio hivyo napambana na Hali yangu.bahati mbaya kwangu huwa nashindwa kujizuia kuangalia mechi za man u,yaani tunapigwa Kama siku ile na everton mtu unajiapiza siangalii Tena mechi ya man u lakini ikifika siku anacheza unakomaa dakika ya 15-20 huyo kwenye kideo na tabasamu la kuvizia!Cha Moto nakiona......lakini nitabaki kuwa RED FOREVER.
 
Pole sana brother umeongea kwa uchungu sana,lakini hamna namna haya ndiyo maisha ya soka lolote linaweza tokea,tulikuwa tumeisahau futui sasa tunarudi tena huko huko kuungana na malafiki zetu Asernal.
 
Naona umeamua kukimbia kabisa
 
Pole sana brother umeongea kwa uchungu sana,lakini hamna namna haya ndiyo maisha ya soka lolote linaweza tokea,tulikuwa tumeisahau futui sasa tunarudi tena huko huko kuungana na malafiki zetu Asernal.
Arsenal tunahamishia majeshi Europa kulibeba,

Futuhi mtaenda peke yenu
 
Arsenal nae kishapoteza CL, anategemea spurs afungwe magoli mengi na yeye ashinde magoli mengi ili amzidi Spurs kwa GD. Kitu ambacho si rahisi kutokea. Chelsea amesha book CL na ubovu wao wote.
Mbona mna conclude mapema,

Hivi hamjui alhamis nakata tiketi ya kucheza final ya Europa ,hivo napitia mlango WA unai,
 
Mbona mna conclude mapema,

Hivi hamjui alhamis nakata tiketi ya kucheza final ya Europa ,hivo napitia mlango WA unai,
Usijipe moyo pasipo na natumaini, tupeane pole, tujipange Europa. Ila ki ukweli mechi za alhamisi huwa zinanikera sana.
 
Usijipe moyo pasipo na natumaini, tupeane pole, tujipange Europa. Ila ki ukweli mechi za alhamisi huwa zinanikera sana.
Nisijipe moyo kivipi, ikiwa alhamis naenda kukamilisha ratiba kwenda Baku kwa fainal ya Europa?

Wewe una hiyo chance ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…