sina uelewa mkubwa sana wa masuala ya mpira hususani kwenye tactics kama wengineo lakini miaka yangu yote tokea niifahamu manchester united nikiri ya kwamba manchester united hatujawahi kuwa bora kwenye kumiliki mpira kwa kiwango kikubwa sana kama timu nyengine mfano zile zinazotoka Hispania, Germany (bayern munich).
kama nitakuwa nipo sahihi manchester united ndio timu kubwa pekee ambayo bado imeshikilia falsafa za kiingereza huku timu nyengine mfano liverpool na man city wameshaachana kitambo na mpira wa kiingereza wa kuziba nafasi nyeti kwenye maeneo ya hatari (
Space Oriented Zonal Marking). Ni mfumo ambao nimeushuhudia kwa miaka yangu yote ya kuishabikia manchester united tokea mwaka 2001 ukitupa faida kubwa sana hususani tunapokutana na timu zenye uwezo mdogo sana wa kumiliki mpira kama zilivyo timu za uingereza lakini tunapokutana na timu zinazo dominate possession na counter pressing tunapata tabu sana na kwa ushahidi wa hilo jni pale tunapokutana na timu za spain na hata timu ya taifa ya uingereza bado ni waumini wa style hii ya kiuchezaji.
Ili uweze kudominate possession mara kwa mara unapaswa kwanza umdhibiti adui kwenye eneo lake la kujidai kitu ambacho manchester united hatufanyi mara kwa mara labda tuwe kwenye situation ya kutafuta magoli kama ilivyokuwa kwenye mechi yetu ya southampton au kuna mechi fulani mwaka 2008 tulikwenda half time tukiwa nyuma kwa magoli mawili dhidi ya spurs ya darren bent, lennon, pavlyuchenko n.k, ukija upande wa wapinzani wetu wakubwa kama liverpool na manchester city wao wanaanzia kukaba juu ndio maana ukiangalia mechi zao unakuta eneo la kati kati wapo wengi hivyo basi inakuwa ni vigumu kwa timu pinzani kufika maeneno yao ya hatari na hata wanapopoteza mpira wanarudi kwenye maeneo yao kwa haraka sana, ndio maana mechi ya guardiola na klopp inakuwa ni ngumu sana kwa pande zote mbili.
kama hatuwezi kuachana na utamaduni wetu wa soka la kuziba maeneo yetu ya kujidai basi atleast wachezaji wetu wanapaswa wabadilike kifikra na kiuchezaji ndipo baadae tuelezekeze shutuma kwa kocha na benchi lake la ufundi, msingi mkuu wa kuhakikisha timu inakuwa na umiliki mzuri wa mpira unapaswa uanzie eneo la ulinzi ndio maana guardiola alipotaka kuingiza falsafa yake ndani ya manchester city alianza kurekebisha eneo la ulinzi hivyo basi na sisi tunapaswa kuliangalia kwa jicho la tatu eneo letu la ulinzi kwa kuanzia golikipa.
Tuna golikipa mzuri sana linapokuja suala la kuokoa michomo ya magoli lakini ukigeuza sarafu utagundua ya kwamba kwa timu kubwa za uingereza (man city, liverpool, chelsea) sisi ndio tuna golikipa muoga wa kucheza ukilinganisha na hao niliowataja. mipira mingi anayoianzisha
david de gea ni ile ambayo yupo kwenye presha ndogo sana, pengine safu yetu ya ulinzi ndiyo inamfanya david awe mzito wa kuanzisha mipira mara kwa mara bila ya kuwa na khofu yoyote. ukiwaangalia makipa kama
ederson, allison, ter stegen, buffon, arrizabalaga, manuel neur wote hawa wanazidiwa na david degea kwenye saving lakini wanamzidi kwenye kucheza.
Josep guadiola hakumuondoa
joe hart kwa sababu ni mbovu bali alimuondoa kwa sababu hii ya kutokuwa na uwezo wa kucheza hivyo basi david degea anapaswa aende na wakati kama wenzake. ukiangalia ukuta wa juventus nyakati zile ulikuwa unaundwa na walinzi wasiokuwa na degree yoyote ya skills mfano chiellini, barzagli, bonucci, lichsteiner lakini cha ajabu unamkuta buffon anaanzisha mipira hata kama adui yupo karibu.
smalling, young, jones, darmian:
utawezaje kumiliki mpira kwa kiwango cha 60 - 70% kila mechi ikiwa mchezaji wako wa kikosi cha kwanza ni ashley young ambaye kila mechi anayocheza lazima apoteze mipira kipumbavu zaidi ya mara 5 kwa kupiga long pass zisizo na uhakika na mara tano akiwa out of possession ya kuanziwa mipira kama wanavyofanya walinzi wengine mfano wa jordi alba, walker, robertson, pique n.k.
ndio maana nawapenda sana manchester city na sera zao za kuendesha timu kwa sababu kocha mpya anapokuja anapewa uhuru wa kufanya anachokihitaji tofauti na sisi, timu yetu imejaza wachezaji wazito wanaoshindwa kufanya maamuzi ya haraka hata kama wapo under pressure, ndio maana tunapokutana na timu bora mfano wa juventus, barcelona, liverpool, man city tunaishia kudhalilishwa kimpira japokuwa tunapata ushindi, wachezaji kama ashley young, smalling, jones hata kama utawapeleka barcelona hawezi kubadilika tena kimpira kwa sababu wao wenyewe hawataki kubadilika kiuchezaji.
unapomuangalia gerrard pique jinsi anavyojiamini halafu unamuangalia smalling utafikiri mmoja kati yao amezaliwa na miguu minne kumbe wote ni sawa kihuduma wanazopewa na klabu zao. Ili tuimprove kwenye kumiliki mpira ni lazima eneo letu la ulinzi liundwe na wachezaji mfano wa lindeloff, shaw na hata eric bailly linapokuja suala la ubunifu na si nguvu.
marcus rashford, mctominay, sanchez, martial
kwa ufupi wachezaji wengi wa kiingereza tabia zao zinafanana kiuchezaji kwa sababu ni wazito wa kuomba mipira tofuti na ilivyokuwa kwa
paul scholes nyakati zake vile vile ukiangalia timu yetu kwa sasa tuna wachezaji takribani 6 ambao viwango vyao vinategemea na jinsi wanavyoamka.
kiukweli napenda sana kumuona rashford akifanikiwa kwa sababu ametoka kwenye damu ya manchester united lakini baadhi ya nyakati haeleweki anapomiliki mpira anakuwa ovyo sana utafikiri uwanjani anacheza na mbuzi. mimi nadhani kwanza waingereza waache kumjaza sifa za kumuaminisha ya kwamba uwezo wake anaweza kumfikia ronaldo, kabla hajafikia level za ronaldo ajaribu kwanza kufikia level za andy cole mmoja kati ya washambuliaji waliokuwa wanakupa faida kubwa sana kwenye eneo la ushambuliaji hata kama hafungi magoli.
kama nilivyosema mwanzo hata nyakati za alex ferguson tulikuwa hatumiliki mpira kama manchester city ya guardiola au chelsea ya maurio sarri kwa sababu si utamaduni wetu, tulichokuwa tukikifanya ni kumiliki mpira kwa kiwango cha wastani huku tukishambulia kwa posession, kwa ufupi ulikuwa unafahamu ni wapi movement za kutengeneza magoli zinaanzia na wapi zitaishia ndio maana safu yetu ya ushambuliaji ilikuwa na uwezo wa kufunga na kutengenezeana magoli mengi kupitia maeneo tofauti ukilinganisha na nyakati hizi ambapo tunategemea zaidi miujiza ya upande wa kushoto.
lakini pia kama umiliki wa mpira ni muhimu sana basi nyakati za LVG tulikuwa tunamiliki mpira kwa kiwango kikubwa lakini hatukuwa na mipango imara ya kushambulia ndio maana si ajabu kukuta mechi nyingi tuliishia kutoa suluhu. jambo muhimu ni kuhakikisha tunapokuwa na mpira adui anapaswa kuwa na pressure kubwa ya kufungwa na si kuwa katika hali ya kumfanya adui arelax kama kilichotukuta kwenye mechi zetu dhidi ya juventus na PSG uwanjani kwetu.
ball possession ni muhimu sana lakini bila ya kuwa na mipango imara ya kutengeneza nafasi na kujilinda tutakuwa hatuna tofauti na manchester united ile ya LVG au arsenal ya wenger.
kwa hili la kuwa na possession ndogo kwenye mechi kubwa tumhukumu ole msimu ujao ndio itakuwa ni muda sahihi zaidi kuliko wakati huu ambao ameikuta timu bila ya kuongeza chochote.