nadharia yako ipo sahihi kwa 75% kwa uoni wangu dhaifu wa kibinadamu, tukija upande mwengine wa sarafu unaweza ukajipa imani ya kwamba labda klabu imeamua kumpa mkataba mpya ili kuepuka dirisha lijalo asiondoke klabuni akiwa huru jambo litakalopelekea klabu kushindwa kutengeneza faida yoyote ya kifedha na kwa ushahidi wa hilo tujaribu kurejea dili la mkataba mpya la
marouanne fellaini mwanzoni mwa msimu, miezi nane baadae klabu ilitengeneza takribani paundi millioni 11 kwa mauzo yake.
tuachane na mambo ya faida na hasara ambayo hayatufaidishi chochote sisi wapiga debe tunaoshindia chapati, kwangu mimi suala la kupewa mkataba mpya kwa
phil jones mwenye rekodi mbovu za majeruhi pale klabuni nimelichukulia kama ni ujumbe mzito unaotumwa na CEO ed woodward kwa wadau wote wa manchester united,
- maarifa yangu yaliojaa udhaifu yananilazimisha niamini ya kwamba ed woodward anaamini ya kwamba ni bora zaidi uendelee kumhudumia phil jones (injury prone) kwa miaka 5 zaidi ndani ya klabu kuliko kulipa paundi millioni 40 au zaidi kwa dhumuni la kutafuta mlinzi mpya wa kati.
- ed woodward anaendelea kusimamia msimamo wake ule ule wa mwanzoni ya kwamba hana mpango wa kusajili walinzi wawili wa kati kwa msimu mmoja kama yalivyokuwa madai ya jose mourinho nyakati za utawala wake, hivyo basi ameona ni bora ampe kandarasi mpya phil jones mwenye rekodi zisizoridhisha juu ya afya yake halafu baadae dirisha lijalo ndio atafute mlinzi mmoja wa kati baada ya kelele kuwa ni nyingi.
- lakini kabla hajaingia sokoni kutafuta mlizni mmoja wa kati ni lazima atafute mwanadamu wa kumtoa sadaka pale klabuni ili kuziba mwanaya wa matumizi ya mshahara na tayari tumeshuhudia kupewa mkataba mpya kwa walinzi wawili wakati ambao ni chris smalling na phil jones.
- Kwa performances zinazoonyeshwa na victor lindeloff pamoja na eric bailly sioni dalili ya watu hawa wawili kutolewa sadaka hivyo basi mwanadamu pekee mwenye asilimia kubwa ya kutolewa sadaka ni marcos rojo, mashabiki wa yule muhuni wa Kiargentina munapaswa mujiandae kisaikolojia kuanzia muda huu na wale wenzangu na mimi team phil jones tukutane hoteli ya kempinski ili tujiburudishe na vinywaji vilivyojaa ladha ya nemanja vidic.
wakti tukiendelea kusherehekea pale kempinski tutapaswa tuangalie upande mwengine wa hoteli ilio jirani yetu ambayo meneja wake mkuu
josep guardiola ambaye backup yake inaundwa na
vicent kompany pamoja na
otamendi ameshaanza kuonyesha dalili ya kutokutaka kuendelea kufanya kazi na wanadamu wawili hao huku sisi wengine tunawang'angania jamii ya
phil jones, lovren na
matip.
Solskjaer on Jones' new deal :
“Phil knows what it takes to be a Manchester United player, he has won the Premier League, FA Cup and Europa League and is now one of the senior players within the team.
“He is coming up to his 27th birthday and entering into his prime years as a centre half. We are delighted Phil has committed his future to the club.”
- ole gunnar ameyazungumza maneno haya kama nani?
- nakusudia je amehusika kwenye mazungumzo ya kupewa mkataba mpya kwa phil jones haliyakuwa ana miezi miwili tu tokea aanze kazi?
- kama hakushirikishwa kwa nini ameamua kuzungumza stori isiyomuhusu, wakati upande wa pili maurizio sarri alinukuliwa akisema ya kwamba hafahamu chochote kuhusiana na usajili wa pulisic kutoka dortmund?
- kama ishu ni kuifahamu timu basi hata antonio valencia anastahili kandarasi mpya, hivi kuna mwanadamu anayemshinda antonio valencia kwa kutumikia muda mrefu pale klabuni?
- je inawezekana maneno ya OGS juu ya phil jones ni tafsiri tosha ya kwamba jamaa ndiye kocha mpya wa manchester united anayesubiriwa kutangazwa na ndio ameshaanza kazi rasmi ya kujenga timu kwa ajili ya msimu ujao?
- kama sivyo kitatokezea kitu gani endapo kocha ajae atawakataa wachezaji aina ya ashley young, phil jones, smalling haliyakuwa wote wameshapewa kandarasi mpya?
- je inawezekana ed woodward anatudanganya pindi anapodai ya kwamba manchester united ina uwezo wa kumsajili mchezaji kwa gharama yoyote bila ya kuleta athari yoyote ya kifedha ndio maana ameamua kukimbilia kuwapa mikataba mipya wachezaji aina ya smalling, jones, young, mctominay kwa sababu hatuna uwezo wa kutafuta wachezaji watano au zaidi kwa dirisha moja kwa ajili ya kuziba nafasi zao ?
- hivi tuna uhakika gani kama ujio wa football director utaondoa matatizo ya klabu kwenye ishu za usajili wakati kisheria mwenye mamlaka ya kimaamuzi bado yatabaki kwa ed woodward ambaye ndiye CEO?
View attachment 1017691