Kieran trippier na davies walikua wanapanda kuja kuchezea juu kabisa ya mstari wa kati, hapo ndipo tulipotumia advantage ya martial na rashford pembeni ili kutumia mwanya wa kuwa alone kwenye flanks,
Rashford anaanzaga kati kama striker, lakini jana alicheza sana kulia na kushoto, lingard akatokea sana kati,
Angalia chances zote tulizopata, hakukuwa na defender wa spurs wa pembeni hata mmoja karibia kila chance,
Ilikua ni moja kwa moja either martial/rashford vs /vertonghen/toby,
Yani wings zetu zinapopata mpira zinafika moja kwa moja chumbani, sebule ya spurs hakuna mtu,
Angalia chance ya goli letu, angalia space aliokua nayo rashford, angalia davies alipokua, angalia wakati tripier ana-misplace pasi aliipotezea katikati kwenye mstari kabisa,
Rashford anapata pasi ya pogba, yuko moja kwa moja against last defender,
Angalia nafasi ya martial aliopiga kipa akacheza na miguu, alikuwa peke yake moja kwa moja against toby, anamchukua anapiga,
Angalia mpira ambao martial alishindwa kuucontrol ule, ilikua yuko peke yake against last defender,
Christian Erricksen alikua ana ochestrate game sana pale kati, karibia chances zote za spurs zilitoka miguuni mwa erricksen, kwenda straight kwa kane, kwenda kwa delle, kwenda kwa trippier apige krosi,
Sissoko alikuwepo kama engine ya kukokota mipira nyuma adi mbele, driving ya timu,
Lakini bado kwa technique waliokuja nayo spurs, hawakuchagua kuheshimu pace ya united iliopo kwa wale watu watatu wa juu na uwepo wa pogba chini yao ambae anaweza akapiga accurate pass pengine kuliko wengi pale Epl,
Waliamua bado kupeleka watu juu,
Naweza mlaumu potchetino kidogo,
Na hapa ndipo ninapoona potchy sio kocha mwenye mbinu za ushindi,
Unacheza na timu yenye pace kwenye counter, na umejaribu mara nyingi kupiga mashuti wanablock pale kati, beki wamejaa sana kati, kwanini usiwatanue pembeni???
Mipira mingi ya trippier kupitia pembeni ilikua na hatari zaidi kuliko, either ikisababisha rebound mbovu, au poor clearance, au direct header, ni wazi phil jones hawezi mdhibiti harry kane hewani, alizidiwa movement na harry kane, header zote za harry kane vs jones, kane aliwin header zote, hakuna clearance hata moja aliofanya jones vs harry kane,
Hata game iliopita ndio ilikua hivyo hivyo, alifunga mbele ya jones,
Game hii jones anapotezwa kila muda na kane, kane anapiga free header,
Sasa kwanini usiwafungue united ukamvuta lindelof pembeni?? kati akabaki jones ambae hawezi kummudu kane, ukapiga krosi ndani, kwanini usimlete son heung min akaja kulia, na lamela akaenda kushoto, ili kufungua defence ya united?? amekomaa kulazimisha son avunjie ndani kutokea kushoto ambapo kila akiingia anakutana na young na herrera pamoja, kule napo lamela kila akivunjia ndani anakuta watu wamesimama shaw na matic wameziba njia za mpira,
Lakini kama angechagua kwenda wide, ina maana angekutana na young pekee, kwa technique ya son au lamela wanaweza kupiga krosi juu, kwenye box la united kumejaa pogba na matic ambae hawapigi header haijalishi urefu wao, kuna herrera mfupi, shaw mfupi, jones ambae hamuwezi kane, sana sana lindelof tu,
Kitu kingine davies alikua hafanyi overlap kama trippier, aliishia sana kucheza pasi badala ya cross ins, kama ange overlap pengine nayeye angeleta madhara,
Ila alichokifanya potchy ni kuongeza pressure again and again akiamini tutashindwa kuhimili presha, anaingiza llorente anakua na double striker, lakini hawa wanaenda kucheza pale pale ambapo united wamejaa golini, mipira inaishia kugongana gongana tuu miguuni,
Ulishwahi kujiuliza kwanini leroy sane na umahiri wake wote na ufungaji wake, bado anacheza kushoto?? kwanini asitokee kulia ili alione goli vizuri??
Sababu anapofungulia kushoto mara nyingi anamfosi beki wa pembeni afungue pembeni zaidi hadi mwisho wa uwanja, ina maana lazima beki wa kati aje kuziba hii nafasi hapa, asipokuja basi mchezaji mwingine wa city anaingia kukaa pale, beki akija anatoka anaenda kukaa alipotoka beki yule, beki za kati anazivuta pembeni akina aguero na wenzie wanapita nyuma ya beki alipotoka,
Sent using
Jamii Forums mobile app