Kwa Kiasi kikubwa yamepungua Kama Sio kuisha yote.
Tatizo lilikuwa uwepo wa Mourihno.
Licha ya kutupa Kombe la UEFA Ndogo na kuturudisha Katika nne bora kushiriki kucheza UEFA.
Soka lililochezwa uwanjani halikuwa la kuvutia, timu ilicheza Mpira mbovu mno, haikuwa Man United tuliyoizoea Au kuitegemea.
Wachezaji walilalamika, Mashabiki tulilalamika, binafsi sikuwa Mpenzi wa soka la Mourihno hata Kidogo.
Tulipishana Katika Falsafa, Mi ni muumini wa soka la Ufundi na uwazi, la kushambulia kwa Kasi na wachezaji kuwa huru kuonyesha uwezo wao binafsi.
Soka la Mourihno lilijaa mbinu ngumu mno, Falsafa ya kukaba Muda wote Ndio iliyotaka kuwapoteza wachezaji wazuri.
Mikhtaryan ameflopy kwa sababu ya Mou, Rashford alilazimika kutumia Nguvu nyingi kuliko akili uwanjani, Martial ye yalimshinda akaanza kulalama sambamba na Pogba.
Tatizo lilikuwa kwa Kocha (Mourihno), wachezaji walilalamika kuhusu Mbinu zakena mifumo aliyotumia uwanjani.
Tuliowaona hata Ma legend wa timu wakikosoa Mbinu zake.
Alitengeneza uwadui kwa Wachezaji na kwa Ma Boss wa Timu, vyombo vya Habari.
Mourihno alikuwa kivuruge Kweli Kweli pale Carrington na Old T.
Alitunyima radha ya kuwa shabiki wa Man United.
Zaidi hakutaka kuziishi Falsafa za Man United, kuwa pale Old T inaanza Man United kisha SAF.
Alitaka kuwa zaidi ya Klabu.
Alitumia zaidi ya pound 400m kukisuka kikosi chake.
Hakuwa Manager Mzuri kote alipopita, Pale Real Madrid pia ilikuwa hivihivi.
Hizi ni timu kubwa zenye mashabiki wa kutisha zenye Falsafa zake.
Alishindwa kutofautisha Kati ya Man United/Rwal Madrid na Chelsea.
Na hata alipokuwa Darajani alikumbana na matatizo ya namna hii.
Sio Muumini wa wachezaji wenye vipaji/Makinda na Sio Muumini wa wachezaji Mastaa, alishindwa kubalance timu/Club.
Kuondoka kwa Mourihno pale Man United kumekuwa na Kheri kubwa kuliko angeendelea kuwa Kocha wetu.
Huyu Mourihno Ndio aliyetaka kutuaminisha hawa akina Mata, Lukaku, Salah, De Burnye, Sterrling kuwa Sio wachezaji wazuri.
Kwangu naamini kumfukuza Mou Klabu imeshusha Mzigo mkubwa sana.
Chini ya OGS hatuwezi kushinda match zote lakini match ambazo tunatakiwa kushinda nina uhakika tutashinda kwa Kishindo Sio kwa kinyonge kwa soka tunalocheza sasa.
Tulianza kufungwa na wajinga wajinga tena hapa hapa Old T.
Tukaanza kuvihofia hata hivi vitimu vidogo, tufungwe na timu Ndogo lakini iwe kwa bahati mbaya, tulikuwa tunafungwa kwa Shida hata Kama hatuchukui ubingwa.
Tulianza kudharaulika, lakini Sasa nina imani hata PSG wataanza kutuchukulia kwa umakini.
#Kheri ya Mwaka Mpya.
Matatizo ya United hayajaisha ingawa kuna improvement kubwa on the pitch ndio maana still kuna proposal ya kuwa na position ya Director of Football kupunguza confusion between executive(CEO+Owner) na technical (manager+players) to allign club philosophy which was missing since post SAF era .Makocha wote waliopewa timu baada ya SAF hawakuanza vibaya so its too early kuanza kushangilia mistake aliyoifanya Woodward ni kumpa kazi Mourinho akidhani labda atabadilika na biggest mistake ilikuwa ni kumuongezea mkataba.
Sent using
Jamii Forums mobile app