D A E M U S H I N
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 22,633
- 121,022
Happy Independence Day
- uhuru kwa andreas perreira kutoka namba 6 hadi namba 11 japokuwa alichezeshwa kwa dakika 7, ni matumaini yangu benchi la ufundi litaendelea kumtumia kama kiungo mshambuliaji.
- uhuru kwa walinzi wetu wa kati angalau jana walifanikiwa kupumzika, unapolinda kwa njia ya kushambulia hata kama beki wako wa kati ni Damushin basi ataonekana hodari kuliko thiago silva wa AC MILAN.
- uhuru kwa benchi la ufundi, inaonekana dhahiri michael carrick na mwenzake mckenna walikuwa hawafurahishwi na kitendo cha jose mourinho kumchezesha andreas perreira kiungo mkabaji, ni ngumu kuamini kama yale mabadiliko aliyafanya solskjaer haliyakuwa mechi za manchester united alikuwa hazifuatilii kwa kiwango cha standard gauge.
- kwa mara ya kwanza nimeshuhudia kocha wetu akiingia uwanjani kuwapongeza wachezaji wake na kwa mara ya kwanza nimeshuhudia kocha akiwasifia wachezaji na si kujibebesha sifa yeye kwa asilimia kubwa.
- ngoja nicheke kwanza : kwa mara ya kwanza muheshimiwa radika na timu yake wanazungumza lugha moja na muheshimiwa Daud1990 na timu yake
- nilishazoea kuangalia mechi ya manchester united tukicheza dakika 30 bila ya kupiga shuti goli la wapinzani lakini jana ilikuwa ni tofauti, tumepiga mashuti 17 na mashuti 9 yalilenga goli.
- kuna tofauti kubwa kati ya kumiliki mpira bila ya kufanya chochote na kumiliki mpira huku timu ikionyesha harakati za kutafuta magoli, nyakati za van gaal tulikuwa tunamiliki mpira kuliko AJAX lakini baada ya dakika 90 tunapata suluhu. Jana timu ilimiliki mpira 74% na timu ilionyesha harakati za kutafuta magoli.
- dah! namuonea huruma sana fred, kwa mpira huu wa kugusa mara moja unamfaa sana lakini wapinzani wake nao pia ni wabaya sana, ni matumaini yangu uhuru wa jana utaturudishia rotation kama ilivyokuwa nyakati za fergie
ni mjinga peke yake ndiye atakayekuwa na matumaini ya kwamba tutashinda kila siku, kwangu mimi haiwezekani kwa sababu mpira una matokeo matatu. Tulichokuwa tunakitaka mashabiki wa manchester united chini ya jose mourinho ni mpira wenye kueleweka ambao utatoa uhuru kwa wachezaji kujisikia furaha kufanya kazi walioichagua maishani mwao, na hata kama itatokezea tupo nyuma kwa magoli dhidi ya wapinzani wetu basi ionekane morali ya kutafuta ushindi na si kudhalililishwa na wapinzani wetu kama walivyotufanyia liverpool na manchester city.
wanasema tumewafunga cardiff FC, ok wapo sahihi na tunawashukuru wapinzani kwa kutukumbusha ya kwamba tumeifunga timu iliyo nafasi ya nne kutoka chini na ni matumaini yangu familia ya manchester united haitabweteka na ushindi tulioupata jana bali itakuwa ni chanzo cha kuendeleza wimbi la ushindi dhidi ya huddlesfield town siku ya jumatano.
Kinachonikera ni kwamba jose mourinho ameiacha timu tukiwa nyuma kwa pointi 11 dhidi ya wapinzani wetu watatu ambao wanawania nafasi 4 za juu kama sisi, kama tungeliweza kumfukuza jose mourinho mechi dhidi ya west ham united basi muda huu tungelikuwa tunawania nafasi ya 3, cha ajabu jose mourinho ameondoka na fedha zetu na pia anaelekea kuondoka na nafasi yetu ya 4.
wapinzani wetu muda huu baada ya ole gunnar solskjaer kuingizwa dakika za majeruhi, cha ajabu wametupita kwa point nyingi lakini wameanza kuweweseka kama mzee wa ujasiriamali, sijui kwa kiingilishi linatamkwa vipi kiutani.
