Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Achana na hao akina Valence na Young ni shida nao.
 
Hao ndo nyota wenu ulitaka nani acheze.
 
Guendo ametawala kati? Hivi mimi na wewe tumeangalia game mbili tofauti. Dogo amepoteza mipira mingi sana

United kipindi cha pili hawakutengeneza nafasi? Nadhani hii mechi hukuiona, bali umesimuliwa. Goli la pili liliingiaje? Vipi kuhusu ile faulo aliyocheza Toreira kwenye penalty box mpaka akaumia? Embu niambie nafasi mlizotengeneza nyie.
 
Hii mechi ilikuwa ya valencia over dalot mata over lingard na fred angafanyiwa sub
Yap Valencia alipaswa kuanza, hakuna ubishi kuhusu hilo. Kuna wakati ni ngumu sana kumuelewa Jose, anamuacha Dalot nje mechi kama ya Southampton (apate uzoefu kwanza) na badala yake anakuja kumuanzisha mechi ya Gunners, mechi yenye pressure kubwa.

Kwa Lingard nipo tofauti na wewe mkuu. Man Utd game plan yao ilikuwa kucheza game yenye high tempo, kutompa adui nafasi ya kupumua (kwa dakika 15 za kwanza tulifanikiwa). Mata ni mzuri sana, lakini sio mkimbiaji, sio mtu wa ku press adui na ni mstaarabu sana hata sio mtu wa kucheza technical fouls.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…