Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mimi pia siyo muhumini wa fukuza fukuza haijengi kabisa zaidi inawapitisha kwenye kipindi cha mpito kila mnapo leta mwalimu mpya
Kabisa juzi giggs ukifukuza kesho unarud palepale ulipopaacha hupig hatua maana kila mtu anakuja na project mpya
 
hakuna timu isiyofungwa issue ni kwamba unafungwaje?? unafungwa kwa uwezo au uzembe that's all
 

Pogba anatoa assist za maudhi sana. Nikikumbuka ile ya Fred na hii aliyompa Martial jana ni hatari sana.

Yani ungelijua jinsi hii post yako inavyowapa hasira Washabiki wenzio ambao Ni Mo-Out Hata usingeliiandika.
 
Yani ungelijua jinsi hii post yako inavyowapa hasira Washabiki wenzio ambao Ni Mo-Out Hata usingeliiandika.
Haha,mkuu hatuna budi kuishabikia timu tu,maana hata nikijaribu kuombea ifungwe ikifungwa bado roho inauma.

Mimi pia sipendi mbinu zake za uwaziri wa ulinzi,na kutowaacha wachezaji waonyeshe vipaji vyao. Jana nadhani ndio aliwaambia wakapambane wawe huru kipindi cha pili.

Vipi lakini,leo unapona kweli?Kuna fundi anaitwa Bernardo Silva, hatari sana.
 
Wakuu Mimi bado naamini Mou hatufai eti only because amemfunga Newcastle nitembee kifua mbele never.... Angalieni arsenal anachezaje hulk ndo mje mtetee hijacked zenu.... game 8 zijazo tutajua nani yupo sahihi humu
 
Mashabiki wa man u jf ndio wanaotaka special one aondoke ila mashabiki wa man u theater of dream wanataka Ed awe responsible. Naendelea kuona tofauti ya mweupe na mweisi
Wote ni mashabiki na tuna uhuru wa kuchagua na kuamua..huwezi kwenda hovyohovyo kama ling'ombe eti kisa unawafuata wazungu..huo ni upopoma..morinho aondoke united!!
 
Mkuu..kumfamanisha morinho na Sir.Alex Ferguson ni upuuzi..najua unampenda huyo jamaa ila huu ni upuuzi..morinho amekaa utd kwa miaka 3 ila fergie amekaa zaidi ya miaka 20..nashangaa sana unavyotumia hiyo post kama kigezo cha kumtetea huyu morinho
 
Wakuu Mimi bado naamini Mou hatufai eti only because amemfunga Newcastle nitembee kifua mbele never.... Angalieni arsenal anachezaje hulk ndo mje mtetee hijacked zenu.... game 8 zijazo tutajua nani yupo sahihi humu
Ukweli mtupu..subiri baada ya mechi mbili tatu uone..majivuno yataanza na mambo ya kukosoa wachezaji hadharani nayo yataanza
 
baada ya takribani wiki mbili za majonzi na dhihaka kupita angalau jana pro mourinho walilalala kwa furaha na amani iliojaa kwenye nafsi zao wakiongozwa na manahodha wao radika na Cole Williams ambao wameonyesha msimamo usiyoyumba kwa kile wanachokiamini, hahahahahaaaaaa hongereni sana pro jose mourinho ila musisahau vita hii ngumu ndio kwanza inaendelea na kwa wale tunaopuliza pande zote mbili acha tuendelee kufurahia comeback ya ukweli ilio onyeshwa na vijana kwa siku ya jana.

Nafahamu ya kwamba muda huu anti mourinho wote wamekata moto kwa kiwango fulani lakini musiwe na khofu wiki mbili zijazo kuna balaa la chelsea, juventus na manchester city. Kama atachomoa mechi hizi tatu basi wapinzani wa jose mourinho nyote kwa pamoja mutalazimika kumtafuta haraka haraka wa jose mourinho anayepatikana humu JF kwa dhumuni la kuunga mkono juhudi za jose mourinho.
Naamini pande zote mbili muda huu zinasubiri kwa hamu ifike January 2019 kwa sababu:-
  1. ed woodward atafanya kila njia ajiondoe kwenye huu mtego alionasa uliowekwa na jose mourinho na wafuasi wake ambao hadi jana pia tuliwaona uwanjani wakimponda, hivyo basi atahakikisha dirisha dogo la usajili anatafuta japo wachezaji wawili.
  2. jose mourinho kiupande wake itakapofika mwezi january hizi kelele zinazoendelea zinazotaka afukuzwe zitazimika ghafla kama mshumaa pindi upepo unapovuma, pengine huenda ikifika mwezi january tutakuwa tupo nafasi angalau ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu (tuombe hivyo inshaallah) jambo hili litazidi kuchochea kushuka kwa presha inayomkabili mourinho na wachezaji wote muda huu.
nadhani njia pekee itakayoweza kuondoa mvutano uliopo kati ya pande mbili hizi ni kuhakikisha tunamaliza nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu ili tupate nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa msimu ujao tupate kujipanga na msimu unaofuata bila ya hivyo jose mourinho atawajibika na hata ed woodward atapaswa kuwajibika.Tukiachana na vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea muda huu kwenye klabu turudi tena kwenye mechi ya jana

hivi hili suala la wachezaji wetu kupoteza mipira ovyo wanapofika kwenye maeneo ya adui tatizo ni mbinu za kocha au wachezaji wetu kukosa ubunifu wa kutosha?

  • ukiziangalia timu kama barcelona, manchester city, liverpool na hata real madrid ya msimu uliopita wanapofanya mashambulizi ni nadra sana kukuta wanapoteza mipira ovyo haijalishi timu pinzani wameweka ukuta wa chuma lakini kwetu sisi ni tofauti kabisa, ndio maana imekuwa vigumu sana kiupande wetu kuifunga timu pinzani magoli zaidi ya matatu kwenye mechi kwa kukosa kwetu umakini. marcus rashford, romelu lukaku, martial, alex sanchez hawa watu inafika nyakati wanakufanya utamani kuangalia mbio za farasi kuliko mpira wa manchester united, kasi yetu ya ufungaji wa magoli inazidi kupungua siku hadi siku.
waheshimiwa mumeionaje formation ya 1- 2 - 4- 3
kwa mtazamo wangu mimi nadhani ni bora zaidi kutumia formation hii tunapocheza na hizi timu ndogo zisizokuwa na viungo wabunifu hususani tukiwa uwanjani kwetu kuliko kutumia formation ya kujaza walinzi 6 kama alivyofanya jose mourinho kwenye hizi mechi tatu za mwisho.Timu nyingi za uingereza ukizichezea mpira wa kushambulia kidogo tu zinachanganyikiwa na hatimaye huishia kujilinda, makocha kama guardiola, sarri ball na klopp kwa kiasi kikubwa wameutumia udhaifu huu wa timu za uingereza kwa kuhakikisha wanaweka nguvu kubwa kwenye kushambulia kuliko kujilinda zaidi.
unapocheza na hawa wazembe kama mark noble, shelvey, lallana, gana idris na huku unajilinda ni ujinga zaidi ya kulala na kahaba bila ya kinga
shaw + matic + pogba + fred / fellaini / herrera + martial + mata fundi + sanchez = sexy football
waliokaribu na jose mourinho wajaribu kumwagia angalau ndoo 50 za maji baridi ili aondokane na huu usingizi mzito wa kujilida ovyo
  1. They [the board] gave me a contract until July 2020. I have a contract to 2020, I didn't point a pistol at them. They give me the contract because they wanted to give it me."
  2. As a friend of mine was saying to me this morning, if tomorrow it rains in London it is my fault
  3. If there are some difficulties with the agreements of Brexit, it is my fault
  4. You can win, you can lose, but that dignity must always be there.
One Life, One Love, One Club.
Glory Glory Manchester United.
 
Kuna vitu watu wanachanganya;
i.Ukiwa mchambuzi bora sio lazima uwe au uliwahi kuwa kocha bora eg;Garry neville.
ii.Ukiwa mchambuzi bora sio lazima uwe au uliwahi kuwa mchezaji bora eg;Garry neville.
iii.Kati ya wataalamu bora wa uchambuzi wa soka namwona Garry neville ni bora zaidi.
 
Mkuu..kumfamanisha morinho na Sir.Alex Ferguson ni upuuzi..najua unampenda huyo jamaa ila huu ni upuuzi..morinho amekaa utd kwa miaka 3 ila fergie amekaa zaidi ya miaka 20..nashangaa sana unavyotumia hiyo post kama kigezo cha kumtetea huyu morinho
Naona umekurupuka mkuu hizo takwimu wanatoa sky sio mimi halafu sio kwamba nampenda mourinho naipenda manchester united nzima hadi mkata nyasi wa uwanja ili mradi yupo ndani ya timu atapata heshima yangu hata mourinho akifukuzwa ajae ntampa sapot kama hii

Pia si kwamba sir alex kafananishwa na mourinho hizo ni takwimu tu za ushind ktk mech sir alex tabak kuwa mtu special sana.
 
Wenzetu wanazibamiza kweli kweli hizi timu ndogo. Bingwa safari hii kazi ipo. Wote wanaupiga wa ukweli.
 
Sijakurupuka nimekucrush wewe uliaayetumia hizo takwim kumsupport morinho..Ukiwaweka hao watatu hapo maana yake umecompare uwezo wao..na ndo nikakwambia ni upuuzi kumlinganisha fergie na huyu jamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…