swali gumu sana na hili linatokana zaidi na pressure iliotawala klabuni kwa miaka 6
kwa makocha ambao wameshavuka miaka 50 ya kuzaliwa kwa maoni yangu carlo ancelotti a.k.a ,mzee wa
‘diamond midfield’ atatufaa sana kwa miaka 3 huku tukiwasubiria ryan giggs, michael carrick,zidane, thomas tuchel wakiendelea kupata uzoefu.
- carlo ancelotti hajawahi kuwa mtumwa wa kutegemea mfumo mmoja wa ufundishaji soka ndio maana ameendelea kuwa mwalimu mwenye kuhitajika na klabu tofauti.unakumbuka msimu wake wa kwanza pale chelsea wakati mashabiki wanajiuliza ni ipi khatma ya washambuliaji drogba na anelka, carlo aliwatumia wote wawili kutokana na mahitaji ya mechi wakati huku kwetu jose mourinho hajawahi kutumia washambuliaji wawili kwenye mechi moja.alipokwenda real madrid aliachana na fasafa ya mourinho ya 4-2-3-1 na kuamua kutumia mfumo wake pendwa 4-3-3 huu ni msimu wa nne makocha wa real madrid wanatembelea nyota yake.
- yupo vizuri sana kwenye ishu ya kuwatafutia wachezaji sehemu sahihi za kuufurahia mpira wao, pale madrid alimgeuza di maria angel kutoka namba 11 hadi kuwa namba 10, alipokuwa ac milan alitengeneza utatu mtakatifu uliotishia afya za makocha wa timu pinzani na kumfanya ricardo kaka kuwa mtakatifu. pale chelsea alitengeneza utatu mtakatifu wa essien, ballack na lampard ulikuwa hatari zaidi kuliko chanjo ya pepo punda, kule mbele anelka na drogba walikuwa wanafunga magoli kama wana kichaa cha mbwa
- mpira wa karne hii ya 21 unaendana na kasi ya teknnolojia ila cha ajabu baadhi ya makocha wameendelea kuishi wakiwa na fikra za karne ya 20, bahati njema carlo ancelotti yupo kama software kila baada ya muda anaji update mwenyewe bila ya shinikizo. ukiwatazama makocha wengine licha ya mafanikio yao waliopata utagundua ni watumwa wa mfumo mmoja wa ufundishaji kwa kuanzia na guardiola, diego simeone, jurgen klopp na jose mourinho hivyo basi wanapokutana na watu wanaowafahamu vizuri kimfumo wanaishia kuweweseka. Alipokuwa juventus alipendelea kutumia mfumo wa 3-4-1-2 na aliamua kuwapa nafasi ya kucheza pamoja Zinedine Zidane akiwa numa ya Alessandro Del Piero na Filippo Inzaghi.
- ikiwa carlo ancelotti aliweza kufanya kazi na watu wagumu kama vile Silvio Berlusconi, Roman Abramovich, Uli Hoeness , Karl-Heinz Rummenigge na Florentino Perez kwa mafanikio sidhani kama atashindwa kufanya kazi na familia ya glazer pamoja na ed woodward na kama atatafutwa football director mwenye ushawishi kama marotta wa juventus basi itapendeza sana.
- pia carlo ancelotti yupo vizuri sana kwenye kujenga mahusiano na wachezaji wake na hilo amelidhihirisha alipokuwa real madrid, chelsea, ac milan na hata PSG. Alipokwenda real madrid aliikuta timu ilioachwa na mourinho ikiwa imegawanyika pande mbili na alifanikiwa kubadili hali ya hewa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwa muda mfupi wa kazi, naamini kwa hali iliopo manchester united anaweza kuirekebisha kwa wiki moja tu.
View attachment 886094
udhaifu wake mkubwa ni ukimya wake kwa wachezaji na hata kwa mabosi wake.