ninapaswa nikushukuru kwa michango yako unayoendelea kuandika kwenye hii thread na nathubutu kusema ya kwamba wewe ni miongoni mwa wapenzi wanayoifanya hii thread kuwa update kila siku, na pia ni mara chache sana kukuona ukitumia lugha ya dhihaka dhidi ya wale unaotofautiana nao kimtazamo.
Mungu azidi kukubariki na wengineo kwa ujumla.
kiukweli hata mimi nilikuwa ni miongoni mwa waliovutiwa sana na uwepo wa jose mourinho ndani ya manchester united na sababu kubwa ni kwamba kwenye ulimwengu huu wa sasa hivi ni ngumu sana kumpata mwalimu mwenye wasifu uliotukuka kwenye kazi unaolingana na wasifu wa jose mourinho,ni josep guardiola pekee ndiye anaweza kusimama na mourinho kwenye mafanikio.
- bado nakumbuka alichokifanya jose mourinho miaka 14 iliopita akiwa na fc porto msimu wake wa mwisho.
- bado nakumbuka alichokifanya jose mourinho akiwa na chelsea misimu miwili ya mwanzo
- bado nakumbuka alichokifanya jose mourinho akiwa na inter milan misimu yake miwili ya kazi
- bado nakumbuka alichokifanya mourinho akiwa na real madrid miaka yake mitatu, ndiye mwanadaamu aliyeondoa upumbavu wa real madrid kufungwa ovyo na olympique lyon na juventus kwenye UEFA kupitia hatua ya mtoano
- pia bado nakumbuka alichokifanya mourinho akiwa na chelsea kwa mara ya pili
- na pia bado nakumbuka alichokifanya mourinho akiwa na manchester united msimu wake wa kwanza na hata wa pili.
lakini ukiangalia kwa upande wa pili wa shilingi utagundua ya kwamba nguvu ile ile aliyoitumia jose mourinho kwa ajili ya kujenga CV yake amekuwa akiitumia kinyume chake kwa dhumuni la kuiharibu CV yake.
mourinho ameshindwa kufahamu ya kwamba arsene wenger ndiye alikuwa mwanadamu wa mwisho kwenye ulimwengu huu kuwa na nguvu dhidi ya mwajiri wake baada ya ferguson. mpira wa sasa hivi umeingiliwa na mabepari na wajamaa ambao lengo lao kuu ni kuwa juu ya nembo ya timu.
- wenger ndiye mwanadamu wa mwisho aliyekuwa na uwezo wa kuwaaminisha wamiliki wa klabu ya kwamba usajili wa elneny ni bora zaidi ya usajili wa modric kwenda real madrid.
- wenger ndiye mwanadamu pekee aliyekuwa na jeuri ya kuwaaminisha viongozi na mashabiki wa arsenal ya kwamba kufungwa goli 8 na manchester ni faida kubwa kwa upande wao kwa sababu watapata kuingia sokoni kutafuta wachezaji kwa mafungu.
ukimuangalia jose mourinho naye anataka kuwa na nguvu kama hii kwenye klabu zote alizozifundisha jambo ambalo linamwia vigumu kuweza kulitekeleza.
- msimu wake wa tatu akiwa na chelsea alitofautiana na bepari abramovich na hatimaye akafukuzwa chelsea.
- msimu wake wa tatu akiwa na real madrid alitofautiana na florentino perez na watoto wake ramos na casillas na hatimaye akafukuzwa
- msimu wake wa tatu kwa mara nyengine tena alitofautiana na viongozi, wachezaji, madaktari wa timu akafukuzwa tena chelsea
- kwa mara nyengine tena msimu wake wa tatu ameanzisha vita na mwanadamu asiye na dhambi kwa familia ya bepari malcom glazer ambaye ni ed woodward na hatujui kitakachotokezea.
inaonekana dhahiri jose mourinho amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kukosa uvumilivu, busara na hekima kwenye kazi yake ya ufundishaji ndio maana hujikuta akiwa kwenye nyakati ngumu sana kwenye kazi zake.
Anashindwa kufahamu ya kwamba hata makocha wenzake nao pia wanakutana na changamoto kama za kwake yeye lakini ni nadra sana kuwakuta wakizungumza maneno ya ovyo dhidi ya klabu husika,wachezaji na hata viongozi.
mfano mdogo ni jurgen klopp alipendekeza usajili wa nabil fekir lakini mwisho wa siku viongozi wa klabu walifelisha dili la nabil fekir lakini jurgen klopp amenyamaza na kuendelea kufanya kazi lakini upande wa pili bado mourinho amekuwa akilalamika kutokusajiliwa kwa ivan perisic.
jaribu kuangalia kikosi cha liverpool wachezaji walionao utashangaa sana kuona wachezaji wao wengi ni wa kawaida sana lakini ni nadra kumsikia jurgen klopp akijitokeza hadharani kumponda dejan lovren kwa makosa anayofanya.
leo hii klopp amewafanya wachezaji kama robertson, alexander arnold, widjnaldum, milner, joel gomez, karius na wengineo kujisikia fahari kuwa wanafamilia wa anfield. na pia kuwafanya waonekane ni tishio dhidi ya wapinzani wake lakini kwetu sisi jose mourinho licha ya kuwa na kikosi chenye wachezaji wenye majina na uwezo wa hali ya juu ametufanya tuonekane ni kituko mbele ya wapinzani wetu na kupewa majina ya ovyo na wapinzani wetu
kwenye ishu ya CV ya mafanikio jurgen klopp hathubutu kukanyaga sehemu aliyopita jose mourinho lakini unakuta klopp anamzidi mourinho kwenye ishu ya kukaa na wachezaji kwa busara na uvumilivu.
na kwa ushahidi mwengine jaribu kuangalia muunganiko wa timu aliyoujenga pale dortmund jinsi alivyotengeneza muunganiko wa wachezaji wenye kuvutia kuwatazama kama vile gundogan, subotic,weidenfeller, lewandowski, sahin,hummels, bender, kagawa,grosskreutz na mpaka kesho jose mourinho hawezi kusahau kilichomkuta kwenye uwanja wa signal iduna park akiwa na real madrid.
hata kama jose mourinho atapewa tena miaka 5 ya kuifundisha manchester united hataweza kuishi na wachezaji wake kama ni watoto wake.
- Hiki kikosi tulichonacho tulipaswa sisi ndio tuwe tunazungumzwa zaidi kuwa ni tishio msimu huu na siyo liverpool
- hiki kikosi tulichonacho liverpool ndio walipaswa wakikutana na sisi ndio wakae nyuma kwa ajili ya kutafuta drawa
lakini cha ajabu jose mourinho ametufanya mashabiki wa machester united tugawanyike makundi mawili nayo ni team mourinho na team ed woodward.
mourinho aliyekuwa na uwezo wa kukaa na wachezaji pamoja na viongozi kwa hekima alifariki akiwa FC PORTO na kufufuka kidoogo akiwa na INTER MILAN.
dah hii mechi tim howard alinipotezea usingizi wangu na kunifanya nichelewe jukumu lakuosha vyoo vya skuli.
ilikuwa ni tarehe March 10, 2004 uwanja wa Old Trafford ndipo mwanamme huyu alipozidi kupigilia msumari wa moto CV yake ya ukweli.
hivi jamani mourinho hana kioo ofisini kwake akapata kujiangalia?