Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ed Woodward considering Manchester United legend Edwin van der Sar as new director of football
si mbaya kumpa nafasi mtu ambaye ameshafanya kazi ndani ya klabu lakini manchester united inamhitaji zaidi mtu mwenye ushawishi na uzoefu wa masuala ya uongozi.
dunia ya wakati huu mwenye fedha ndiye anayeonekana mwanamme
manchester city walimng'oa Txiki Begiristain kutoka barcelona na anachokifanya pale etihad kila mtu anakishuhudia.
kwangu mimi hawa ndio best football director
  1. monchi = AS ROMA
  2. Giuseppe Marotta = JUVENTUS
  3. Michael Zorc = dortmund
  4. Andrea Berta = atletico madrid
    kila la kheri edwin van der sar
 
Kinyang’anyiro cha Ligi Kuu England, kimeanza tangu wikiendi iliyopita, timu zinazotabiriwa kumaliza ndani ya nne bora, mabingwa watetezi Manchester City, Liverpool, Tottenham na Manchester United zikianza kwa kishindo.
Tottenham iliyoziengua Chelsea na Arsenal katika ‘top four’ ikitamba kwa msimu wa tatu mfululizo licha ya kujadiliwa sana kutokana na kutosajili mchezaji yeyote katika dirisha la usajili wa kiangazi, lakini imethitisha kuwa haikuwa na sababu za kusajili kwani inacho kikosi bora baada ya kushinda ugenini kwa mabao 2-1 dhidi ya Newcastle United.

Ujio wa Kocha, Maurizio Sarri, unaweza kuwa suluhisho kwa Chelsea, kwani aliiwezesha kushinda mabao 3-0 dhidi ya timu ngeni katika Ligi hiyo, Huddersfield Town, lakini wikiendi hii ndipo atapaswa kuthibitisha kama anao ubavu wa kuchuana kuing’oa Tottenham ndani ya nne bora.
Sarri atathibitisha hilo, atakapoiongoza Chelsea kuikaribisha Arsenal kwenye Uwanja wa Stamfodge Bridge, iwapo itaondoka na ushindi wa kishindo kama ilioupata kwa Huddersfield ataanza kuwashawishi wengi kuipa nafasi ya kufanya vema msimu huu.
Arsenal jana Jumapili iliyopita ilicheza mechi yake ya kwanza ya ushindani bila Arsene Wenger kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1996, licha ya kuwa nyumbani kocha Emery Unai hakuweza kuiepusha na adhabu kutoka kwa mabingwa watetezi City na kufungwa mabao 2-0.

Kocha wa kuwa huyo wikiendi ijayo pia atakuwa katika wakati mgumu kwani atasafiri kuifuata Chelsea moja ya timu ambazo zinaonekana zina vikosi bora vinavyoweza kupigania ubingwa.
Kwa upande wake Kocha City, Pep Guardiola alitamba kuwa kikosi chake kitazidi kutoa dozi kwa kila timu itakayocheza nayo akidai timu hiyo inamarika siku hadi siku.
Guardiola alisema kuwa anaamini katika mechi ijayo sio Bernardo Silva na Raheem Sterling pekee walioifungia mabao hayo, watakafunga tena wikiendi ijayo bali wafungaji wataongezeka watakapoikaribisha Huddersfield Jumapili hii.

Nayo Manchester United chini ya Jose Mourinho imeanza vema Ligi baada ya kuichapa timu bingwa ya Ligi hiyo msimu wa 2015/16, Leicester City kwa mabao 2-1 na wikiendi hii itaifuata timu isiyo na uzoefu ya Brighton.
Upande mwingine, Henrikh Mkhitaryan aliyehamia Arsenal akitokea United pamoja na washambuliaji mahiri Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette hawakuibeba Arsenal kama walivyofanya katika timu zao za zamani Aubameyang alikua tegemeo la mabao kwa Borussia Dortmund ya Ligi Kuu Ujerumani ‘Bundesliga’ na Lyon ya Ufaransa ‘Ligue 1’.
City ambayo iliilaza Chelsea mabao 2-0 katika mchezo wa Ngao ya Jamii inaonekana kuzidi kuimarika kila kukicha na sasa ni wazi kuwa inaweza kuandika historia ya kuwa timu ya kwanza kutetea taji la Ligi Kuu.

City iliyomnunua Riyad Mahrez pekee katika dirisha la usajili wa kiangazi kwa Pauni 60 milioni kutoka Leicester City, alionyesha ana kitu amekiongeza kwa City.
Mitambo ya Liverpool inaonekana imeongezeka nguvu na imeonyesha dalili kuwa itaangamiza zaidi msimu huu baada ya Sadio Mane kufunga mawili, Mohamed Salah na Daniel Sturridge nao wakitupia, huku James Milner na Robeto Firmino, wakicheza soka la kiwango cha juu, hata hivyo Liverpool wikendi hii itakuwa ugenini ikiifuata Crystal Palace.
 
kwa wale mliokuwa hamfahamu maisha ya nje ya uwanja ya mourinho leo mtaifahamu familia yake kwa picha😎
2C157A8200000578-3227035-image-m-67_1441751364760.jpg
2C15937100000578-3227035-Jose_Mourinho_and_daughter_Matilde_certainly_impressed_the_crowd-m-56...jpg
2C1A897000000578-3227035-image-a-12_1441788765786.jpg
 
mkuu hapo hauoni yupo mke, mtoto wa kiume, mtoto wa kike na mourinho mwenyewe au ulitaka maelezo gani tena
Huyo atakua sio mbongo.....

Mbongo halisi nipe picha tu, maelezo ntaweka mwenyewe mpaka historia ya kuzaliwa kwake na ya bibi na babu yake kwa picha hizo hizo.
 
Ndugu zanguni mpo?
Mbona mmepooza sana na CL yenu?
Najua mnatuogopa sana kwa sasa!
Kule Keita na kule Fabihno
Mbele wale wanyama watatu ni shida kwa kweli!
Nani haya bado hayaogopi Majogoo ya Anfield
Nani hayaogopi Majogoo?
 
Mkuu wewe hangaika sana lakini timu yako haina kiungo anayeweza kupata namba pale MUFC.
 
Mkuu wewe hangaika sana lakini timu yako haina kiungo anayeweza kupata namba pale MUFC.
Kichekesho hiki tutume kwa namba ipi mkuu?
Keita akija Man U anapewa kabisa kitambaa awe nahodha
Fabihno akija anakuwa nahodha msaidizi
Kiungo Liverpool sasa ni quality tupu!!
Combine ya Man U na Liverpool atakaye anza kutoka kwenu ni beki Bailly tu acheze na VVD
Kiungo pia wataanza Keita,Pogba na Fabiho
Kule mbele wote wanaanza Liverpool
Hata keeper Allson ataanza
Man U watakuwa na wachezaji wawili tu ktk combine hiyo
 
Mkuu,unatumia pombe kali?
Ama unatumia bangi kama mojawapo ya mboga zako za majani?

Mchezaji wenu mmoja tu Salah ndio anaweza angalau kupata namba pale MUFC.
 
Hahaha, Milner amuweke nje Fred?
Wijnaldum amuweke nje Matic,dunia si itasimama kwa lisaa limoja kuomboleza kifo cha mpira wa miguu?
Hapo sijamtaja Pereira wala Herrera.
Hamna kipa dunia hii ya sasa anaweza kumuweka bench De Gea,likitokea hili linaweza kupelekea ujio wa Yesu ghafla tukiwa hatujajiandaa mkuu.

Beki zenu ndio zile Rashford alizichambua kama njugu?
 
Mkuu,unatumia pombe kali?
Ama unatumia bangi kama mojawapo ya mboga zako za majani?

Mchezaji wenu mmoja tu Salah ndio anaweza angalau kupata namba pale MUFC.
1.Allson
TIA .Bailly .VVD. Robertson
Keita. Pogba .Fabihno
Mane. Firmo. Salah

Man U beki za pembeni hata hazijulikani ni nani hadi ni gugo kuwajua
Katikati akae nje Keita na Fabihno acheze Pereira na Fred?
Acha kushekesha watu wewe
Pembeni mbele nimuweke nje Mane acheze headless Sanchez?
Huna team kaka kubali tu
 
Hahaha, Milner amuweke nje Fred?
Wijnaldum amuweke nje Matic,dunia si itasimama kwa lisaa limoja kuomboleza kifo cha mpira wa miguu?
Hapo sijamtaja Pereira wala Herrera.
Hamna kipa dunia hii ya sasa anaweza kumuweka bench De Gea,likitokea hili linaweza kupelekea ujio wa Yesu ghafla tukiwa hatujajiandaa mkuu.

Beki zenu ndio zile Rashford alizichambua kama njugu?
Mkuu unajichosha tu maana Looserfool hawawezi kukuelewa
Jaribu tu kumukumbusha kaka Malafyale kuwa misimu miwili iliyopita wameambulia point tatu tu kutoka kwetu
 
Back
Top Bottom