Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ninachoshangaa hata kupaki basi pia hatuwezi....Muda wote kipa anatoa michomo sipati picha wangekua wanapata nafasi za kushoot watu na akili zao,tungepaki basi na bado tungefungwa 10-0


Hahahaja hatar
 
Basi hapa kocha hatuna Afukuzwe tu
 
chelsea vs atletico madrid kipindi kile mou akiwa chelsea alifanya upuuzi huu huu wa kutafuta droo ya bilabila ugenini kilichomtokea pale darajani hakuamini.
Alianza kushinda dk ya 45 phillipe luis akachomoa basi likawa halina maana tena ikabidi afunguke hapo ndipo alipopigwa km kasimama tena na mpira mwingi.

Matokeo ya jana ni ya kiduwanzi kweli
 
Let's call a spade a spade and not a big spoon, kwa kweli timu yetu inacheza mpira mbovu sana.

Yaani hata kupanga shambulizi ni tatizo, balls zinapotea hovyo, wachezaji hawajiamini (Mfano Smalling) sidhani kama wengi wetu hapa tunafurahia hii style of play..
 
mkuu,hii ndio timu yetu,hiki ndicho tulichonacho,kama ni mtoto ni mtoto flani hivi dunya kwelikweli,kwa vile ni mtoto wako na ni dunya utamtupa?au unadhani mzazi akiwa na mtoto dunya hajui kama mwanae ni dunya??soo jana toto dunya limetoka kitaa limekuja na kilo ya mchele inabidi nifurahi tu,usidhani mwanangu dunya anapoleta kilo ya mchele sioni watoto wa wengine smart wanavyowajengea wazazi wao majumba!!

kwa maelezo haya,elewa kuwa,usidhani hao mashabiki unaowalaumu hawaoni unachokiona wewe juu ya hii timu,walichokuzidi wamejaa busara na hekima za mzazi,this is our team...this is our pride.

Unahitaji nizungumze zaidi???
 
hivi tukivuka hapa inachezeshwa draw tena au tunajua tunaenda kukutana na mshindi kati ya nani na nani??
 
Pitieni comments zangu za nyuma humu ndani kuhusu team yetu. Nilionesha wazi wazi kuwa mourinho hana uwezo wa kuipeleka hii team tunapopataka ila nilishambuliwa sana na Radika na wenzake.



Niliegemea zaidi kwenye mbinu za mourinho dhidi ya soka la kisasa. Soka la kisasa halihitaji kucheza kwa kujihami. Soka la kisasa kujihami ni wewe kushambulia ili team pinzani wasije golini kwako na sio kupack bus unawaruhusu maadui kuja golini kwako kila muda, hiyo ndio Njia ya kisasa na aina ya uchezaji wa kisasa.


Team yetu sasa hivi imekuwa ikishinda watu haturidhiki kwa sababu ya kiwango kibovu. Ikifungwa pia haturidhiki.


Niliwahi kusema humu na ninaomba mpitie tena muone kwamba chini ya Mourinho wachezaji wengi wataonekana wa hovyo licha ya kuwa wachezaji wazuri hapo awali ... Nilisema micktaryan ( Bahati nzuri tayari tumepata ushahidi kumechotokea). Nilimtaja Pogba ( Tunaanza kuona ), anaefuatia ni Lukaku. Na wengine wengi.

Huwezi kuniambia wachezaji wote hawa kiwango chao kimeanguka kwa sababu za uwezo wao binafsi kushindwa kulisakata Kabumbu. No. Sababu ni Mourinho. Nikipata muda nitakuja kuezelea sababu za kiufundi kwa nini lundo la wachezaji wa team yetu viwango vyao vimeonekana kuwa domant kwa mbinu za kipuuzi za Mourinho. Leo tunamlaumu Lukaku ,niwaulize swali hivi Jana usiku striker Wetu Jana mfumo wa kiuchezaji wa team umemtengenezea Nafasi ngapi ???? Wote tuliona Nafasi walizotengeneza sevila na De gea kuokoa ,Je, Nafasi nyingi vile Kama zingekuwa kwa upande wa Manchester united tungeshindwa kweli kufunga . Siri ya mpira na kufunga magoli ni kutengeneza Nafasi nyingi. Nafasi chache unajipa Nafasi ndogo ya kufunga magoli. Kwa aina ya uchezani Wetu wa kujihami team haitengenezi Nafasi tutafungaje ????



Narudia tena Mourinho hafai hafai hafai .... Atatuharibia wachezaji viwango





Nawakumbusha tu, hivi ni lini mwisho team yetu ilifunga goli la kona
 
Tulishaongea saana hili suala
 
hivi tukivuka hapa inachezeshwa draw tena au tunajua tunaenda kukutana na mshindi kati ya nani na nani??

Ndiyo Draw inchezeshwa na Utakutana Na Mshindi wa Kati ya Michezo Hii Mitatu:

• Roma/Shakhtar Donetsk
• Bayern/Besiktas
• Barca/Chelsea

Hii Ni Probability tu, Do not take it seriously!
 
Ndiyo Draw inchezeshwa na Utakutana Na Mshindi wa Kati ya Michezo Hii Mitatu:

• Roma/Shakhtar Donetsk
• Bayern/Besiktas
• Barca/Chelsea

Hii Ni Probability tu, Do not take it seriously!

unajua watu wengi hawajui kitu kimoja,man utd huwa inapata shida sana kucheza na timu inayomiliki mpira,hii ni siku zote.Team pekee inayomiliki mpira halafu inafungwa na Man Utd ni Arsenal tu,hivyo mimi nikiona tu Man Utd inacheza na timu inayomiliki mpira huwa najua shughuli pevu siku hiyo!!Katika timu zilizobakia Man Utd itacheza balanced games na Roma,Chelsea na Liverpool tu!!!Zingine zote Barca,bayern,City,Madrid,Sevilla hata Shakhtar tutapata shida sana!!!Sijui kwanini hatunaga mbinu za kuvunja mbinu za timu pinzani kumiliki mpira,nadhani falsafa ya club ndio shida!!Van Gaal nilimuelewa alikuwa amekuja kubadilisha falsafa ya club kama alivyofanya Johan Cluyff kule Barcelona tatizo tulikuwa na haraka sana na kutaka matokeo makubwa haraka!!
 
Tuna wachezaji wazembe, wasiojituma, wasio badilika, wasiofahamu ukubwa wa Man U wanaokaa kujilemba Nywele kuliko majukumu yao ya uwanjani. Tumegeuza Degea kama Punda wetu hakuna mchezaji anaweza kuonesha jitihada binafsi ukiacha David.

Kila mtu angekuwa anatimiza majukumu yake kama DG anavyofanya najua Man U ingekuwa Timu tishio zaidi, Kocha kawa kama Masau Bwire Vijembe na maneno mengiii ila uwanjani hakuna lolote la maana ambalo linafanywa na timu.

Naishabikia Man U ila siwezi kuwa mshabiki hata katika mabaya ni lazima kila mmoja akubali Man U hatuna timu yenye kujituma kutafuta ushindi, Pogba, Rashfod, Mata, Martial wangekuwa wanajua thamani na ukubwa wa Man U wangeacha kabisa utoto na kujipanga ili kutengeneza majina OT.

Nakiri hata kama tutafuzu hatua inayofuata tutatolewa hakuna timu ya kushindana pale.

Siku JM anapewa mkataba mpya niliumia sana kuona anazidi kubaki pale OT.
 
Hapa pa van gal nimekuelewa japo nae alikuwa mtata alichokuwa ananikera wachezaj wanaanza kuumia mazoezin had mkifika siku ya mech academy yote imeitwa kusaidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…