Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Hii ndio formation tumecheza jana , 4-2-3-1 .... Timu kama Newcastle unawaweka matic na Pogba wapaki basi???? Kwanini tusicheze na matic peke yake Pogba awe Juu ????

Hivi unataka kuniambia lingard ana ubora wa kumnyima namba Pogba hapo Juu ???? Jana lingard kama namba nae na muda mwingine 10 akichange na Alexis amepiga pasi ngapi "Murua" za mwisho kwa namba Tisa????

Vyovyote iwavyo Paul Pogba si mkabaji na hatendew haki. Nina Uhakika kama Jana Pogba angecheza Jana kama namba nane au 10 tungekuwa aggressive kwenye mashambulizi refer mechi ya kwanza old Trafford, Alifunga goli 1 na assist 2 nadhani.

Safu ya ushambuliaji hata uwe na ronaldo au messi bila kuwa na namba nane au 10 mzuri hawatafanya lolote. Jana ndicho kilichotokea
Kwahiyo mkuu namba nane jana alicheza nani?
 
Swali nililokuuliza ndio jibu lako. Jana tumecheza na double number 6 ( matic na Pogba ) ... Lingard alikuwa false number 8.... Alexis Sanzez alikuwa namba 11 ila hakuwa natural namba 11... Muda Mwngi upande wa winga ya kushoto alikuwa anacheza Ashley young kama WING BACK ( beki wa kupanda na kushuka).

Una lingine ????.
Nnachojua ni kwamba matic ni namba sita, pogba ni namba nane... Sasa pogba na matic wanakua sehem moja yaani pogba yuko kushoto mwa matic!!

Pogba ni box to box midfeld na ndio maana mou anapendelea kumpanga kama namba nane maana anajua anaweza kupanda na kushuka, na hii ndio kazi anayofanya pogba pale man u....

Kama timu ikiwa inashambulia utamuona pogba kapanda na matic kabaki nyuma muda mwingi, na kama timu inashambuliwa utaona pobga na matic wote wamerudi nyuma kulinda!

Wengi wanapenda pogba acheze namba kumi ambayo inampunguzia jukumu la kulinda, ili muda mwingi atumie kushambulia na sio kushambulia na kurudi kulinda!!

Huwezi sema timu haina namba nane au timu ina namba sita wawili huo ni uongo mkuu!!
 
Kwahiyo mkuu namba nane jana alicheza nani?
Nimekuwekea picha Mzee ya kikosi na formation ya Jana, hebu soma maelezo yangu + hiyo picha ya kikosi cha Jana utajua nani alicheza namba 8.

Kwa kifupi Mourinho ni muharibifu. Niliwahi kuongea humu namna alivyomuharibu Micktaryan, Leo amekuwa Pogba na orodha itaendelea( tunza haya maneno). Na yote haya ni kwa sababu ya poor formation ya mwalimu( defensive formation au kupaki basi au kujihami). Kokote Duniani kuchezesha viungo Wawili wakabaji mbele ya mabeki wannne huko ni kucheza kwa kujihami.

Yaani mechi na Newcastle unamuweka matic na Pogba mbele ya Smalling,Jones, Ashley young na Valencia kama mabeki. Unatengeneza wachezaji sita nyuma ya msitari wa kati. Hii ni aibu. Kibaya zaidi zaidi zaidi zaidi kati ya wachezaji wanne waliobaki kucheza mbele,eti unampa kazi lingard ndio awe kiungo wa kuwaunga. Ni Mara kumi Juan Mata. Unaona alivyoingia mata hali ilikuwaje.
 
Attachments

  • 1518427629528.png
    1518427629528.png
    29.9 KB · Views: 38
Nnachojua ni kwamba matic ni namba sita, pogba ni namba nane... Sasa pogba na matic wanakua sehem moja yaani pogba yuko kushoto mwa matic!!

Pogba ni box to box midfeld na ndio maana mou anapendelea kumpanga kama namba nane maana anajua anaweza kupanda na kushuka, na hii ndio kazi anayofanya pogba pale man u....

Kama timu ikiwa inashambulia utamuona pogba kapanda na matic kabaki nyuma muda mwingi, na kama timu inashambuliwa utaona pobga na matic wote wamerudi nyuma kulinda!

Wengi wanapenda pogba acheze namba kumi ambayo inampunguzia jukumu la kulinda, ili muda mwingi atumie kushambulia na sio kushambulia na kurudi kulinda!!

Huwezi sema timu haina namba nane au timu ina namba sita wawili huo ni uongo mkuu!!
Sijui kama unaelewa mpira vizuri. Namba nane ukipewa majukumu ya kukaba au kusimama mbele ya mabeki wewe ni holding midfielder . Ndicho anachofanywa Pogba hivi sasa hebu soma hiki alichokisema Murphy baada ya Game ya Tottenham

Paul Pogba causing Manchester United defenders 'problems' | Daily Mail Online

Ndivyo alivyo kiasili Pogba hawezi majukumu ya "kuhold" yule ni "free roller ".
 
Nimekuwekea picha Mzee ya kikosi na formation ya Jana, hebu soma maelezo yangu + hiyo picha ya kikosi cha Jana utajua nani alicheza namba 8.

Kwa kifupi Mourinho ni muharibifu. Niliwahi kuongea humu namna alivyomuharibu Micktaryan, Leo amekuwa Pogba na orodha itaendelea( tunza haya maneno). Na yote haya ni kwa sababu ya poor formation ya mwalimu( defensive formation au kupaki basi au kujihami). Kokote Duniani kuchezesha viungo Wawili wakabaji mbele ya mabeki wannne huko ni kucheza kwa kujihami.

Yaani mechi na Newcastle unamuweka matic na Pogba mbele ya Smalling,Jones, Ashley young na Valencia kama mabeki. Unatengeneza wachezaji sita nyuma ya msitari wa kati. Hii ni aibu. Kibaya zaidi zaidi zaidi zaidi kati ya wachezaji wanne waliobaki kucheza mbele,eti unampa kazi lingard ndio awe kiungo wa kuwaunga. Ni Mara kumi Juan Mata. Unaona alivyoingia mata hali ilikuwaje.
So kuchezesha viungo 2 ndio kupaki bus? Na ukichezeshwa namba 6 hutakiwi kwenda kushambulia

Na game ya jana United wamepaki bus ?

Tatizo ni United ni namba 10 ambayo ilimshinda Mikhi anachezeshwa Lingard naye ni mzigo Pogba ni namba 8 sio namba 10 na kuna game nyingi Pogba amecheza the same formation na akacheza vizuri(angalia first 10 games)

Kocha angemuanzisha Mata namba ya Lingard but sio Pogba hata huko Juve hakucheza namba 10
 
Nashukuru leo mumekuja na uchambuzi mzuri,safi sana haya maongezi yanavutia.......baada ya kupoteana jana leo mupo hapa tunapata ABC enheee ....
 
ce1e5c4563f262e161e0c55b8138f628.jpg
yaliyopita si ndwele jamani mimi nimefurahi hiyo habari ya mourinho hapo juu
 
Suala sio kucheza pamoja issue ni wote kuchezeshwa kama "Holding Midfielders"

Nadhani utakuwa unanielewa

Samahanini Wakuu!
Nahisi Munglielewana Upesi Sana iwapo Kwanza Mutakuwa Tayari Kutofautisha Baina ya "HOLDING MIDFIELDER (Kiungo Mzuiaji) na DEFENSIVE MIDFIELDER (Kiungo Mkabaji).

Munaweza Mukatafuta wenyenye Lakini Manchester Haijawahi Kucheza na Holding Midfielder Wala Haitumii Mfumo huo na Mourinho Tokea Porto, Chelsea, Inter, Real mpaka Man U havutiwi na wala hana Plan Za Kuchezesha Holding Midfielder kwani si Mpenzi wa Wachezaji aina hiyo (Pirlo, Xavi n.k...
)

Nadhani Nilipotaja Hayo Majina tu hapo juu basi Mushapata Picha ya Majukumu na Uchezaji Wa Holding Midfielder (Kiungo Mzuiaji anaepoza Move za Maadui).

Kiungo Huyu (HM) ni lazema mbele yake Awe Na Very Talented Central & Wide attaking Midfieder Kama Pirlo alivyokuwa na Ricado Kaka AC Milan, Xavi alivyokuwa na iniesta.

So, unapokuwa na HM ni lazina uwe na Viungo 3 kati kati.

•Sergio Busquet-Xavi-Iniesta
• Gattuso-Pirlo-Kaka
• Yaya-Xavi-Iniesta

Kuhusu Defensive Midfielder Huyu ni Natural Namba 6.
Kwahiyo Huyu Namba 6 (DM) si Rahisi Kuwa Holding Midfielder (ingawa anaweza Kuwa) Kwani
yeye kazi Yake ni Kuwalinda Mabeki na si Kupoza Move za Maadui.

Una uhakika pogba anacheza kama holding midfielder?? Unaelewa maana ya holding midfielder??
 
Nnachojua ni kwamba matic ni namba sita, pogba ni namba nane... Sasa pogba na matic wanakua sehem moja yaani pogba yuko kushoto mwa matic!!

Pogba ni box to box midfeld na ndio maana mou anapendelea kumpanga kama namba nane maana anajua anaweza kupanda na kushuka, na hii ndio kazi anayofanya pogba pale man u....

Kama timu ikiwa inashambulia utamuona pogba kapanda na matic kabaki nyuma muda mwingi, na kama timu inashambuliwa utaona pobga na matic wote wamerudi nyuma kulinda!

Wengi wanapenda pogba acheze namba kumi ambayo inampunguzia jukumu la kulinda, ili muda mwingi atumie kushambulia na sio kushambulia na kurudi kulinda!!

Huwezi sema timu haina namba nane au timu ina namba sita wawili huo ni uongo mkuu!!

Mkuu Pogba si Box-to-Box (B2B).
Na ndiyo mana Mukawa munamlaumu hasaidii Kulinda.
Kidogo Matic Ndiyo anasifa ya Kuwa B2B midfielder.

B2B ni Yule Anaecheza Baina Ya Mabox Mawili! Yani anarudi Boxini Kwenu Anakaba ikisha Timu ikishambulia Anapanda Boxini Kwa Wapinzani Anashambulia Kama sometime anavyofanya Matic au alivyokuwa Yaya Toure Wakati Wa Ubora Wake.

Sasa Pogba Yeye Anatembea Kwenye Box la Wapinzani na Anarudi Kwa Set Pieces tu kama utampeleleza.

Kwahiyo Pogba ni Mtu Wa Offensive Zaidi Yani Central attacking Midfielder (Kiungo Mshambuliaji wa Kati) au Upper Playmaker (Kiungo Mchezeshaji).
 
Tatizo la Pogba sijui utoto au ajui majukumu yake maana kuna game akicheza kama Pogba ninayemjua anawaziba midomo watu wote, lakini kuna siku kama amelazimishwa ujui kama anazuia au anashambulia akinyang'anywa mpira anatembea sijui labda ndivyo alivyoelekezwa na kocha wake.
 
Tuache kumlaumu JM, je misimu minne iliyopita tushawahi kushika nafasi tuliyoishika sasa hivi? Je walio muongezea mkataba unadhani ni wajinga??

Alichukua timu ambayo kwenye uefa haipo ila sasa hivi tupo uefa na msimu ujao tutakuepo!!

Kwa mtazamo wangu hamna kocha anayeifaa man u zaidi ya mou kwa sasa!!
Mkuu Katika andiko langu nmebainisha wazi..

JM nampenda sana hasa Silka yake kama binadamu..
Mpambanaji, mpiganaji na asiekubali kushindwa..

Binafsi nacholaum kias kidogo ni Man Utd kutokua na kikosi cha kwanza kinachoeleweka ili walau anapoumia mchezaji au suspension pengo linazibika kiurahisi..

Pia nafasi stahiki za wachezaji mfano Kamnunua Mkhi acheze wap??
Kamleta PP acheze wap kwa mfumo upi??

Straika aliekua anatakiwa Utd alipaswa aje kucheza vipi??
Mwisho wa siku timu ikiharibu ni yeye atakua responsible,, na sio wachezaji..

Mkuu ni fedheha timu kama Manchester Utd kufungwa na kna hudder,, hata kwa babu ilikua inatokea and then baada ya hapo haijirudii ila kwa sasa ni kama mwendelezo..

Ishu ya UCL ipo wazi sheria za Uefa za bingwa wa Europa kushiriki ndio zmetubeba... Ligi tulimaliza wa ngapi mwaka jana??

Sipendi JM aondoke Man Utd bila ubingwa mkubwa wa heshima,, ila tunaomba mabadiliko.. Alete anaohisi watamfikisha anapotaka na aweze kuwatumia pia...

Mwanadamu yeyote anaposhindwa kuyamudu mazingira yake akiwa na vitendea kazi anakuwa Primitive...

Mpira wa sasa hauhitaji uvumilivu.. Man Utd wakisema watulie wajenge timu ni mengi mno yatapotea na brand itashuka sana rejea mkataba na Addidas pekee...
Carlo kafanya nn Munchen?? Baada ya mda gan kaondolewa??

Kuhusu mkataba binafsi naamini Ed n big mind.. JM alishaanza kutumia kundi lake kuwaaminisha kuwa anaondoka Utd kaamua ampunguze nguvu..
Ukizingatia timu haikuwa vibaya na hana sababu za kumwondoa,,
Alisikika akilaum kumkosa wide player kaletewa AS7.
Ed n master sina shaka kamtia kitanzi.. Kwa nn hajapewa miaka mingi kama Moyes??

Finale... Man Utd bado ina watu wa kawaida wengi labda tu tusiwe tunakuwa na matumaini makubwa..

Utd 4ever...
 
Pogba ni mzuri akipiga 10 hakika,ila chini yake wawepo watu wa maana ,kumbuka juve kulikuwa na watu mfano pirlo na vidal ila hapo dah mtamlaumu sana........wacha KDB aupige mwingi hivi unajua shughuli inayopigwa na kina FERNANDINHO pale chini?unaachaje kung'aa kwa mfano?
Sure Mkuu PP n mashine ile kipaji kinaootezwa kwa kulazimishwa kutumika kivingine...

Mwl wa Chemi,, Bio na Phy unamlazimisha atibu mtu...
 
Nashukuru leo mumekuja na uchambuzi mzuri,safi sana haya maongezi yanavutia.......baada ya kupoteana jana leo mupo hapa tunapata ABC enheee ....

Daa inabid tuwe tunakukaribisha tusikuvunje moyo usije kujifia mkuu ni bora unavyotema nyongo maana burnley ukizubaa tu wa 7

Hiki bado hakijapoa cha hapo kwako

FB_IMG_1518437966760.jpg

Sikufaham kabisa kama ww ni arsenal kumbe mti wetu mkuu ruksa tunakupa nafas ya kujimwaga hapa

Arsenal mwenzio kakupa moyo anakusifu kwa kuvamia hapa ila muwe mnakumbuka na sikukuubya 8/8
 
Back
Top Bottom