Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

48D906D200000578-5348055-image-a-182_1517677953670.jpg
 
Leo EPL haina Faraja Kwangu! 😀 😀 Hapa Mumeshinda! Na Kule Arsenal anammiminia Toni Kiama.
Bora Nikaangalie Movie hamna Namna.
 
Alexis Sanchez alifunga bao lake la kwanza akiichezea Manchester United baada ya timu hiyo kuishinda Huddersfield na hivyobasi kuisukuma katika eneo la kushushwa daraja.
Baada ya kipindi cha kwanza Romelu Lukaku aliipatia United uongozi kunako dakika 55 baada ya kupokea krosi nzuri.
Sanchez baadaye alichezewa rafu na beki wa Huddersfield Michael Hefele na hivyobasi kutunukiwa mkwaju wa penalti aliopiga ukapunguliwa na kipa kabla ya kuupata na kufunga.
 
Leo nilimkubali sana Mou kwa treatment aliyompa Pogba,ili awe mkamilifu anatakiwa atubu sasa kwa maneno yake ya kishamba aliyomrushia the legend Paul Scholes manake kwa sasa naona alichokisema Scholes kimeonekana wazi na yeye sasa anakula matapishi yake.
 
Leo nilimkubali sana Mou kwa treatment aliyompa Pogba,ili awe mkamilifu anatakiwa atubu sasa kwa maneno yake ya kishamba aliyomrushia the legend Paul Scholes manake kwa sasa naona alichokisema Scholes kimeonekana wazi na yeye sasa anakula matapishi yake.
Pogba alisema nini mkuu!?!
 
Pogba alisema nini mkuu!?!
No,Pogba hakusema kitu bali ni Paul Scholes kuna kipindi timu ilikuwa haifanyi vizuri sana sasa yeye wakati anachambua baadhi ya mechi hizo akasema "inasikitisha sana kuona timu kama Man U ina wachezaji wasiojituma na kuwa tayari kuifia timu. Ukiangalia matokeo yanazidi kuwa mabaya kila siku ni aibu sana" Alipoulizwa yeye anahisi tatizo hasa ni nini? Akasema "Mimi nionavyo tatizo linaanzia kwa Paul Pogba, ukiangalia Man U inajengwa kumzunguka Pogba kwa hiyo anapocheza vibaya na timu haichezi vizuri. Pogba amekuja hapa kwa gharama kubwa na tuna matumaini makubwa na yeye lakini ukimuangalia hajitumi ipasavyo, yuko wapi Pogba Wa Juventus? Yuko wapi Pogba aliyekuwa anaonekana kila sehemu ya uwanja pale Juventus? Yuko wapi Pogba aliyekuwa anavunja ngome za wapinzani pale Juventus? Yuko wapi Pogba aliyekuwa anafunga magoli kutoka mita ishirni na tano pale Juventus? Ukijiuliza unaona ni mchezaji tu amefeli na wakati mwingine unaweza kuona pengine kocha naye anafeli, kwa sababu Ni aibu kubwa sana kwa timu kuwa na mchezaji kama Paul halafu akashindwa kutumika kwa kiwango kinachotakiwa". Mou alipoulizwa kuhusu maoni ya Scholes akajibu kwamba Scholes anatakiwa apuuzwe kwa sababu anamuonea wivu Pogba kwa hela anazoingiza pale Man U ndio maana ana msema Mara kwa Mara. Sahz naona somo limemuingia na anamchukulia hatua kimya kimya.
 
Back
Top Bottom