Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Yupo tu humu humu anajijua....Hakarabati uwanja yy anakarabati majukwaa tu......Hadi spurs kamzidi...
4839AC5E00000578-0-image-a-2_1516189929488-600x400.jpg

4839AC7A00000578-0-image-a-3_1516189936998-600x400.jpg

4839AF7600000578-0-image-a-4_1516189949416-600x400.jpg

4839B05900000578-0-image-a-7_1516189967197-600x400.jpg

4839B1D200000578-0-image-a-6_1516189958799-600x400.jpg

Anatakiwa aombe radhi aisee
 
Hii picha ya Mkhtaryan Leo mchana alipokuwa anaondoka kwenye viwanja vya mazoezi "Carrington" imeniumiza moyo sana. Ukimuangalia kwa makini jamaa machozi yanamlenga na inawezekana alilia kabisa. Hata mazoezi hakufanya nahisi kwa sababu kocha ashamtoa jamaa kwenye mipango yake. Na inasemekana jamaa anaumia sana kitendo cha Man U kum push aondoke ili aje mchezaji mwingine kiasi kwamba kumuona yeye ni nuksi Wa ucheleweshaji wa ujio Wa Alexis. Maisha yana changamoto asee!
 
Attachments

  • 330919.jpg
    330919.jpg
    13.3 KB · Views: 39
Hii picha ya Mkhtaryan Leo mchana alipokuwa anaondoka kwenye viwanja vya mazoezi "Carrington" imeniumiza moyo sana. Ukimuangalia kwa makini jamaa machozi yanamlenga na inawezekana alilia kabisa. Hata mazoezi hakufanya nahisi kwa sababu kocha ashamtoa jamaa kwenye mipango yake. Na inasemekana jamaa anaumia sana kitendo cha Man U kum push aondoke ili aje mchezaji mwingine kiasi kwamba kumuona yeye ni nuksi Wa ucheleweshaji wa ujio Wa Alexis. Maisha yana changamoto asee!
Dah hata mie imeniumaaa inabidi aende tu Kambi popote iwe mvua iwe jua maisha lazima yaende
 
Paul Pogba ana mchezo wenye ubunifu zaidi ya kiungo wa kati wa Manchester City Kevin De Bruyne, kulingana na takwimu.
Mchezaji huyo wa Manchester City amekuwa akionyesha mchezo mzuri katika kikosi cha Pep Guardiola msimu huu.
Lakini ni kiungo wa kati wa Manchester United aliyevunja rekodi ya usajili ambaye amefaa zaidi uwanjani.
Pogba ametoa pasi tisa za magoli katika mechi 13 za Man United.

De Bruyne amefanikiwa kutoa pasi kama hizo lakini katika mechi 23.
Usaidizi wa pasi zinazotolewa na Pogba ili kupata magoli ni mzuri zaidi ya mchezaji yeyote yule katika ligi tano za bara Ulaya msimu huu.
Paul Pogba (Man Utd) - Pasi 9 katika mechi 13
Neymar (PSG) - Pasi 9 katika mechi 14
Philipp Max (Augsburg) - Pasi 9 katika mechi 18
Pione Sisto (Celta Vigo) - Pasi 9 katika mechi 19
Leroy Sane (Man City) - Pasi 9 katika mechi 21
Kevin De Bruyne (Man City) - Pasi 9 katika mechi 23

Kevin De Bryune ametoa usaidizi kama huo wa Pogba lakini katika mechi 10 zaidi.
Neymar anamfuata Drogba katika jedwali la kutoa pasi zilizozaa magoli.
Hatahivyo, licha ya Pogba kuwasaidia wachezaji wenzake , ni safu ya mashambulizi ya Manchester United ambayo imekifanya kikosi cha Jose Mourinho kuwa nyuma ya Manchester City kwa pointi 12.

Antonio Valencia, Anthony Martial na Romelu Lukaku wote walifunga wakati United ilipoicharaza stoke City mabao 3-0.
Pogba alihusika katika kutoa pasi ya bao lililofungwa na Valencia kunako dakika ya tisa na bao la Martial dakika ya 29 baadaye.
Kwa jumla msimu huu City imefunga mabao 67 huku majirani zao wakifunga magoli 48.
 
Mshambuliaji wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan, 28, yuko huru kuhama kwenda London kujiunga na Arsenal. (Mirror)

Kiungo wa kati raia wa Armenia, Henrikh Mkhitaryan, 28, anasema anataka nyongeza ya mshahara kuweza kuhama Manchester United kwenda Arsenal. (Mirror)
 
Hii picha ya Mkhtaryan Leo mchana alipokuwa anaondoka kwenye viwanja vya mazoezi "Carrington" imeniumiza moyo sana. Ukimuangalia kwa makini jamaa machozi yanamlenga na inawezekana alilia kabisa. Hata mazoezi hakufanya nahisi kwa sababu kocha ashamtoa jamaa kwenye mipango yake. Na inasemekana jamaa anaumia sana kitendo cha Man U kum push aondoke ili aje mchezaji mwingine kiasi kwamba kumuona yeye ni nuksi Wa ucheleweshaji wa ujio Wa Alexis. Maisha yana changamoto asee!
Acha niisave hii picha ipo siku nitaishusha hapa akianza vitu vyake popote atakapoenda. Picha inaumiza sana hii
 
Tukiiangalia Match ya Liverpool na Man City kuna vitu vingi vya kujifunza juu ya Match Ile iliyojaaa ufundi na msisimko wa aina yake.

Liverpool wametuonyesha udhaifu wa Man City, Man City hawana mabeki wazuri wala kipa, same as Liverpool lakini wana Striking force nzuri inayowafichia madhambi yao.

Tactically, zilikutana timu zenye Falsafa moja ya kushambulia muda wote wa Mpira, lakini Zenye madhaifu sawa upande wa Mabeki na Kipa.

Kushinda mchezo kulihitaji mbinu za Makocha binafsi, Kloop baada ya Match ametuambia alitumia mifumo zaidi ya Minne kuweza kupata ushindi Ule haikuwa kazi rahisi kuwasimamisha na kuwafunga City ya Pep Gurdiola.

Kosa kubwa alilofanya Klop ni kupunguza pressing force langoni mwa City kwa kuwatoa Salah na Mane' ili kulinda ushindi jambo lililoipa City nafasi ya kusawazisha magoli.

Ni makosa kujilinda mbele ya Viungo na Washambuliaji wa City, Gurdiola ni fundi katika Creativity eneo la 18 la timu pinzani, anawafanya akina De Bruyne, Sane na Silver kuwa ma ghost pale mbele, watakufunga ndani au nje ya 18 licha kuweka wachezaji zaidi ya Sita kuzuia.

Klop aligundua udhaifu wa City kuanzia safu ya Kiungo, ndio mana alitumia zaidi Mawinga/viungo wa pembeni wenye mbio.

Na goli la mapema la Chamberlain liliwashangaza City.

Tumemuona Gurdiola licha ya kutanguliwa goli zaidi ya tatu hakuwa na Pressure alibadilisha mchezo na kuifanya City kucheza mpira wake dakika 15- 20 za mwisho za mchezo na kufanikiwa kurudisha magoli mawili.

Strike force ya Liverpool haikuwa makini, wangeweza kushinda magoli zaidi ya Site kama wangekuwa na utulivu, Mane' hakuwa na bahati.

Pengo la Countihno lilionekana katika kiungo cha Liverpool na kazi kubwa ikahamia kwa Salah.

City nao kumkosa Silver kulifanya mfumo kutokuchezeka, wa pasi nyingi nyingi na fupi fupi kati ya Silver, De Bruyne na Sane hali iliyopelekea kutokuona makali ya Aguero.

Ukiangalia kikosi cha Liverpool, City na hata Chelsea hakuna timu yenye kikosi chenye mchanganyiko Mzuri kama Man Utd kwa sasa pale Old T.

Mourihno anatakiwa kubadilika na kuachana na mbinu zake kujilinda, anatakiwa kuifanya timu na wachezaji kuwa huru.

Man Utd ingekuwa chini ya Gurdiola tungekuwa tunaongea mengine muda huu.

Mfumo wa kujilinda na kukaba unafanya vipaji vingi kupotea au kufanya pale Old T.

Timu inakosa kasi na ari ya kushambulia, Mikhtaryan ndio huyo ameshapotea licha ya uwezo na kipaji alichonacho, A. Martial hayupo huru uwanjani na anabidi kutumia muda mwingi kulinda kuliko kushambulia.

Licha ya Shughuli ya Matic kuijua lakini hatuoni ile kasi yake uwanjani, Matic mwisho wake ni katikati katikati haruhusiwi kwenda kushambulia.

Wakati msimu uliopita ndio alikuwa moja ya Wachezaji waliokimbia Km nyingi, Mou anaua kipaji cha Any Hererra kwa kumtaka akabe kuliko kushambulia, Kabla Herera alikuwa kama Countihno wa sasa.

Kwa falsafa ya kukaba zaidi kunaifanya timu kukosa Ubunifu pale mbele, ni kweli tunashinda lakini katika mazingira magumu, hard football na sio Sexy football kama ya City au Barcelona.

Asili ya Man United ni kucheza soka la nguvu, kushambulia na la kasi kwa kutumia Mawinger zaidi.

Tete si za kusajiliwa Sanchez au Ozil nataka kujua Mourihno amekubali kubadilika, hawa akina Sanchez ni wachezaji wanaocheza soka wakiamini katika vipaji vyao na kasi ya timu.

Mourihno akibadilisha style na falsafa yake na kucheza soka la kushambulia na kasi muda wote, timu itafunga magoli mengi zaidi ya wanachokifanya City.

Timu ina upungufu wa Creative players kutokana na mfumo, kwa sasa ni Pogba tu, lakini kuna akina Mikh, Martial na Matta.

Asernal World Class Player alikuwa Sanchez na Ozil pekee timu ilikosa top players wengi.

Man United kuna mchanganyiko Mzuri.

Tusubiri Ujio wa Sanchez.
Mchanganyiko mzuri wa lukaku na yule beki wenu lindorf acha mahaba mkuu stock city ana squad kubwa kuliko man
 
Kweli kabisa nakubaliana na wewe Mourinho anaua vipaji, mfano mzuri ni Lingard. Uyu ajawai kufunga magoli 10 ndani ya msimu mmoja lakini msimu huu kafunga magoli 11.
Mourinho akiendelea hivi, Lingard atafikisha goli 20+ na kipaji chake kitakua kimekufa kabisa.
Bila ya kumsahau Martial ambae mpaka sasa kafunga magoli 10, 8 kwenye Epl.
Kabla nilikuwa sijakuelewa lakini now nimekuelewa kwa lugha uliyotumia, ni sahihi now Lingard anafanya vizuri mno, magoli 10 katika msimu mmoja ni kitu kizuri lakini ni mapema mno kumtumia yeye kama mfano wa kukuza vipaji kwa Mou, tujiulize Ni sahihi kwa Kipaji na Kiwango cha Martial na Performance yake uwanjani kwa msimu? Rejea msimu uliopita? Naamini akipewa nafasi zaidi na akiwa huru uwanjani anaweza kufanya mambo makubwa zaidi ya haya tunayoyaona sasa, Kwa kipaji na Kiwango cha Martial ni kizazi cha Mbappe kama sio Neymar!! Ila naamini mfumo, falsafa na Itikadi za Mou zinarudisha nyuma Kiwango chake, Ye mwenyewe ameripotiwa mara nyingi akilalamika kuhusu nafasi na majukumu anayopewa uwanjani na hata kiwango chake sio Consistence ni kinapanda na kushuka tofauti na makinda wenzake.

Tunaona consistence ya kiwango cha De Bruyne wa Man City kikikuwa match to match.

Tumeona Floppy ya Mikh,

Simuoni Mourihno kama mlezi mzuri wa wachezaji wenye vipaji hasa makinda, jaribu kulifatilia hili.

Angalizo:- ni shabiki wa damu wa Man United guys tuwe huru zaidi na tujenge hoja bila kudhihakiana, kutukanana na kuvunjiana heshima, naamini humu sote ni waungwana na mashabiki wa Damu wa Man United.
 
Kocha gani ambae anachukua makombe halafu kikosi chake sio cha gharama kubwa?
Nisaidie nadhani anamaanisha kuwa Mourihno ni aina ya Makocha wanaopenda kuwa na wachezaji waliotayari kwa mapambano, wachezaji waliokamilika au waliokuwa ili iwe rahisi ye kuwapa majukumu na sio hawa wanaokuwa/vijana/makinda
 
Moja ya post ya hovyo kabisa kuwahi kuisoma humu jf.

Unasifia striking force ya liverpool hivi unajua wamefunga magoli mangapi zaidi yetu?

Inakuaje timu inayopaki basi na kuua vipaji ikafunga magoli mengi zaidi ya arsenal, Chelsea, spurs na wapuuzi wengine.

Unazungumzia sexy football, hivi tangu aondoke Ferguson ni lini tulishawahi cheza mpira wa kushambulia? Au umezimisi side pass na back pass za van gaal?

Hakuna kitu kizuri kwenye mpira kama makombe mzee, mbinu za mreno ni kukupa makombe, mashabiki wa ass no wanabweka kila siku Mr bean aondoke wakati ni moja ya timu zinazocheza mpira wa kuvutia sana England.
Sawa pamoja na kuwa ya hovyo lakini inawezekana hukuielewa post yangu vizuri, nimeiongelea game ya Liverpool vs Man City, nimeisifia Stike ya Liverpool kwenye game na Man City tu kama mfano au hadidu na rejea yangu.

Lakini siamini kama hawa wote uliowataja ni washinda ni au kipimo chetu kwa sasa.

Wapinzani wetu ni Man City katika EPL wametuzidi kila kitu, Point na hata Goal difference, ni kweli Strike yetu haijafunga magoli mengi kama ilivyo kwa City.

Lakini hata hao tuliowazidi ni kwa magoli machache, tofauti kati yetu na City ambapo kuna pengo kubwa, City ana uwiano mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa dhidi yetu.

Kwa kuingalia Man City basi bado kuna kazi kubwa ya Kufanya, City wana magoli Mengi ilihali sisi tuna magoli machache.

Simuongelei David Moyes mana hakuwa na sifa za kuifundisha Man Unite au kuwa mrithi wa Sir, na nilishangaa alivyopewa timu sikutegemea makubwa kutoka kwake, na pale ndio mwanzo wa kuharibika historia yetu.

Nakubaliana na wewe kuwa tunahitaji heshima na Makombe lakini hoja yangu ni kucheza soka la nguvu na la kushambulia zaidi kama ilivyokuwa Man United ya Sir Alex.

Fergurson hakuwa na timu ya kutisha lakini wachezaji walikuwa na njaa na kiu ya kutafuta ushindi muda wote walikuwa wanapambana.

Luis Van Gaal nadhani tuliwahi kumtimua Falsafa zake zilihitaji misimu zaidi ya minne kuleta matunda, alikuwa analeta aina mpya ya soka pale old T.
 
na pia wana ma super star wa kutosha
martial=messi
lukaku = suarez
mata= coutinho
hapo bado kuna kina dembele sub nakubaliana na wewe@Chief Mkwawa lakini kwa kikosi tulicho nacho msimu huu tupo Class moja na Barca, Madrid, Bayern na PSG, vikosi vyetu havina tofauti kubwa sana.

kocha ndio anajua acheze mfumo gani, yeye ndio kazi yake hio na sio sisi. hao mabeki wazoefu wazuri ni wapi? hebu nitajie, sawa kwa mfano tuna Valencia, Jones, Baily, Marcus Rojo.

umedanganya na huangalii mpira kwa hii comment unaonekana unahadithiwa tu. kwanini nakwambia hivi?
-crystal palace tulimfunga 4-0 na stats ni hizi

Nafahamu na nina hizo Statistics ila nimeitumia Crystal Palace kama timu ndogo ya mfano, timu ngapi ndogo zimevunja mwiko na Record yetu kwao kwa msimu huu au uliopita Mkuu? Najifunza kukubaliana katika tusivyokubaliana.
QeeyJAQ.png

-burnley tulitoka droo 2-2 na stats ni hizi
kIay4OM.png

sasa kama sisi tumemiliki mpira asilimia 71 halafu unasema tumepaki basi sijui nikuambie nini.

kifupi sijamuona mou akipaki basi na timu ndogo, inatokea sometime timu imeshinda ana defend dakika za mwisho, ila sijawahi ona eti tunacheza na timu ndogo mwanzo mwisho kakaa nyuma, sawa lakini naongelea Falsafa nzima ya Mou, tunaiona hiyo ya kupaki basi katika match na timu kubwa coz wao wanatuzidi lakini hizi ndogo tunawazidi lakini game na timu za kawaida bado Mou amekuwa akitumia hii Falsafa, na kuona hili tuwe tunaangalia sana mifumo anayotumia, tunafahamu mifumo ya ushambuliaji ni ipi.

na kwa taarifa yako kama hujawahi iona man u ya fergie ilikuwa hivyo hivyo kuna muda timu inaongoza 1-0 anamtoa striker au kiungo mshambuliaji anaingiza beki tunadefend hadi mechi inaisha. kuna mwaka vidic alikuwa mchezaji bora epl. kaangalie tulikuwa tunachezaje, Vidic kuwa mchezaji bora sio kwamba tunadefend hata Alonso au Marcelo wa Madrid wanakuwa kati ya Mabeki bora sio kwa kuwa Madrid wanadefend, nadhani ni mchango wao na jinsi wanavyotimiza majukumu yao kwa u sahihi.

Sio Vidic tu hata Rio Ferdinand alikuwa mmoja wa wachezaji bora wa EPL.

So siamini kama kupaki bus ni moja ya vigezo vya kuwa mchezaji mzuri au bora.

hao makocha waliokuja baada ya fergie na wakawa wanashambulia walishinda nyingi eeh, nadhani tumuongelee Van Gaal, Moyes tulimuonea kumpa timu.

hebu nitajie mwaka ambao martial au rashford wamecheza vizuri kuliko msimu huu, sikuelewi ujue rashford huyu huyu ambae ana goli 9 na assist 5? martial huyu huyu ambae ana goli 10 na assist 6? hawa jamaa wapo kwenye form ya maisha na wanacheza vizuri kushinda miaka yote waliyowahi cheza. ili labda uelewe Eden Hazard ana goli 6 na assist 4 msimu huu. amepitwa na wote hao wawili.

Kuna kucheza vizuri kwa msimu na kuwa performance kwa kuangalia Vipaji na Viwango, inaweza kuwa msimu huu wamefanya vizuri lakini mafanikio waliyoyapata au wanayoyaoata yanaendana na Viwango na Vipaji vyao? Kama jibu ni ndio basi nitakuwa liana na wewe.

Lakini Martial msimu uliopita alilalamikia kutokufurahia nafasi na majukumu anayopewa na kocha, akasema yanamfanya asiwe huru hivyo kushindwa kuonyesha uwezo wake ndio mana nasema inawezekana tukifunguka zaidi huyu Martial anaweza kuwa katika sayari nyingine na ya peke yake.

Hawa madogo licha ya hayo mafanikio lakini hawana consistency ya uhakika, leo Rashford ameshaflopp, tunamuona Lingard akifanya vizuri lakini sio mafanikio ya muda mrefu.

Case ya Hazard ni nyingine, ana changamoto lakini dunia inamfahamu akiwa katika Climax yake zaidi ya misimu mitatu hadi kutajwa kama mrithi wa CR7 n.k, hana furaha tena na Stamford Bridge, tamaa na ndoto zake sasa zipo Madrid anaiona nafasi yake.

Huwezi kuwafananisha hawa akina Martial, Rashford na Hazard, ukiwaweka leo Sokoni nadhani Hazard ana thamani kubwa zaidi yao.

si kweli, carrick alikuwa mara anaitwa mara haitwi, jones na smalling pia hivyo hivyo, butner, bebe, de gea wote walikuwa hawaitwi.

Nikukumbushe Sir Alex Fergurson ameifundisha Man United kwa miaka zaidi ya 24 zaidi ya misimu 22, hao akina Smalling, Jones, De Gea walikuta zama za babu zipo ukingoni lakini sasa ndio tegemeo katika timu zao.

Sio wote walikuwa wanaitwa lakini wengi wao walikuwa na uhakika na namba kwenye timu zao za taifa, sina haja ya kukutajia.

kama nani kipaji chake kinauliwa?Mikhtaryan, Martial, Rashford

Kwa nini tusicheze na washambuliaji wawili kama ulivyo utamaduni wetu, timu ikawa na washambuliaji wanne, ndani wawili sub wawili, Lukaku ana Mzigo mkubwa sana kwa kubaki peke yake, ngumu kufikia Malengo.

Nilitegema Tisa na Kumi wangecheza Lukaku na Rashford.

Rashford ni mzuri akicheza nyuma ya Mshambuliaji kuliko Winger.

lini sir Alex amemponda mou? link please. na hao wachezaji wa zamani uliowataja ni ma pundit, kazi yao ni kuponda wanalipwa wafanye hivyo, kama unachukua opinion za pundits na kuzifanya ni fact nakuonelea huruma. maana utahangaika kila siku.

Gary Nevel ni mmoja wa wachambuzi wakubwa na wanaolipwa pesa nyingi kwa sasa kutokana na Uchambuzi wake sahihi, na huwa ni mkweli.

Akina Scholes kutoa kasoro ni haki yao, wamecheza pale kwa muda mrefu, wanajuwa Falsafa ya Old Trafford wanafahamu Ligi kuu ya England na ndio mana wanasema huu sio utamaduni wa Man United.

Hutuwezi kujihami hata kwa timu ndogo, tulianza vizuri kabisa hata game za majaribio zilitupa Mwanga.

si ndio maana tumekaa mechi zaidi ya 40 bila kufungwa OT,
[/QUOTE]

Nashukuru kwa Homework@Chief Mkwawa, tuendelee kujenga hoja na kufahamishana.

Tunapokosea tuelekezane, ila tunaokosa pia tunaenda kuona mabadiliko kupata mafanikio makubwa zaidi ya haya, lazima turudi kwenye Ufalme wetu.
 
Hii picha ya Mkhtaryan Leo mchana alipokuwa anaondoka kwenye viwanja vya mazoezi "Carrington" imeniumiza moyo sana. Ukimuangalia kwa makini jamaa machozi yanamlenga na inawezekana alilia kabisa. Hata mazoezi hakufanya nahisi kwa sababu kocha ashamtoa jamaa kwenye mipango yake. Na inasemekana jamaa anaumia sana kitendo cha Man U kum push aondoke ili aje mchezaji mwingine kiasi kwamba kumuona yeye ni nuksi Wa ucheleweshaji wa ujio Wa Alexis. Maisha yana changamoto asee!
Ukikumbuka alikuwa Top classic player duniani hivi karibuni, aliamini furaha yake ingekamilika pale Old Trafford kwa kucheza kwa heshima na kwa muda mrefu, lakini ndio hivyo ameshushwa thamani kwa kubadilishwa na mchezaji, hapewi nafasi ya kuchagua timu, kuondoka kwa Heshima, ila Kwangu Mikh atabaki kuwa mmoja ya wachezaji wazuri mno tuliowahi kuwa nao lakini tulioshindwa kutumia uwezo wao.

Jamaa ni fundi haswa, tumtakie maisha mema na yenye mafanikio huko aendako.
 
Mchanganyiko mzuri wa lukaku na yule beki wenu lindorf acha mahaba mkuu stock city ana squad kubwa kuliko man
Aaaah aaaah aaaah Stock City wana Norma player while Man United tuna World Classic Player (Pogba), Top Players ( Matic,Valencia Lukaku, Martial, Herera) na Normal players wa kutosha.

Kuna tofuti kubwa sana kati ya Stock na Man Unite.

Welcome Alex Sanchez. No 7.
 
Hii picha ya Mkhtaryan Leo mchana alipokuwa anaondoka kwenye viwanja vya mazoezi "Carrington" imeniumiza moyo sana. Ukimuangalia kwa makini jamaa machozi yanamlenga na inawezekana alilia kabisa. Hata mazoezi hakufanya nahisi kwa sababu kocha ashamtoa jamaa kwenye mipango yake. Na inasemekana jamaa anaumia sana kitendo cha Man U kum push aondoke ili aje mchezaji mwingine kiasi kwamba kumuona yeye ni nuksi Wa ucheleweshaji wa ujio Wa Alexis. Maisha yana changamoto asee!
Duuuuh hii picha jamaa kama analia hivi. Utashangaaa mikosi ndy kwanza imeanza man utd tena upya. Kulazimishwa kuondoka 7bu ya mtu mwingn kuja ni kushushwa heshima. Mbn mi naona jamaa haja drop sana kivile ila muda zaid wa kucheza ungemtengeza upya!! Basi amuuze na lukaku ambaye ni mzito hadi kugeuka tu anachukua mwezi. Unaccepted to mikhi but pains to him na mimi. Sanchez anaeza asifanye lolote pale Man utd. Lets wait and see.
 
Kabla nilikuwa sijakuelewa lakini now nimekuelewa kwa lugha uliyotumia, ni sahihi now Lingard anafanya vizuri mno, magoli 10 katika msimu mmoja ni kitu kizuri lakini ni mapema mno kumtumia yeye kama mfano wa kukuza vipaji kwa Mou, tujiulize Ni sahihi kwa Kipaji na Kiwango cha Martial na Performance yake uwanjani kwa msimu? Rejea msimu uliopita? Naamini akipewa nafasi zaidi na akiwa huru uwanjani anaweza kufanya mambo makubwa zaidi ya haya tunayoyaona sasa, Kwa kipaji na Kiwango cha Martial ni kizazi cha Mbappe kama sio Neymar!! Ila naamini mfumo, falsafa na Itikadi za Mou zinarudisha nyuma Kiwango chake, Ye mwenyewe ameripotiwa mara nyingi akilalamika kuhusu nafasi na majukumu anayopewa uwanjani na hata kiwango chake sio Consistence ni kinapanda na kushuka tofauti na makinda wenzake.

Tunaona consistence ya kiwango cha De Bruyne wa Man City kikikuwa match to match.

Tumeona Floppy ya Mikh,

Simuoni Mourihno kama mlezi mzuri wa wachezaji wenye vipaji hasa makinda, jaribu kulifatilia hili.

Angalizo:- ni shabiki wa damu wa Man United guys tuwe huru zaidi na tujenge hoja bila kudhihakiana, kutukanana na kuvunjiana heshima, naamini humu sote ni waungwana na mashabiki wa Damu wa Man United.
Tatizo LA Mou ni kuwanyima Uhuru wa chezaji uwanjani. Hilo ndo limefanya wafikie pabaya na Mkhtaryan. Na kuna kipindi hata Martial alishakata tamaa akaomba kwenda sevilla kwa mkopo. Kwa kifupi some times mou huwatumia wachezaji Fulani ktk nyakati Fulani si kwa matakwa ya moyo wake Bali ni kwa sababu hakuna namna. Na anapopata suluhisho,haijalishi huyo mchezaji yupo form au la anamuweka kando kupita kiasi. Rejea Herrera msimu ulopita mpaka tukasema itabidi awe captain.
 
Back
Top Bottom