Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Bora uongee na wewe pengine utaeleweka!
 
Mimi kwangu huwa sikwepeshi Blue ni blue, nyeusi ni nyeusi na kama wewe ni mjinga huwa sipindishi kukuita mjinga;

Ingia hapa uone gigs alivyomponda Van Gal kuwa alimwambia na kumshauri awasajili Mbape na Gabriel Jesus >>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>> Ryan Giggs says he advised Manchester United to sign Kylian Mbappe and Gabriel Jesus

Kwa wenzetu kutoa maoni ni haki ya kikatiba, scholes katumia haki yake ambayo yupo entitled kikatiba ilimradi havunji sheria.


Halafu kama hutaki kuwa Quoted kaanzishe jamii forum yako uwe unadiscuss topics na mkeo ndio utakuwa una mamlaka ya kumkataza asiku-Quote ila hapa ni Bampa to Bampa, Jiwe kwa Jiwe.

Ukiongea Mazuri utaambiwa ukiongea Pumba utaambiwa pia , hivyo hivyo Mimi pia.


GGMU
 
Acha uongo Paul scholes huwa halembeshi kuanzia kwa David Moyes , huyo David Moyes, Felaini, Mata wameshapata Joto yake Manchester United boss David Moyes refuses to slate Old Trafford legends' criticism

Kamuulize Dogo wa arsenal alichofanywa na scholes.

Muda mwingine muwe mnatumia akili
 

pamoja na maoni ninachoshukuru mourinho kamnyoosha next time ataacha shobo kwenye kazi za wanaume wanaume wenye shobo ni kuwapa za uso tu by the way

utaendelea kuqoute kimpango wako mara sijui mourunho atoke ndo kwanza wanampa kandarasi mpya wenye timu na bod wameona kazi yake wenye shobo na ujuaji pigeni madebe tu

kwa kumalizia hapa hamna tulipojadili sijui giggs kumponda vana gal amasajili mbape yeye alichosema kuyumba kwa timu ni ubovu wa makocha wawili waliopita fukuzafukuza hajasema habar za mourinho mbovu

na wakimsema mourinho nnachompenda ni nyundo tu kama trump.
 
Narudia Tena na Tena Ikibidi tunzeni haya maneno ,


Manchester United chini ya Mourinho haiwezi kufika popote, Mbinu za mourinho zipo outdated.


malizia huko chini kwenye maelezo yake yeye,bodi na mkurugenzi.


hapo nshamaliza labda uhamie city ukamuunge mkono pep


" Siondoki United " - Mourinho

Jose Mourinho amesema kwamba amejikita Manchester United na anataka kubaki Man United kwa zaidi ya mkataba wake wa sasa.

Mourinho kwa sasa yupo katikati ya mkataba wake wa miaka mitatu ambao aliusaini mwaka 2016 kuchukua nafasi ya Louis van Gaal.

Mazungumzo kuhusu kuongeza mkataba yalianza mwezi Oktoba baina ya wakala wa Mourinho , Jorge Mendes na Man United.

Alipoulizwa kuhusu mustakabali wake, Mourinho alizielezea taarifa za kwamba ataondoka mwishoni mwa msimu huu kuwa ni ' Takataka ' na ni juu ya Man United kuamua kubaki kwake Old Trafford.

" Kama unataka kuniuliza mimi moja kwa moja kama najiona kuwa Man United msimu ujao , basi nasema kwamba najiona kuwepo hapa msimu ujao ."

" Kama nilivyosema nilipowasili hapa , nitaondoka pindi klabu itakapotaka niondoke, kwasababu sina nia ya kuondoka hata kidogo."

" Lengo langu ni kubaki na kufanya kazi na kuboresha na kuirejesha klabu pale inapostahili."

" Na nataka kubaki, sioni sababu yoyote ya kutotaka kubaki. Bado nina mkataba. Na ndio kwanza nipo katikati ya mkataba wangu. Sipo katika miezi michache ya mwisho."

" Matamanio yangu ni kubaki mpaka pale Wamiliki na Bodi wakiwa na furaha na kazi yangu."

" Nipo katikati ya mkataba wangu. Kama nitasaini mkataba mpya bila shaka hiyo inategemea na klabu, lakini kujikita kwangu ndani ya klabu ni asilimia mia na nataka kubaki."

Pindi alipoulizwa kama anataka kubaki United zaidi ya mkataba wake wa sasa, Mourino alisema," Ndio najiona kubaki hapa zaidi."

" Ni swala la Wamiliki, Bodi ya Wakurugenzi na Ndugu Woodward wana furaha na mchango wangu na wanataka mimi kubaki zaidi ya mkataba wangu wa sasa . Lakini ndio nataka kubaki."
 
Scholes anafanya kazi yake (mchambuzi) analipwa kwa hiyo kazi na Mourinho anafanya kazi yake (to manage Manchester United & protect his players) analipwa na kazi ya uchambuzi ni nyepesi kulinganisha na ukocha ndio maana Garry Neville alisema hatakuja kufundisha tena soka
 
Unajiona ulivyo mweupe kichwani nani kakwambia kuwa na contract ndio Sababu ya kutofukuzwa


David Moyes alikuwa na mkataba wa miaka kibao ila aliitumia miezi 10 tu kama kocha wa Manchester united. Nikuulize Van Gal aliondoka mkataba ukiwa umeisha???


Nikuulize tena Mourinho alivyofukuzwa Chelsea mkataba wake ulikuwa umeisha??? Nikuulize tena wiki kadhaa tumeshuhudia kocha Tonny Pulis wa West Bromwich na Slaven Belisic wa Westham wakitimuliwa , Je sababu ilikuwa ni mikataba ??? Vipi kuhusu Carlo ancelot na Bayern Munich??? Una mfahamu kocha wa simba sport club Joseph Omog ?

Jibu ni moja wote hao walifukuzwa wakiwa na miaka kadhaa kwenye mikataba yao. Unapaswa kujifunza security ya kocha ni team kupata mafanikio tu na sio kupewa miaka 30 kwenye mkataba.


Nimekuona huna hoja, legends wa Manchester especially class of 92 huwa hawana soni hata Mara moja Moyes, Van Gal na Leo mourinho wakizingua wanaambiwa.

Leo mashabiki wengi wa Manchester united wanalalamika team haichezi vizuri ila scholes alikuwa ameshaliona hili long time wakati wewe ukiwa uko kwenu kwenye vibanda umiza ukitemeana mate na wenzako Paul Scholes believes Manchester United will NEVER play entertaining football under Jose Mourinho


Kama nilivyokwambia Legends wa Manchester united especially Paul Scholes huwa harembeshi Kama wewe unavyomtetea mourinho hata anapokosea, hapa Paul Scholes alimpa heko kwa usajili aliofanya Paul Scholes hails Jose Mourinho's 'great signings' at Manchester United


Soma alichosema Legend mwingine baada ya vita vua maneno kati ya Paul scholes na Mourinho na sio wewe kuwa biased wakati huna lolote unalojua
Neville steps into Mourinho and Scholes row over Pogba | Daily Mail Online

GGMU
 


Ferguson mwenyewe aliwahi kukalia kuti kavu kutimuliwa ingia hapa Fergie's winter of discontent

Kilichombakiza ni matokea Tuuuuuuuuuu... Amini usiamini kitakacho mbakiza Mourinho ni matokeo na sio hizo taarabu unazoniwekea hapa. Tunza hii comment yangu
 


Manchester wamewahi kucheza kama barcelona? toka niijue hii timu ni counter za fast mpira matokeo taarabu zipo uswahilin kwenu huko

unakuja kulialia hapa mourinho atoke umemuandaa kocha wewe wa kuchukua nafasi?
 
Duuuu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…