FA imemuuliza meneja wa Manchester United kuelezea kauli zake alizosema kabla ya mechi ya Ligi Kuu Uingereza dhidi ya City uwanjawa Old Trafford
Jose Mourinho ametakiwa na Shirikisho la Soka kuelezea kauli alizosema kwenye vyombo vya habari kabla ya mechi kubwa ya Manchester.
Mreno huyo alishuhudia timu yake Manchester United ikinyukwa 2-1 na mahasimu wao Manchester City kwenye mechi ya Ligi Kuu Uingereza Jumapili ambapo baada ya mechi kulikuwa na tafrani nyingi kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo Old Trafford.
FA tayari imeshaziuliza klabu zte kuhusu mtazamo wao katika tukio hilo, ambapo kwa mujibu wa habari Mourinho alimwagiwa maziwa.
Hata hivyo Mourinho amejikuta kwenye wakati mgumu kutokana na kauli zake alizosema kabla ya mechi, alipoishutumu City kwa kutumia ujanja kwenye mchezo, akisema: "Wakipulizwa kidogo na upepe wanaanguka."
Mourinho pia alidai kuwa City wanatumia "mbinu ya faulo" kuvuruga mchezo alipokuwa akizungumzia mechi dhidi ya hasimu wake wa siku nyingi Pep Guardiola.
Tangazo la FA inasomeka: "FA imeomba uchunguzi wa kauli za Jose Mourinho kwenye vyombo vya Ijumaa Disemba 8, kabla ya mechi ya Jumamosi dhidi ya Manchester City.
"Amepewa muda wa kujibu hadi saa kumi na mbili jioni Disemba 18 Jumatatu."
City walitoka kifua mbele, shukrani kwa magoli kutoka kwa David Silva na Nicolas Otamendi walioongeza pengo la pointi kuwa 11 kileleni mwa msimamo wa ligi.
Lakini klabu zote mbili zinaweza kuwa matatani, na huenda FA ikawashughulikia kufuatia tafrani iliyozuka kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo ambapo wachezaji walikuwa wakitofautiana.
Inasemekana Mourinho aliingia kwenye chumba cha City cha kubadilishia nguo, akiwa hajafurahishwa na muziki uliopigwa baada ya timu ya Guardiola kuibuka na ushindi.
City na United zimepewa muda hadi Ijumaa jioni kutoa majibu kwa FA kuhusu mtazamo wao kwa tukio hilo.