Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mkuu hawa jamaa hawatabiliki kwa sasa wanasilaha nyingine hazieleweki kazi zake nini? ila kwenye vita unashangaa kuona matumizi yake.Mimi napenda watoke hata sale au suluhu japo ni miujiza kidogo lazima mtu alie pale
wale man city wameshaanza kuchoka..ni suala LA muda tu kuanza kutunguliwa,ukimkamata de bruyner na Silva hawafungi goli hata moja
 
Tulizeni ball,ManCity hawana ubavu O/Trafford,watapigwa tu,waulizeni Arsenal mpira mwingi waliocheza uliwasaidia nini, mwasema hawa wapiga kelele wa M/City wanaupiga mpira mwingi, utawasaidia nini wakati goli halipatikani,tusubiri hiyo siku haiko mbali
 
Mimi ningevaa viatu vya Mourinho, ningetumia mbinu zote kumfanya Kevin De Bruyne awe na kesi ya uzururaji ndani ya Uwanja.
mkuu de bruyne asipo kuwa funga basi tegemea Silva hakuachi Silva akikuacha tegemea staling halazi damu basi ikishindikana hapo tegemea aguero atakuumiza

Hapo katikati tegemea kiungo cha man u bila paund 100 watazidiwa sana
 
By the way I attend most of Man city home games and some United games. I have played to decent level in Uk.

I have got some coaching badge in UK in my spare times with many others qualifications in other other areas in UK, USA and Europe.
that prove nothing mkuu, maelezo yako yote yanaonyesha unaongea kishabiki na wala huongei kama mtaalamu wa ukocha.

and by the way hizo cv zako compare na mtu kama mou au pep ni nini? we tulia subiri wataalamu wa mbinu watuonyeshe ujuzi wao.

mwenzako garry neville siku hizi kapunguza kuongea.
 
Hahaa man city ipo vizuri ila ukidhibiti viungo hao wawili de bruyne na silva umemaliza.
Zaidi ya hapo, man city wakikutana na timu yenye foward wenye speed na wanaojua kupiga counter attack watapigwa goli za kutosha cz wana mchezo wa kujisahau beki wote wanapanda juu kushambulia.
 
Timu ipo kwa silva mkuu chunguza vizur

Timu iko kwa De Bryune, angalia anavyocheza nyuma ya line ya ushambuliaji, angalia anavyocheza kwa kupitisha mipata kwa Sterling/Silva pale Aguero au Jesusu wanavyokua wamekabwa.
Pasi zake nyingi ndio zinatengeneza magoli, uyu ukimsumbua tu Man City hawatoweza kucheza mpira kwa uhuru.
 
Hata siku ya mechi ya liverpool zisingefika goli tano kama asingetolewa mane mapema kwa red card. City angeweza kupigwa siku hiyo.
 

Uyu atakua ni Souness anayejua kuichambua Man Utd kwa mabaya wakati ukocha umemshinda.
 
By the way mechi na united nilitegemea ingekuwepo partnership ya lingard, pogba na martial/rashford kwa counter attack cz lukaku siyo mzuri kwa mbio/counter attack. Lakini sasa kwakuwa pogba hayupo sijui itakuwaje
 
Nyota wa Manchester City ametajwa kuwa shakani kwa ajili ya mechi ya Jumamosi Ligi Kuu Uingereza, lakini kocha huyo wa Kireno hasadiki
Jose Morinho anaamini kuwa Pep Guardiola anaongopa kuhusu uwezekano wa kukosekana kwa David Silva kwenye mechi ya jiji la Manchester Jumapili.
Manchester United wataikabili Man City katika uwanja wa Old Trafford wakiwa na lengo la kupunguza pengo la pointi baina ya timu hizo mbili.
 
Silva aliachwa kwenye mechi ya Jumatano Ligi ya Mabingwa dhidi ya Shakhtar Donetsk, na Guardiola amedai kuwa huenda mchezaji huyo akaikosa mechi ya Jumapili.
Baada ya kumsikia Arsene Wenger akisema Alexandre Lacazette ataikosa mechi ya United lakini alicheza Jumamosi, Mourinho anaamini Guardiola naye anafanya ujanja sawa na mwenzake.
Alipoulizwa kuhusu majeruhi wa timu yake, Mourinho aliwaambia waandishi: "Unataka ukweli au unataka nini? Unataka ukweli.
"Ukweli ni kwamba Eric Bailly hatacheza wikiendi, Phil Jones kuna uwezekano, [Marouane] Fellaini kuna uwezekano, Zlatan [Ibrahimovic] kuna nafasi kubwa na [Nemanja] Matic ni majeruhi lakini tutacheza kwa hakika. [Michael] Carrick hana nafasi.
"Nasema kweli kabisa, ni majeruhi lakini atacheza kwa hakika. Hakuna habari za Lacazette au David Silva. Zote ni kweli.
"Wapinzani wetu wote wana matatizo haya. Wana tatizo kubwa lakini mwisho wa siku kila mtu yupo tayari kucheza.
"Wanapenda makuu sana. Sisi ni wanyenyekevu kiasi.
"Tunapokuwa na tatizo tuna tatizo. Wachezaji wanapokuwa majeruhi, ni majeruhi. Nakwambia ukweli."
 
Mkuu Sterling, Otamendi, Sane,walker, Delphi all have improved. Even the keeper is like sweeper (centerback). We will see what happens.
hao wanaonekana baada ya mambo kukaa sawa katikati..magoli wanayofungwa man city yanaonesha uteke wao katika ulinzi..na hata mechi za karibuni ile flow yao imekua tofauti
 
Naogopa ata kukoment, pogba ana red, filaun huwa analetaga ujinga kama gem flan ivi alifungisha goli cjui morinyo atumie trick gan kuwabaka wale vijana daaaah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…