Tetesi
Tottenham Hotspur imeripotiwa kuwa iko tayari kumuuza Danny Rose kwenda Manchester United Januari 2018, ikiwa Mashetani hao watakuwa tayari kutoa paundi milioni 45.
Rose, mwenye umri wa miaka 27, alikosoa sera ya uhamisho wa Tottenham kabla ya kuanza kwa msimu mpya, na licha ya kurudi kutoka kwenye majeraha katika wiki za hivi karibuni, mlinzi huyo wa kushoto amekuwa akiingia na kutoka kwenye kikosi.
Rose, ambaye amezaliwa katika mji wa Doncaster, anaaminika kuwa ana nia ya kurudi kaskazini, na kwa mujibu wa Daily Star, Spurs wamewaambia United kuwa paundi milioni 45 ndiyo ada ya uhamisho ya mlinzi huyo na Spurs itamuuza mwanzoni mwa 2018 kama Manchester itakuwa tayari kutoa kiasi hicho.
Ashley Young amekuwa akifanya vizuri upande wa kushoto kwa United msimu huu, lakini kocha mkuu Jose Mourinho anataka mchezaji mwenye asili ya mlinzi wa kushoto, na kuwasili kwa Rose kutafungua milango kwa Luke Shaw kuondoka Old Trafford.
Rose, ambaye amefanikiwa kuanza mechi moja pekee kwenye Ligi Kuumsimu huu, ana mkataba na Tottenham mpaka Juni 2021.