Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mourinho amesema beki huyo wa kati alipigwa sindano sita za kutuliza maumivu ili acheze mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa.

Pia Mourinho amemshukia kocha wa England Gareth Southgate kwa kumtumia mchezaji akijua kuwa alikuwa majeruhi.
 
Kumpiga mchezaji sindano sita za kutuliza maumivu katika mchezo wa kirafiki, sijapata kuona,” alisema Mourinho.

Alisema Southgate anatakiwa kuwahoji madaktari wa England kwa tukio hilo alilodai halikuwa la kawaida na ametaka uchunguzi zaidi ufanyike.
 
Sikuwahi kuona mchezaji mmoja akichomwa sindano sita kwa wakati mmoja tena katika mchezo wa kirafiki,” aling’aka kocha huyo Mreno.

Ijumaa iliyopita, FA ilitoa taarifa kuwa imeshitushwa na kauli ya Mourinho, na kutetea uamuzi wa mchezaji huyo kuchomwa sindano sita kwa madai kwamba ni jambo la kawaida.
 
Manchester United bado ina dhamira ya kumsajili kiungo wa pembeni wa Real Madrid, Gareth Bale, ambaye anapitia katika wakati mgumu kwenye klabu hiyo.

Awali, Man United ilidai haina mpango wa kumsajili mchezaji huyo kwa kuwa amekuwa akiandamwa na majeraha ya muda mrefu.
 
Kocha wa Man United, Jose Mourinho amedai anaweza kumsajili nyota huyo wa Wales mwishoni mwa msimu. Mourinho anafuatilia kwa karibu maendeleo ya nyota huyo wa zamani wa Tottenham Hotspurs.
 
Mchezaji huyo mwenye miaka 28, amecheza mechi tisa msimu huu na hajacheza tangu Septemba 26 baada ya kupata maumivu makali ya kifua na misuli.

Winga huyo anataka kubaki Real Madrid kwa kuwa ana mkataba unamfunga hadi mwaka 2022, lakini amekuwa katika mazingira magumu na klabu hiyo inafikiria kumpiga bei.
 
kitu
 

Attachments

  • 23622490_10155292865617746_5702532455404256052_n.jpg
    23622490_10155292865617746_5702532455404256052_n.jpg
    58.7 KB · Views: 45
Tetesi
MOURINHO ANAMTAKA WILLIAN MAN UTD


Jose Mourinho anamtaka Willian Manchester Unite ikiwa Mbrazili huyo ataondoka Chelsea majira ya baridi, kwa mujibu wa Sunday Express .
Blues wanataka kumsajili Lucas Moura kutoka PSG, kwa maana hiyo kutakuwa hakuna uhakika wa mchezaji huyo kuendelea kubaki Darajani.
 
Mshambuliaji wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic, 36, anasema kuwa iwapo watu wangejua kuhusu jereha lake, wangeshangaa kwamba anacheza , kufuatia kurudi uwanjani kwa kile kilichotajwa kuwa jeraha la goti alilopata mwezi Aprili(Guardian)

Mshambuliaji wa huyo wa zamani wa Sweden anaamini kwamba Manchester United inaweza kushindana na wapinzani wao wa jadi Manchester City kushinda taji la Uingereza.. (Daily Mail)
 
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amefichua kwamba huwachezeshi pamoja Anthony Martial na Marcus Rashford kwa sababu mchezo wao unafanana (Independent)
 
Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez anasema kuwa kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 24, lazima aonyesha mchezo mzuri kwa miaka 10 ama 15 ili kuweza kufananishwa na mchezaji wa zamani wa Liverpool Steve Gerrard(Daily Star)
 
Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez anasema kuwa kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 24, lazima aonyesha mchezo mzuri kwa miaka 10 ama 15 ili kuweza kufananishwa na mchezaji wa zamani wa Liverpool Steve Gerrard(Daily Star)
Achana nae huyo fundi saa.

Usitegemee atamsifia progba au mou hata kidogo ilhali wamemchabanga.
 
Manchester United inatarajia kuingia sokoni kunasa saini ya mshambuliaji mmoja.

Majina yanayotajwa kuwindwa na Man United ni Antoine Griezmann wa Atletico Madrid na Gareth Bale anayecheza Real Madrid.

Hata hivyo, kocha wa Man United, Jose Mourinho hajui atamsajili mchezaji gani kati ya Griezmann au Bale .

Washambuliaji wote wanamvutia Mourinho na atalazimika kuchagua mmoja ili kwenda kuongeza kasi katika safu ya ushambuliaji Man United.

Mourinho ana Romelu Lukaku na Zlatan Ibrahimovic aliyerejea uwanjani akitokea katika maumivu ya goti yaliyomuweka nje ya uwanja miezi saba.

Mshambuliaji Griezmann na Bale mmoja kati yao anapewa nafasi ya kuvaa uzi wa Man United katika dirisha la usajili Januari, mwakani endapo mpango huo utafanikiwa mapema kabla ya majira ya kiangazi.
 
Back
Top Bottom