Big Fella ni pengo lakini linazibika, nadhani Matic ndo habari akiumia.
Niongelee kuhusu Majeruhi na match tulizonazo this October.
Kwa taarifa zilizosahihi na zilizothibitishwa na timu tutakosa huduma ya Fellain kwa muda wa wiki 2 na Siku kadhaaa kwa maana hiyo hatohusika kwa namna yeyote kwenye game yetu na Liverpool,ni Pengo nitaeleza kwa nini?
Pia ni kweli hatutokuwa na Pogba kwa muda wa miezi miwili na siku kadhaaa hivyo atakosa match zote kubwa za round ya kwanza msimu huu ni pigo hasa nitaeleza kwa nini?
Inaonekana kuwa Majeruhi yameanza kuiandama timu yetu tukiwa tayari tumecheza michezo zaidi ya 10,tukielekea kwenye Peak,kumbuka Ligi ina jumla ya michezo 38,timu ndio inapanda mlima, ndio mana Mou analalamikia haya mapumziko ya Match za kalenda ya Fifa.
Eneo la kiungo limeonekana kuathirika,wachezaji muhimu wawili wanakosekana,Kila mtu anajuwa umuhimu wa Pogba katika kiungo cha Juu na kila mtu anafahamu Super sub Fellain katika kubadilisha na kutuliza mchezo katika eneo la kiungo.
Fellain amemuaminisha kocha kuwa yeye ndio Plan B,binafsi sifurahishwi eneo la kiungo kuchezwa na Fellain na Matic,hamna Chemistry,timu haichezi mpira katika kiungo na mara nyingi huwa tunazidiwa licha ya kushinda,tumeona game za hivi Karibuni,Fellain huwa ni mzuri anapokuja kama sub mana huja kutekeleza kile Mwalimu anachokitaka.
Tunaenda kupambana na Liverpool iliyovizuri katika eneo la Kiungo,Wana wachezaji wazuri Katika eneo la Kati,binafsi humuogopa sana Coutihno,lakini Coutihno huyu sio yule wa msimu uliopita,hana Furaha tena pale Liverpool.
Nimejaribu kusoma soma kuhusu Mou kuelekea match yetu na Liverpool,ameonesha kutokuwa na wasiwasi licha ya kuwa na Majeruhi, anaimani na kikosi chake,anafahamu ana watu wa kazi,ndio mana hatakiwa kuwazungumzia akina Fellain na Pogba ama Caric,Ye anawazungumzia waliofit sasa kuelekea kwenye mapambano.
Matic anatuambia tusiwe na wasiwasi timu itashinda bila uwepo wa akina Pogba na Fellain.
Tuna Under Herera,ambaye watu wengi walikuwa wanajiuliza hatma yake pale united licha ya uwezo mkubwa aliouonyesha last season kupelekea kuwa mchezaji bora wa Club.
Herera anaenda kucheza kiungo cha juu akisaidiana na Mata,Matic akicheza kiungo cha Chini.
Matic na Herera ni watu wa kazi,na vema wanakuja kucheza pamoja kipindi hichi ambacho tunatakiwa kucheza na Liverpool,Totenham,Man City na Benifica.
Kuna mpira flan hivi wa kasi na nguvu eneo la kiungo tuliumiss kwa muda,ule wa kama ule wa Man City vs Chelsea au ule wa Man U vs Chelsea last season,basi game yetu na Liverpool jumamosi tutashuhudia aina hii Burudani,watu wa kazi watawajibika.
Sina hakika kama Mou ataanza na Darmian au Young aliyonekana kucheza vizuri kama beki 3.
Nasikitika huyu muhuni kutokupona haraka Marcus Rojo.
Kwanini Mou hana wasiwasi,siri ni moja tu,Liverpool hawapo vizuri katika match hizi za mwanzoni,hawana kipa, hawana beki nzuri kulinganisha na Man united lakini vile vile strike force yao sio ya kutisha na kulinganisha na Strike force ya Man United,Man City kidogo ndio wa kuwachunga na kuchanga vizuri karata zetu.
Mou anafahamu kwa Liverpool hii haiwezi kuwazuia akina Mikhtaryan,Martial,Rashford, Lingard na Lukaku kutokufunga magoli.
Mou hana wasiwasi na beki zake,wametimia na hamna Majeruhi kinachobaki ni Tactics tu za kocha,Na Mou ni mzuri zaidi ya kocha wa Liverpool.
Binafsi siioni Liverpool ikiizuia Man United kupata ushindi ingawa mpira unadunda na kuna bahati lakini this season Man United tumejiandaa tuna wachezaji wa wastani wenye kupambana.
Shughuli ingekuwa pevu kwa Liverpool kama hawa wanaume wawili Pogba na Fellain wangekuwepo uwanjani Siku hiyo,Mou atakosa Super sub kwenye eneo la kati.
Pengo la Pogba litazibwa vizuri na Herera akishirikiana na kati ya Mata au Mikh.
Kukosekana kwa Super sub kutamlazimu Mou kuanza na Lingard ili Martial atokee Banch as Super sub.
Wachezaji wawili kwa Man United wenye uwezo wa kubadilisha mchezo kwa sasa basi ni Fellain na Martial.
Ndio mana nimeagiza Supu nyingine ya ulimi hapa kwa Mangi niliposikia Aserne Wenger anamtaka Anthony Martial,nikishushia na Coca-Cola ya Baridi.
Nasubiri Match ya Man United vs Man City nitatoa Uchambuzi wangu hasa juu ya kiungo cha Man City.
Ila kwa Match yetu inayofata jumamosi basi mashabiki Wenzangu tuondoe shaka na tuvae jezi zetu,tuwahi kwenye tv zetu na kulipia ving'uzi vyetu,hutakiwi kukosa game yeyote ya Man United kama unataka furahi huu msimu,Mou hajawahi kuniangusha.
Man United 3 - Liverpool 1.