Nemesis
JF-Expert Member
- Feb 13, 2008
- 5,536
- 4,532
Wangeangalia matokeo ya mechi walizokutana wao kwa wao.Naomba kuuliza, hivi mfano leo ingekuwa ndio mechi ya mwisho kombe lingetolewa kwa nani kati ya mu na mc?
Wangeangalia matokeo ya mechi walizokutana wao kwa wao.Naomba kuuliza, hivi mfano leo ingekuwa ndio mechi ya mwisho kombe lingetolewa kwa nani kati ya mu na mc?
Manchester utd 1:2 MadridDaaa lukaku siyo clinical finisher wandugu manake ni game yake ya kama ya NNE hivi anakosa goli LA wazi kabisa. Na hapo anakutana na defenders ambao ni average. Je akikutana na best defenders Wa timu kubwa atapata hizo nafasi za kizembe? Na hapo ndo itapokuja ile ishu ya Lukaku kuendelea kufunga timu ndogo tu.
hata jon champion alisema game is over baada ya goli la pili kuingiaMashabiki walikuwa sahihi.
Lukaku anakosa nafasi nyingi sana mwanzoni mwa mchezo, kabla ya ku-assist na kufunga goli.
Leo nilikuwa namsikiliza Jose mourinho.Anasema hivi
" timu ilipoteza nafasi nyingi mwanzoni, baada ya kipindi cha kwanza nilitegemea kutoka sare ya 1-1 na everton"
"Lakini kipindi cha pili timu ilibadilika na mimi nikaona tunaweza kushinda 2" .
"Goli la 3 na la 4 ni magoli ya bahati, sikutegemea magoli hayo na kwangu sio ya msingi sana. Yale mawili yaishatosha"
Hahaaa! Jose bhanaa..
sasa mkuu unataka wacheze 15 uwanjani??Mou anazingua nae sometimes na tactics zake... Martial , Herrera..wanaanziaje bench ?
Tuashe kelele bhana na sisi,wachezaji kibao wakubwa wanakosaga magoli kama yale..na ukiangalia vizuri alikuwa na lengo zuri sema kipa alikuwa mjanja akaziba goli..hivi kuna mtu aliyekuwa anakosa magoli kama zlatan mwaka jana,na watu walikuwa hata hawamsemi..lukaku mechi sita tu watu washaanza porojo mingi..Daaa lukaku siyo clinical finisher wandugu manake ni game yake ya kama ya NNE hivi anakosa goli LA wazi kabisa. Na hapo anakutana na defenders ambao ni average. Je akikutana na best defenders Wa timu kubwa atapata hizo nafasi za kizembe? Na hapo ndo itapokuja ile ishu ya Lukaku kuendelea kufunga timu ndogo tu.
Hawa sky sports statoo wazushi sana, mimi najua Chelsea ilianzishwa mwaka 2004 sasa hayo magoli ya 1999 huko wameyatolea wapi.?Sky sports statoo wanasema goli la kwanza la chelsea kwenye uefa lilifungwa mwaka 1999![]()
mwaka ambao utd ilichukua treble.
Huwa tunajitukana wenyewe kujibizana habari za mpira na hawa vifaranga.
![]()
FAKE NEWSHawa sky sports statoo wazushi sana, mimi najua Chelsea ilianzishwa mwaka 2004 sasa hayo magoli ya 1999 huko wameyatolea wapi.?![]()
![]()
![]()
![]()
FAKE NEWS





na akakosa goli la waziManchester utd 1:2 Madrid
Unakumbuka goli lilifungwa na nani?
Wote wamesajiliwa kwakuwa wana uwezo.Lakini wanaoweza kucheza ni 11 tu.Jambo la muhimu ni kushinda bila kujali nani yuko benchi au vinginevyo...Mou anazingua nae sometimes na tactics zake... Martial , Herrera..wanaanziaje bench ?
Msimu uliopita zlatan alikosa magoli mengi kuliko aliyofunga, sijui point yako iko wapi?na akakosa goli la wazi
nilipoangalia username tu niligundua hii itakuwa ni comment nzuri kwa ajili ya kuisoma, niliwahi kukwambia ya kwamba lee empire una maarifa makubwa sana ya kutathmini mpira wa miguu na kinachonivutia zaidi ni kwamba huna upendeleo na imenichukua muda mrefu kufahamu ni timu gani unashabikia na kama sijakosea unashabikia timu ambayo ilikuwa na mshambuliaji nisiempenda jimmy floyd hasselbaink (chelsea fc).Ongera Man u mwendo wa dozii....
Kidogo tu kilichoonekana...
...... Walichokikosa Everton ni Romero Lukaku wao tu kumalizia kazi nzuri ya kikundi cha viungo( Davies, Sirgudson, Gana na Shneiderlin). Bado Wayne Rooney mchezo huu ulimhitaji kucheza kama second streker zaidi kutokana na aina yake ya uchezaji.
Baada ya ule mguu wa Valencia kwenda moja kwa moja ndani ya nyavu za Jordan Pickford. Na kabla ya Everton kuutawala mchezo eneo la kiungo katika mchezo huu. Romero Lukaku alishindwa kuweka mipira miwili ya wazi kwenye nyavu za Jordan Pickford. Pamoja na ubora wa Lukaku kwa hivi sasa lakini bado anatatizo la kuzitumia vizuri nafasi zote zinazopatikana, na katika mchezo huu nafasi mbili za wazi akibaki yeye na kipa alishindwa kuzitumia.
Kipindi cha kwanza mchezo ulikuwa chini ya ulinzi wa Manchester United, Nemanja Matic na Marouane Fellaini waliwafanya viungo wa Everton kukubali kuwa wageni pale OT. Maumbile ya viungo hawa wawili wa Manchester united yalifanikiwa kuwatisha viungo wa Everton na kumfanya Rooney kushuka chini na kuongeza nguvu katika eneo la kiungo.
Baada ya kuanza kwa kipindi cha pili hapo ndipo Ilikuja Everton mpya tofauti na ile ya first half. Half time team talk iliwasaidia sana vijana wa Ronald Koeman.... Idrissa Gana, Tom Davies, Morgan shneiderlin na Glyf Sirgudson pamoja na ongezeko la Wayne Rooney katika eneo hilo la kiungo, kuiliwafanya Manchester united kupoteana katikati mwa uwanja na kuukabidhi mcheo wote kwa Everton. Kama sio umahiri wa Davide De Gea basi hesabu za Everton zingekuwa bora katika wakati ule wa umiliki wa mchezo. Pengine pia ni pamoja na kupungua kwa umakini wa Nahodha wa zamani wa mashetani wekundu hao Wayne Rooney, ndiko kuliko sababisha kushindwa kwake kupeleka mipira miwili ya wazi mbele ya de gea.
Baada ya Ronald Koeman kuona amefanikiwa kuufanya mchezo kuwa mgumu, na sasa akaamua kuingiza watu wa kufunguka ili kusawazisha goli. Kumtoa Wayne Rooney mtu aliyekuwa ameongeza wingi wa watu katika eneo la kiungo ilikuwa ni nafuu kwa united. Lakini pia kumtoa Idrissa Gana pamoja na Tom Davies wanadamu ambao waliwafanya viungo wa Manchester united kupoteza mipira muda mwingi na kuwaingiza Kelvin mirales, Calvert Lewin na Sandro Ramirez watu ambao wanakwenda na plan mpya ya kufunguka kutoka katika mpango kazi wa awali wa kulizima eneo la kiungo lote.
Bado tunatakiwa kumuombe Mtalii wa Tanzania Ronald Koeman kuendelea kuishi pale ili Msimu ujao aje tena katika utalii.
Huu ndio ule Msimu wa kuvuna ulichopandaa....