Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ni kweli ame assist lakini...
Ila sijui mkuu kwa upeo wangu finyu Leo nimeona hivyo boss.
Si unajua mitazamo pia imetofautiana

Sent from my HTC ONE using JamiiForums mobile app
Kweli mkuu

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Romelu
 

Attachments

  • IMG-20170716-WA0001.jpg
    IMG-20170716-WA0001.jpg
    37.9 KB · Views: 35
TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI 16.07.2017
Real Madrid wanafikiria kumuuza mshambuliaji Gareth Bale, 27, ili kupata fedha za kumnunua Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Sunday Express)

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Kylian Mbappe atabakia Monaco kwa msimu mmoja zaidi. (Sun on Sunday)

Dau la Chelsea la pauni milioni 88 la kumtaka mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 29, limekataliwa. (Tuttosport)

Kuna wasiwasi kuhusu hatma ya meneja wa Chelsea Antonio Conte, 47, baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kusuasua. (Sun on Sunday)

Liverpool wanatarajiwa kupanda dau jipya kutaka kumsajili kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita, 22 wiki ijayo, baada ya dau la pauni milioni 57 kukataliwa. (Sunday Mirror)

Kumekuwa na wasiwasi zaidi kuhusiana na mustakbali wa Alexis Sanchez, 28, baada ya kusema anataka kucheza Klabu Bingwa Ulaya. (ESPN)

Manchester City wanaongeza juhudi zao za kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Monaco, Benjamin Mendy, 22, kwa pauni milioni 50 hii ni baada ya Tottenham kukataa kuwauzia Danny Rose, 27. (Sunday Express)

Soke City wanasubiri West Ham kupanda dau la tatu kutaka kumsajili Marko Arnautovic, 28. Stoke wanataka pauni milioni 22.5. (Mail on Sunday)

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema kiungo Alex Oxlade-Chamberlain, 23, atabakia Emirates, licha ya Liverpool kumtaka. (Metro)

Leicester City wanataka pauni milioni 40 kumuuza Riyad Mahrez, 26, kwenda Roma. Chelsea na Everton pia wanamtaka winga huyo. (Mail on Sunday)

Riyad Mahrez tayari amekubaliana na Roma. (Mediaset)

Beki wa kulia wa Real Madrid, Danilo, 26, anataka kuhamia Chelsea. (Diario Gol)

Manchester City nao wamejiunga katika mbio za kutaka kumsajili beki wa kulia wa Real Madrid Danilo, 26, ambaye thamani yake ni takriban pauni milioni 21.9. Chelsea na Juventus wanamtaka pia beki huyo kutoka Brazil. (Sunday Times)

Kiungo wa Manchester United Ander Herera, 27, atasaini mkataba mpya wa miaka minne wa mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki kubakia Old Trafford. (Daily Star Sunday)

Andrea Belotti ameiambia AC Milan anataka kujiunga nao, lakini klabu yake, Torino inataka euro milioni 100. Milan wapo tayari kutoa euro milioni 40 pamoja na Gabriel Paletta na M’Baye Niang. (Calciomercato)

Everton wanapanga kutoa pauni milioni 30 kumtaka mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott. (Sunday People)

Winga wa Monaco, Thomas Lemar ameitaka klabu yake ya Monaco kumruhusu kuondoka na kujiunga na Arsenal. (Daily Star).

Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge amekataa kuhamia Beijing Guoan. (Sunday People)

Ivan Perisic ameondoka katika kambi ya mazoezi ya Inter Milan, huku kukiwa na taarifa zaidi kumhusisha na kuhamia Manchester United. (Calciomercato)

Manchester United wanataka Real Madrid imhusishe Toni Kroos katika mkataba wowote wa kumtaka kipa David de Gea. (Daily Mirror)

AC Milan wanataka kumsajili Luka Modric, lakini watakabiliwa na kazi ngumu kumshawishi kiungo huyo kuhamia San Siro. (Calciomercato)

Barcelona wapo tayari kuongeza dau hadi euro milioni 30 kumsajili Paulinho kutoka Guangzhou Evergrande. (Mundo Deportivo)

Inter Milan wanataka kuwapiku Liverpool katika kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita. (Calciomercato)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: Transfers - July 2017
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumapili njema.
 
TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI 16.07.2017

Manchester United wanataka Real Madrid imhusishe Toni Kroos katika mkataba wowote wa kumtaka kipa David de Gea. (Daily Mirror)


Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: Transfers - July 2017
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumapili njema.

Hii vita ya Man Utd na Real Madrid sijui inaelekea wapi, sasa imekuwa ni kukomoana tu. Naona dawa ya kiburi (RMA) wameletewa Jeuri (MU)

N.B: Wote pesa zipo, hakuna kubabaishana hapa.
 
Rooney: "Manchester United are a football club that demands success. Romelu Lukaku has to be strong enough to take up that challenge." [HASHTAG]#MUFC[/HASHTAG]



VIP Rooney anamtisha lukaku au ndiyo changamoto zenyewe
 
Rooney: "Manchester United are a football club that demands success. Romelu Lukaku has to be strong enough to take up that challenge." [HASHTAG]#MUFC[/HASHTAG]



VIP Rooney anamtisha lukaku au ndiyo changamoto zenyewe
Hapana mkuu, hapo Rooney hajamtishia wala nini ila ameongea kitu ambacho ni ukweli. Nimeweka few quotes kutoka kwenye hiyo interview ili uone he was just being honest.

Rooney: "Playing for Manchester United is a test of character. You've got to be strong enough mentally to accept the challenge."

Rooney: "Manchester United are a football club that demands success. Romelu Lukaku has to be strong enough to take up that challenge."

Rooney: "If Lukaku does that then, with the ability he's got, he'll be a success. If he worries about things then it'll be more difficult."

Rooney: "There are standards that you've to keep at Utd. That came from SAF & was passed down through the likes of Giggsy, Gary & Scholesy."

Rooney: "That has been more difficult over the last few years, with some of the players who joined the club. That's not my problem anymore."
 
Sidhani kama ataondoka msimu huu ila ni maandalizi ya yeye kuondoka. Kwa kiasi fulani ataka akacheze Madrid, na Madrid nao ni kama vile wanamtaka.
Bado ana hizo ndoto bado za kwenda Madrid kumbe.
Kwani amesign mkataba mpya.? Au mkataba wake bado unaendelea??


Post sent using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom