Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kama Ferguson angekuwepo angemuuza Rooney tangu 2013,Still Wazza ataendelea kuwa United legend sioni mtu wa kuvunja rekodi yake ya kufunga magoli miaka ya karibuni
Hukumbuki lile saga la kutaka kwenda Chelsea feggie bado alimvumilia wazza alikuwa kwanza hapendi kufungwa pili akitolewa alikuwa ana nuna sio kwa ubaya but ni kuona kwanini anatoka na alikuwa anajua pana kitu atafanya kwa timu. Kuivunja rekodi ya wazza ni jambo gumu ingawa linawezekana tumtakia maisha mema huko toffee pia lukaku akabiliane na pressure ya kuibeba united.Atabaki kuwa ni captain wetu wa nguvu kwa heri rooney kwa heri wazza.
 
Lukaku: "I joined Manchester United because they are the biggest club in the world & are hungry to win the league again." [HASHTAG]#MUFC[/HASHTAG]
 
Kama rooney ameondoka captain atakua nani?? Smalling?? Carrick?? Valencia?? Au herrera??
Carric,Valencia na Herera mmojawapo anaweza kuwa Captain,Valencia na Carric,Valencia nadhani anaandaliwa kuja kuwa Captain wetu msimu ujao baada ya kustaafu kwa Carric.

Herea angeweza kuwa Captain lakini naona kuna sababu za Utaifa.
 
Carric,Valencia na Herera mmojawapo anaweza kuwa Captain,Valencia na Carric,Valencia nadhani anaandaliwa kuja kuwa Captain wetu msimu ujao baada ya kustaafu kwa Carric.

Herea angeweza kuwa Captain lakini naona kuna sababu za Utaifa.
Kwa sasa captain ni caric!! Ila Hapo kwenye utaifa sijakuelewa mkuu!! Ina maana valencia ni mtu wa england??
 
TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI 09.07.2017
Paris Saint-Germain wanataka kuwapiku Manchester City katika dakika za mwisho na kumsajili Dani Alves. Beki huyo kutoka Brazil alionekana kukaribia kuhamia City lakini PSG huenda wakamchukua (Le10Sport).

Wakala wa James Rodriguez amewaambia Liverpool, Manchester United, Inter Milan, Juventus, Manchester City na PSG kuwa wanaweza kumsajili kiungo huyo wa Real Madrid, lakini hakuna kati ya timu hizo iko tayari kutoa euro milioni 75 wanazotaka Real, ambao wanataka kumuuza kutokana na kuwasili kwa Dani Caballos (SPORT).

Beki wa Southampton Virgil van Dijk ameiambia klabu yake kuwa anataka kuhamia Liverpool tu (Mirror).

Manchester United wapo tayari kuwapiga kumbo jingine Chelsea kwa kumsajili James Rodriguez. Chelsea na PSG zinamtaka mchezaji huyo lakini James mwenyewe angependa kwenda kwa Mourinho (Express).

Baada ya kuwazidi kete Chelsea katika kumsajili Romelu Lukaku, Manchester United wanataka kuwapiku tena katika kumsajili kiungo Tiemoue Bakayoko kutoka Monaco, ambao wamekasirishwa na kasi ndogo ya Chelsea kumfuatilia mchezaji huyo. United watamchukua ikiwa watashindwa kumpata Nemanja Matic kutoka Chelsea (The Sun).
James Rodrigues anataka kuhakikisha anaondoka Real Madrid katika saa 48 zijazo ili asisafiri na Real Madrid kwenda Marekani katika mechi za kabla ya kuanza kwa msimu (AS).

Arsenal wamekubaliana maslahi binafsi na Thomas Lemar ya mshahara wa pauni 90,000 kwa wiki, lakini bado hawajafikia makubaliano na Monaco (the Sun).

Celta Vigo wanafikiria kumchukua winga wa Borussia Dortmund Emre Mor ambaye pia amehusishwa na Liverpool (Atlantico).

Dani Ceballos, 20, amekubali mkataba wa miaka sita kujiunga na Real Madrid kutoka Real Betis na atakamilisha mkataba wa euro milioni 18. Barcelona walikuwa ‘wakimchombeza’ mchezaji huyo (Marca).

Antonio Rudiger anakaribia kukamilisha uhamisho wake kutoka Roma kwenda Chelsea kwa pauni milioni 34 na mkataba utakamilika katika saa 24-48 zijazo (Sky).

Arsenal wameweka wazi kuwa hawatomuuza Alexis Sanchez au Alex Oxlade- Chamberlain kwenda katika timu yoyote hasimu ya EPL. Sanchez ananyatiwa na Manchester City huku Oxlade-Chamberlain akihusishwa na Liverpool (Daily Star).

Arsenal watakuwa tayari kumuuza Alexis Sanchez kwenda Manchester City ikiwa tu watatoa pauni milioni 80 (Mirror).

Arsenal wameongeza dau lao hadi pauni milioni 40 kutaka kumsajili winga Thomas Lemar, 21 kutoka Monaco, baada ya pauni milioni 35 za awali kukataliwa (L’Equipe).

Meneja Antonio Conte atarejea Chelsea siku ya Jumatatu kutoka likizo na kutaka mazungumzo na klabu hiyo kuhusu kushindwa kumsajili Romelu Lukaku kutoka Everton (Express).

Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney, 31, amefanya vipimo vya afya Everton (Sky Sports).

Zlatan Ibrahimovic, 35, huenda akapewa mkataba mpya na Manchester United baada ya kupona jeraha la goti (Mirror).

Tottenham wamesema kiungo wao Eric Dier, 23, hauzwi kwa bei yoyote. Hii ni baada ya kuhusishwa na Manchester United kwa pauni milioni 50 (Mail).

Jose Mourinho ameongeza juhudi za majadiliano kutaka kumsajili James Rodriguez, 25, kutoka Real Madrid. Real wanataka pauni milioni 62 (Independent).

Newcastle wamekuwa na mazungumzo na Middlesbrough ya kutaka kumsajili winga Adama Traore, 21 ambaye huenda akagharimu hadi pauni milioni 20 (Chronicle).

Newcastle wapo tayari kulipa euro milioni 20 kumsajili Andreas Samaris kutoka Benfica (O Jogo).
Kiungo wa Bayern Munich Douglas Costa anakaribia kukamilisha uhamisho wake wa mkopo kwenda Juventus na huenda akahamia moja kwa moja baadaye kwa euro milioni 40 (La Stampa).

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: Transfers - July 2017
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Uwe na Jumapili njema.
 
Jaman Lukaku sio straika tulomuhitaji aisee japo ni straika mzuri lkn simuobi akileta old glory pale OT labda tukifanya additn tena kwa kumuongeza ht Morrata
Nipo safarini acha niiweke hii as kiporo nitakuja kukujibu,na tegemea makubwa kutoka kwa Lukaku.

Kama ni washambuliaji wa Mambo mengi pale mbele tayari tunao viungo wa kufanya hiyo kazi,Pogba,Herera,Mikh,Matta na Rashford hata Martial.

Ila tulimuhitaji mtu anayelijuwa goli vizuri ambaye kazi yake ni moja tu,kufunga na Lukaku ana hii Sifa.

Lukaku ni mzuri mbele ya goli,angalia magoli yake aliyoyafunga last season.

Sasa subiri hawa wakata kachumbari wafanye yao afu waweke pale mbele ndio utaijua kazi ya Lukaku.

Ndio mana nasema next Season namtabiria makubwa sana Pogba kung'aaa maana anaenda kuwa free player ndani ya uwanja kitu kitakachomfanya aonyeshe uwezo wake halisi.

Basic Combination inaanzia kwa Pogba na Lukaku,ni nafasi ya wachezaji Wengine kujiongoza
 
Nipo safarini acha niiweke hii as kiporo nitakuja kukujibu,na tegemea makubwa kutoka kwa Lukaku.

Kama ni washambuliaji wa Mambo mengi pale mbele tayari tunao viungo wa kufanya hiyo kazi,Pogba,Herera,Mikh,Matta na Rashford hata Martial.

Ila tulimuhitaji mtu anayelijuwa goli vizuri ambaye kazi yake ni moja tu,kufunga na Lukaku ana hii Sifa.

Lukaku ni mzuri mbele ya goli,angalia magoli yake aliyoyafunga last season.

Sasa subiri hawa wakata kachumbari wafanye yao afu waweke pale mbele ndio utaijua kazi ya Lukaku.

Ndio mana nasema next Season namtabiria makubwa sana Pogba kung'aaa maana anaenda kuwa free player ndani ya uwanja kitu kitakachomfanya aonyeshe uwezo wake halisi.

Basic Combination inaanzia kwa Pogba na Lukaku,ni nafasi ya wachezaji Wengine kujiongoza
Safiri salama [HASHTAG]#GGMU[/HASHTAG]
 
Binafsi ningependa mkongwe huyu kwa heshma yake angebaki mpaka yeye mwenyewe akasema jamani panatosha hapa miguu haina kasi tena wacha nikatafute pa kupumzikia yaani naona kama tumemtosa flan hivi ila ndio hivyo mambo yanabadilika. Wazza kafanya mengi penye club hii kachukua karibu vikombe vyote alivyo pigania kwa heri rooney kwa heri captain kwa heri wazza siku zote ulipenda kuona timu inashinda ulipigana kiukweli hata usoni uchungu wako ulionekana kila la kheri wazza.
Kama ilivyokuwa kwa Gigs lakini ndio hivyo,muda na mazingira hubadilika,now angeendelea kubaki Man U ingemlazimu kugombea namba na chipkizi,kushusha mshahara wake na kuanza kuzoea banch vitu ambavyo asingekubaliana navyo kutokana na hadhi yake ndani ya Club na ukubwa wake na baadaye ingeleta matatizo na wachezaji sasa Mou hakutaka hiki kitokee that y akamtaka yeye mwenyewe afanye maamuzi
 
Lukaku: "I joined Manchester United because they are the biggest club in the world & are hungry to win the league again." [HASHTAG]#MUFC[/HASHTAG]
So i will try to perform better than before!

The man is really happy
 
Back
Top Bottom