Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Msimu ulioisha pamoja na zlatan kupata mabao hayo ila pana nafasi zaidi ya kumi za wazi ambazo alikosa aidha kwa umri yaani hakuwa mwepesi kivile. Sasa lukaku bado kijana na kasi anayo akishirikiana na vile viberenge mbona patanoga tu zile volley za Pogba patakuwa patamu.
 
BREAKING: Manchester Utd have agreed a fee in the region of £75m for Everton striker Romelu Lukaku.

(source: BBC Sport & Sky Sports)
Mourinho ni jeuri na huwa anakuwa na alternatives linapokuja kwenye suala la usajili,well done!
 
Mkuu inaonekana unamkubali zaidi morata na usajili wa lukaku kuja utd haujakuvutia sana. Mie nina imani na mourinho zaidi hata ya wachezaji wake,naona poa tu.
 
Mkuu unafkiri lukaku anaweza kuendana na mfumo wetu?je ni sahih kununuliwa kwa nzigo mkubwa ivo Wa pesa?
Yeah Lukaku anafit katika Mifumo ya Mou yote na ondoa Wasiwasi kuhusu kuperform akiwa na United,tegemea magoli mengi sana kutoka kwake,anakuja kuwa goal Socre machine,atatengenezwa na kupewa majukumu ya kufunga tu kazi kubwa itafanywa na Viungo Zaidi ya 4 katika kumlisha.

Nasubiri kuona kiungo tutakayemsajili mana lazima tusajili kiungo mwingine.

Mou anajuwa upungufu wa magoli hivyo hili atalifanyia kazi mapema katika hii pre season Zaidi hasa katika kutafuta Mifumo ambayo anadhani itaifanya timu kushinda magoli mengi Zaidi.

Pogba,Lukaku,Rashford,Martial,Martial na Felain hapa tunatakiwa kupata washambuliaji watatu katika mfumo wa 4-3-3 mana ndio mfumo ambao Lukaku unaweza msaidia sana kuweza kuperform or 4- 3- 2-1.

Ila naiona Man U ikitumia Zaidi 4 - 3 kama basic formation Yetu.

Kuhakikisha kuwa hatufungwi magoli mengi Zaidi.

So our formation will be,4-3- 3,4-3-2-1,4-4-2,( 4-5-1 ).

Tutakuwa na kachumbari sana ya Viungo pale mbele.
 
Mkuu darmian haondoki kweli ??? Namba 3 Si ya blindi au
 
Mkuu unafkiri lukaku anaweza kuendana na mfumo wetu?je ni sahih kununuliwa kwa nzigo mkubwa ivo Wa pesa?
Mzigo,kwangu binafsi Lukaku hana thamani hiyo lakini ndio hivyo soko limebadilika sana na tunahitaji kuwa na Mshambuliaji wa uhakika zaidi hatuna jinsi Morata ndio kama hivyo,na tukiendelea kuchelewa tunaweza mnunua kwa Zaidi ya hiyo bora hivyo na huku tukienda pre season tukiwa na uhakika na mshambuliaji.

Lukaku kwangu tungemchukua kati ya 60 na 50 or 45.
 
Watachezaje ndugu na huku wote ni 9
Wanaweza kucheza wote,Morata ana asili ya kiungo mshambuliaji hivyo anaweza pia kucheza kama namba 10 au 11.

Lakini sitegemei kusajiliwa kutokana na bei zao sokoni.

Ikitokea hivyo kwetu itakuwa ni faida na sijui nini kitatokea tunaweza kutawala soka la Ulaya next season mana tutakuwa tunapiga ndani na nje.

Ila nadhani Mou anaandaa sana sana akina Rashford,Martial na kale ka Lingard

Mmoja nna uhakika mana kuna uwezekano wa kurudi kwa Ibra January kama atakuwa amepona Completely mana maendeleo yake ni mazuri na tuliogopa kumuongezea mkataba kutokana na aina ya majeruhi yake katika umri wake,na ndio mana tumempa nafasi ya kumtibia na kuendelea kuwa nasi.

Na kuruhusu Rooney.
 
Mkuu darmian haondoki kweli ??? Namba 3 Si ya blindi au
Blind ni kiraka lakini Zaidi anacheza kama kiungo mkabaji (namba 6) na ndio mana hatujamuuza kwa ajili ya hizo namba hasa 4 na sita.
Namba 3 tuna luka Shaw,Darmian,Rojo.

Namba mbili ndio tuna upungufu tuna mchezaji mmoja tu Valencia na namba Sita tuna Carick na Herera tu kiasili.

Pogba sio kiungo mkabaji ila ni kiungo mshambuliaji kama tunaanza kushambulia kutokea katikati ya uwanja huku kazi ya ukabaji ikifanywa Zaidi na namba 4 na 5 ambao hupanda juu kusaidia ukabaji.

Pogba kiasili ni namba 8 na 10 ndio anafiti Zaidi au kucheza kama mshambukiaji anayetokea Pembeni namba 11 au 7.

Nne na Tano sasa tuna Lendorf,Baily,Rojo,Blind hivyo kama hatutosajili kiungo mkabaji basi tunamsogeza Blind kwenda kusaidia kucheza namba 6 yeye na Herera mana Carrick umri umeshamtupa mkono.

Viungo washambuliaji tuna Mata,Pogba,Fellain,Mikh na Lingard.

Huku washambuliaji tukiwa na Rashford na Lukaku.
 
Mpira wa rojo ni kama wa Ramos .....inabidi aanze kuaminiwa bana ... Watoto wa kilatin huwa na roho mbaya mfano Costa tevez .
Mi binafsi naipenda shughuli ya Rojo sio mchezo muhuni sana huyu Mtoto na alifit sana alipocheza na Baily.

Ila ukitaka tukumbuke Man U ya Vidic na Rio basi 4 na 5 wacheze Baily na Lendorf hii combination haina mfano ndugu yangu,hawa watu wana roho mbaya sana na ni makatili haswaa,hawana mchezo na ukitaka sherehe ipendeze Zaidi basi namba tatu acheze Rojo afu mbili Valencia nina uhakika tunaweza kufungwa kwa tabu mana go lini sina Wasiwasi na De Gea,Wasiwasi wangu tunaweza tusione tena kile kiwango cha De Gea mana hatokuwa na kazi kubwa katika huo Ukuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…