Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Siyo utani na ana mashuti anapiga vichwa kubwa Mourhnio huwa hakosei kwenye usajili wa strikers na ndiyo maana katwaa mataji mengi sana

Musimu uliopita alilia sana kwanini Chicharito aliuzwa na alidai angelikuwepo vile vyumba angefunga zaidi ya +20 na Manutd wangelishinda ubingwa wa EPL

Ili kutwaa ubingwa wa EPL Tunahitaji strikers wawili jumla ya mabao kwa musimu yasipungue +50 ukiongezea na midfielders basi yasipungue 80+

Morata na Lukaku kwa pamoja lazima wafunge 50+ na ndiyo maana bila kumsajili Morata ubingwa wa EPL tusahau

Waliopo hawezi kufunga 20+ kwa musimu ili ukijumlisha na Lukaku yafikie 50+ kwa strikers tu kabla ya midfielders
Ila vyanzo vinaripoti kuwa united wameachana na Morata.
 
Ila vyanzo vinaripoti kuwa united wameachana na Morata.
Kama ni kweli bado tunahitaji striker mwingine ila nijuavyo vyanzo ni vyanzo

Tofauti ya offer ya Manutd na Real Madrid ni £5mill nitashangaa sana kama wiki hii ipite na Alvaro Morata hajasajiliwa na Manutd
Ubingwa wa EPL itabidi tusahau musimu huu ujao

We need real fire power na Lukaku pekee hatoshi!
 
Teh! Teh! Teh!
Screenshot_2017-07-06-14-46-36.jpg
 
Siyo utani na ana mashuti anapiga vichwa kubwa Mourhnio huwa hakosei kwenye usajili wa strikers na ndiyo maana katwaa mataji mengi sana

Musimu uliopita alilia sana kwanini Chicharito aliuzwa na alidai angelikuwepo vile vyumba angefunga zaidi ya +20 na Manutd wangelishinda ubingwa wa EPL

Ili kutwaa ubingwa wa EPL Tunahitaji strikers wawili jumla ya mabao kwa musimu yasipungue +50 ukiongezea na midfielders basi yasipungue 80+

Morata na Lukaku kwa pamoja lazima wafunge 50+ na ndiyo maana bila kumsajili Morata ubingwa wa EPL tusahau

Waliopo hawezi kufunga 20+ kwa musimu ili ukijumlisha na Lukaku yafikie 50+ kwa strikers tu kabla ya midfielders

Nakubaliana na wewe,tunaitaji washambuliaji wawili watakaofunga magoli 60+,hawa wengine watachangia kwasababu wengi wao wameonyesha uwezo mdogo msmu uliopita.
 
Morata na lukaku Nani anatufaa zaidi pale mbele
Habari mashabiki Wenzangu wa Man United.

Nimekuwa kimya kidogo kwenye hili Jukwaa lakini ni mfatiliaji na msomaji wa taarifa zote zinazoletwa humu za timu Yetu pendwa.

Naomba nijibu hili swali la Mdau Mwenzetu juu ya Nani anatufaa Zaidi kati ya hawa wachezaji wawili ambao tumewafukuzia kwa muda mrefu.

Baada ya kumalizika kwa michuano ya mashindano ya Msimu uliopita,Mou alianisha maeneo mbali mbali yaliyoonyesha upungufu mkubwa na kusababisha kikosi chake kukosa mafanikio yaliyotegemewa.

Eneo la Ushambuliaji wa kati likichukua nafasi kubwa,Mou katika analysis zake aligundua ufinyu wa mabao katika timu Yetu ndio uliopelekea timu kutokufikia mafanikio yake kama ilivyotegemea hii inatolana na kupata sare nyingi sana kuliko ilivyo ada,badilisha zile sare kuwa ushindi nadhani now tungekuwa tunaongea mwngine,hivyo akaweka mahitaji makubwa ya kupata Main Stricker katika kikosi chake kwa Msimu wa 2017/2018.

Kisha akatoa list ya Wachezaji anaowataka katika nafasi tajwa akianisha uwezo na sifa zao kila mmoja kwa bodi ya Wakurugenzi kutokana na Mipango yake.

Majina ya Moratta,Stricker asiyetumika sana katoka kikosi cha Real Madrid na Romeo Lukaku Stricker aliye perform vizuri msimu ulioisha yakipewa nafasi kubwa kutua katika kikosi cha Man United.

Bahati Mbaya Mou sio mfuasi wa mfumo wa 4-4-2,hivyo sioni uwezekano wa kusajiliwa wote wawili kwa wakati mmoja.

Na kama tukifanikiwa kusajili wote wawili basi ni kwa ajili ya Uefa Champion ,mshambuliaji akitumiwa katika ligi kuu na mwingine akitumika Zaidi Ulaya wote wasaidiwa na Kijana Rashford.

Wachezaji wote hawa Mou anawahitaji kwa wakati mmoja kama soko litaruhusu na kama wanapatikana na kama ikishindikana basi walau mchezaji mmoja wao apatikane katika kikosi chake.

Kwa nini Morata? na kwa nini Lukaku?tukumbuke hawa wote wanacheza nafasi moja ya Ushambuliaji wa kati kiasili (no.9).


Tuanze na Morata, Mou anatamani sana kama tutafanikiwa kumsajili Morata kuliko Lukaku,record za ufungaji wa mabao za Morata zinampa nafasi kubwa kutakiwa na Mou,record zake toka akiwa Juve na sasa Madrid na uwiano mzuri wa idadi ya Match na ufungaji wa magoli.

Technically,Morata ni aina ya mshambuliaji wa kati mwenye sura ya kiungo mshambuliaji hivyo ni advantage kuingia katika mifumo mingi ya Makocha,kama mshambuliaji namba 9 na kama mshambuliaji namba 10.

Ukiwa na Morata kama mshambuliaji utahitaji Zaidi Viungo washambuliaji na timu itakuwa na magoli mengi Zaidi na kumiliki sana mpira, aina ya soka la Barca

Lakini ni Mzuri pia kwenye mashambulizi ya kushtukiza na kwenye kukaba eneo la Juu,Morata anahitaji Viungo wachache kuweza kuifanya kazi yake vizuri pia ni Mwepesi na ndio mana mna ni rahisi kuonekana pande zote za uwanja.

Pia Moratta ni mshambuliaji mwenye Ladha,Fundi wa Mpira na Mwenye magoli matamu/magoli ya Video,na ndio mana ameweza kufit katika Ligi ya Spain licha ya kucheza kwa dakika chache.

Kwangu ukiniambia nichague nani kati ya Morata na Lomeo Lukaku basi Moratta nampa nafasi kubwa kutokana na aina ya wachezaji tulio nao,hawa wote watasaidiwa na Marcus Rashford ambaye sasa atapewa Jukumu kamili la kuwa mshambuliaji msaidizi (no.10).


Kwa nini Lukaku,kama alivyo Morata,Lukaku pia ni Mshambuliaji aliyekamilika katika eneo la kucheka na nyavu,wote tunajuwa record zake akiwa Chelsea na alichokifanya msimu ulioisha akiwa na Everton,huhitaji kuhadithiwa.
Sina tatizo kama pia tukifanikiwa kumsajili.

Uzuri wa Lukaku ni kutokana na umbo lake kubwa linalomfanya kukabwa na mbeki Zaidi ya wawili kwa wakati mmoja lakini pia uwezo wake wa kufunga kwa kutumia kichwa.

Technically Lukaku ni aina ya mshambuliaji asiye na mambo mengi mbele ya goli ye kazi yake ni kufunga tu,sio Fundi sana wa mpira ila ni mpambanaji haswaa.

Lukaku ni mshambuliaji anayehitaji timu kuwa na Viungo wengi pale mbele hasa kiungo mkabaji katika eneo la Mbele kama Fellain.

Hapa nieleweke,ukiwa na Moratta timu itahitaji kuwa na Viungo wachache na mshambuliaji msaidizi. (8,9,10),mfano Pogban,Morata na Rashford au Matta na timu itang'aaa vilivyo.

Ukiwa na Lukaku inabidi timu kuwa na Viungo wengi kwa maana ya ongezeko la kiungo mmoja mkabaji mfano Lukaku,Pogba na Fellain.

Udhaifu wa Lukaku ni Mzito na si mkabaji,lakini ni mfungaji aliyekamilika mwenye kujuwa majukumu yake.

Ila ni mchezaji aliyetuonyesha kuwa ana kitu ndani ya EPL.

Sina shaka nimesoma habari za kuja kwa Lukaku am happy najuwa akili ya Morihno katika kukubali usajili wake tayari ana option na ndio mana alipeleka majina yao wote wawili.

Man United inarudi kucheza kama ilivyocheza Chelsea ya Msimu wa 2003/4 ikiwa na Drogba.

Tunaweza tusifungwe au kufungwa michezo michache sana na droo za kutafuta,nategemea mwisho wa msimu tunaweza kuwa na point za 90+

Baada ya Usajili wa Lukaku sasa nina uhakika tutalazimika kumsajili Matic na kuachana na usajili wa Winger Persic wa Inter Milan.

Karibu Old Trafford Romeo Lukaku a New no. 9.
 
Naona habari ya Lukaku haijakaa vizuri kabisaa...Lukaku is not that massive striker...huwa hana jipya in big games...mlimuona game ya Chelsea msimu uliopita...sawa anaweza akakupa hata hat trick kwenye game za lower table teams...kwa mtazamo wangu Rashford ni bora zaidi ya huyo Lukaku...labda kama tutamleta na Morata pia
 
Back
Top Bottom