Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

SEHEMU YA PILI
Wiki ya kwanza ya mwezi wa 12, 1992 Ferguson alikua kwenye ofisi ya mwenyekiti wa timu kipindi hicho bwana Martin Edward wakijadili mahitaji ya club hasa kwenye suala la ushambuliaji, waliwaongelea wachezaji wengi sana lakini jina lililokua limetawala na kuja kichwani mara kwa mara ni la mfaransa Eric cantona aliyekua akiichezea Leeds united.
Gerald Houllier alikua rafiki sana na Ferguson, pindi anafundisha PSG alikua akimtaja taja na kumsifia sana cantona, mwanzoni mwa mwezi September Manchester waliifunga leeds goli 2-0 lakini mabeki wote wawili wa kati wa Manchester Steve bruce na Pallister baada ya mechi kuisha waliingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kukiri wazi jinsi cantona alivowasumbua "we couldn't get close to him"alisema Bruce.

mazungumzo yakiwa yanaendelea kati ya S.A.F na Edward kuhusu usajili wa mshambuliaji simu ya mezani ofisini ikaita alikua ni Bill Fotherby mwenyekiti wa Leeds utd akiulizia kama utd itakua ipo tayari kuwauzia full back wao Dennis Irwin. Off course ombi lake likakataliwa lakini katika mazungumzo Edward alimuuliza Fotherby kama na wao wanamchezaji yyte ambae wapo tayari kumuuza hasa striker wao Lee chapman (ambae ni mchezaji pekee hadi sasa kuifunga Manchester akiwa na timu sita tofauti) lakini Fotherby akakataa. Ferguson alichukua kipande cha karatasi na peni mezani kwa Edward na akaandika maneno yaliyokua yanamtaka Edward amuulize Fortherby uwezekano wa kuwaulizia mfaransa cantona ambae inasemekana ni mkorofi, msumbufu na hajatulia kwenye timu. Fotheby hakutoa jibu la moja kwa moja ila aliahidi kupiga tena simu muda mfupi baadae, baada ya Fotheby kukata simu Edward na Ferguson wakaagana na Ferguson akaondoka.
Muda mfupi baadae Fotheby kama alivoahidi kweli akampigia simu Edward kumjulisha kuwa ombi lake la kuwauzia cantona limekubaliwa. Ferguson akiwa kwenye gari anaelekea kwake simu yake ya mkononi ikaita hakua mwingine zaidi ya Edward, "WE HAVE GOT HIM" then akamwambia ajaribu kukisia bei yake, msikilize babu hapa: "Trying to be realistic i suggested 1.6 mill, wrong, so then i rattled off three or four more attempts. They were all so far off the mark, it was like one of those tv quizzes. Higher,lower, not even close. Eventually the chair man declared the true figure, 1mill. I just couldn't believe it, 'that's an absolute steal' i blurted out"

Media,pundits na mashabiki wengi tu walidhani na kusema kuwa huu ni usajili kichaa, unamsajili vipi mchezaji kama cantona ambae muda mwingi anakua anatumikia adhabu, msumbufu, mgomvi na kaidi? muda wote alikua kwenye migogoro na timu, utawala na wachezaji wenzake, hata kwenye timu yake ya taifa hali iliku ni hivyo hivyo. sifa yake kuu ni alikua hawezi kukaa na timu moja kwa muda mrefu, hata akiwa anahojiwa mara nyingi alikua anagombana na waandishi. kuna kipindi alishawahi muita kocha wa timu yake ya taifa bwana Henri Michel "sac a merdi" (A shitbag).

mwanzoni wakati anafika England alidhani anaenda kusajiliwa na shefield wed chini ya kocha Trevor Francis, msikie hapa: " i was there for one week, and i thought that i was there to sign. my lawyer was there and he spoke to try and find a way with my contract. I trained and played in friendly game, we won 4-3 and i scored three goals. After one week, Francis asked me to spend one more week on trial. There were not a lot of foreigners in england then, may be some from the north europe but not many from the south. may be they were suspicious, but i was a french international. and shiffeld wed wanted more time to decide about me!! That was not a very good way to go about things"

mwisho wa siku akajikuta yupo Elland road akiitumikia Leeds utd iliyokua ikinolewa na kocha Howard Wilkinson. Leeds wakashinda taji lao la ligi kuu (first division)na cantona kuibuka shujaa wao. cantona alicheza mechi 35 na kufunga magoli 14, kama kawaida bodi ya timu ikashindwa kuendana na mambo ya Eric na kutaka either kumuuza au kumtoa kwa mkopo, ila hofu kubwa ya kocha Wilkinson ilikua ni endapo Eric akaondoka kwa mkopo basi itakua ndio mwisho na hatarudi tena Leeds hivo kupoteza pesa nyingi walizokua wamewekeza kwake.

Ila upande wa cantona ye aliona mambo tofauti: " i had a bad relationship with the manager Wilkinson. We didn't have the same views ob football. I was more like a Manchester footballer. at Leeds football was played the old way. I think you say kick and then rush. But it was very important to play for Leeds at first because i learned a lot with this kind of football and we had success"

74efb77140f31f61bbeb9ebba0e1aa63.jpg

kama S.A.F alivosema kuwa alikua kama kamuiba japo kipindi hicho mashabiki wa Manchester walikua na hofu na mchezaji wanaoenda kumpata na wakawa wanajiuliza atakaa muda gani kwenye timu. mechi yake ya kwanza ilikua ni Manchester derby jumapili ya tarehe 6 December 1992 nyumbani OT. alitokea benchi kwenye kipindi cha pili, aliposimama tu uwanja mzima ukamgeukia, alisogea hadi kwenye touchline, kifua kakitunisha, kola ya shati kaisimamisha huku macho yake yakizunguka kwenye jukwaa mbalimbali ndani ya Old Trafford. kitendo cha kusimamisha kola cantona kakizungumzia: "i put my shirt on, it was a cold day, the collar stayed up so i kept it like that. we won, so it became a habit to play with my collar up"
Goli lake la kwanza alifunga darajani Stamford bridge kwenye droo ya 1-1 na chelsea (ilikua ni mechi yake ya tatu), then siku ya boxing day dhidi ya Sheffield wed ugenini, hadi dakika ya 60 Manchester ilikua ishalia 3-0 lakini mwamuzi anakuja puliza filimbi ya mwisho ubao ulikua unasoma 3-3 huku cantona akiwa kwenye score sheet. hii mechi ilikua kama ndio ufufuo kwa Manchester, maana katika mechi tano zilizofuata tukafunga jumla ya magoli 15, tulishinda mechi nne na kufungwa moja ugenini Portman road dhidi ya Ipswich town.

Improvement kwenye timu ilionekana maana sasa kila mchezaji alikua na uwezo wa kufunga na kuassist cantona, giggs, Hughes, Irwin, Sharpe, McClair, Parker, Kanchelskis na Ince baada ya kufungwa na Ipswich, Manchester ilikua ya pili kwenye msimamo,point moja nyuma ya vinara Aston villa.
hadi msimu unaisha united ilikua kileleni huku ikiwa imeshinda mechi saba mfululizo, hatimaye united ikashinda ubingwa wa kwanza wa ligi kwa mara ya kwanza kwa takribani miaka 26, ubingwa huo ulipatikana siku ya jumapili may 2 1993 siku ambayo Manchester ilikua haichezi. Ushindi wa Oldham athletic dhidi ya villa ndio ulioipatia united ubingwa maana villa sasa asingeweza kuikuta united kwa points. cantona akawa kachukua ubingwa mara tatu mfululizo akiwa na timu tatu tofauti.

sherehe zikaanza, wachezaji, mashabiki wakasherehekea usiku kucha na wengine hadi siku iliyofuata. Lakini jumatatu jioni kulikua na mechi ya kukamilisha ratiba old Trafford.
msikilize cantona: " we had been crowned champions of England by default the day before, now we wanted to play like champions. The lid was ready to jump off, mouth was ready to open. it was a feelings of the greatest delight and madness. The songs that come from the depths of the crowds were so beautiful, that for an instant, i didn't want to have to play, but would have liked to have stand still somewhere and just listen. At a quarter to seven steve bruce led us onto the pitch and the voice of the people became clearly heard. Keny daglish had claimed that blackburn would beat us. Loudspeaker systems had started with Queen's' WE ARE THE CHAMPION' and now it was simply the best by Tina Turner. After a few bars it looked as though paul ince was going to start a dance on the field. Blackburn made a fast start,but then 3 goals for Manchester united.
I went back into the dressing room, the champagne could flow all night. my shower was loong and enjoyable. I didn't go to the celebrations which were given in our hon our by a supporters who owned a hotel in town, i wanted to get home to leeds to be with my young son"


Goli la tatu la Manchester lilifungwa kwa free kick kali ya Garry Pallister, kabla ya hapo alikua ndio mchezaji pekee ndani ya uwanja ambae alikua bado hajafunga goli kwenye ligi msimu huo. CAN-OPENER kama alivoita S.A.F akimaanisha cantona ameshawasili. cantona akatokea kuwa kipenzi na shujaa cha wengi kuanzia mashabiki hadi team mates wake, tangu kipindi cha kina Charlton, Law na Best.

msikilize Roy kean: " “I liked him immediately. Sure, he was different. He tended to do his own thing in training, an indulgence Ferguson and Brian Kidd permitted. He had his own warm up routine, and stayed out practicing his finishing after 5-a-side. Eric also had a fierce temper which sometimes flared up on the training ground. He and Schmeichel in particular found themselves at odds. Fists were raised on one or two occasions.
Behind the enigma, Eric was a great pro, very serious about his football, knowledgeable about the game. Collar turned up, back straight, chest stuck out, he glided into the arena as though he owned the ****ing place. Any arena, but nowhere more effectively than Old Trafford. This was his stage. He loved it, and the crowd loved him. The players loved him too, for many reasons. Most importantly, he got the job done.”


ITAENDELEA SEHEMU INAYOFUATA
 
Real Madrid wana imani kumsajili De Gea na huenda wakamtumia James Rodriguez kama chambo cha kukamilisha usajili huo.
 
Pamoja na Lukaku kuwa mfungaji bora wa ligi lakini Mourhnio angependelea kumsajili Griezmann badala ya Lukaku

Screenshot_2017-05-17-18-04-56.png
 
Pengine Oblak ni kipa namba moja duniani lakini kumng'oa Atletico inahitajika £85 au labda kitita kipunguzwe sana.

Screenshot_2017-05-17-18-04-28.png
 
James Keane akiwa dimbani akichezea Burnley. Manutd ilimuuza kwa £2mill wakati wa Louis Van Gaal sasa huenda ikamnunua kwa kitita cha £25 mill ila kupewa punguzo la 25% ya mauzo kipengele cha mkataba kimeweka wazi hilo

Screenshot_2017-05-17-18-03-40.png
 
Katika usajili wote unaozungumzia ni James Rodriguez una mwelekeo zaidi ila itabidi apunguze matanuzi vinginevyo atajikuta akiuzwa tena.

Screenshot_2017-05-17-17-56-00.png
 
Back
Top Bottom