Manchester United (Red Devils) | Special Thread

mi nilipoona tu bailly kala umeme, nikatafuta njia ya kuondokea, nikakaa kama dakika 20 hivi ndio nikaingia live score, dah huu mfumo aliotuletea mourinho sio kabisa aisee
 
Well said,lakini nadhani na aina ya wachezaji tulionao, Herera na Mhikhtryan wanajitahidi sana sana kutaka timu ipande na icheze mpira wa kasi lakini Pogba,Fellain wanapoza na hawapendi soka la kasi,nadhani jana timu imetemebea km chache sana,tunakosa mawinga aina ya CR7 na Gigs,Di Maria or Ashely young,kwa kifupi timu ina upungufu wa Wingers na namba 9,ukiangalia Zile cross tatu kipindi cha kwanza tungekuwa na stickers anayesimama langoni kama Van Nestoroy yale ni magoli kwa kupress tu.

Sababu nyingine ni aina ya Soka la Mou,kupenda kuzuia na kuruhusu kushambuliwa huku tukiwa hatuna mabeki wa nguvu wa kukabili mashambulizi,Mou anapenda mpira wa kupooza sana,Mbaya Zaidi ajax wanacheza kwa kushambulia Mwanzo mwisho (total football)fainal itatusumbua sana.
 
Tutahitaji sana bahati ili tuweze kushinda kwa ajax
 
Edwin Van De Sar ndio CEO wa sasa wa Ajax na Golikipa wa Zamani wa Manchester United, je siku ya fainal atakuwa anashabikia upande upi?
 
Akileta ndoo atasamehewa vinginevyo kiti moto atawekwa

Jose anatuangusha sana na huu utamaduni wake wa kuzuia sana kuliko kushambulia unatuweka roho juu mashabiki wa Man.Ukitazama takwimu upande wa EPL tulikuwa na wakati mgumu sana wakati tunacheza na top six ugenini yaani hadi unashangaa kwanini tunajilinda tusifungwe badala ya kutafuta magoli.

Mechi yetu na Arsenal imenifanya nisilipe tena Dstv tumefungwa,tumeshambuliwa halafu Jose anacheka huu ni upuuzi wa hali ya juu sana.Tazama aina ya wachezaji tuliokuwa nao Mik,Mata unashangaa wamefeuzwa walinzi wa pembeni huu ni uhani hasa tukizingatia utamaduni wetu wa kushambulia.Mechi ya jana dk sita za mwisho nilihamia chenel nyingine jinsi Celta walivyoachiwa kutushambulia ungezani labda tunacheza pungufu.

Ukweli mchungu pamoja na rekodi nzuri za Jose asipiobdilika msimu ujao hakika OldTraford viti vitabaki wazi.Aina ya mbinu zake alizokujanano huko alikokimbizwa hazitufahi hata kiduchu.
 
Ngongo uko sawa lakini mpira wa ulaya umebadilika sana,timu zinazocheza huo mpira unaosema siku hizi zinapata taabu sana na hazifanikiwi.Angalia Juventus,Real Madrid,Chelsea aina ya soka wanalocheza utagundua defence ni priority kwanza na defender ndio wanakuwa key players timu inaposhambulia

Marcelo +Carvajal +Casemiro ndio key players kwenye ushindi wa mechi nyingi pale Madrid,Barcelona walikuwa na Alba +Alves nafikiri unaona wanavyopata taabu msimu huu baada ya Alves kuondoka na umeona mchango akiwa Juventus.

Angalia Chelsea Conte anawaanzisha bench Cesc na Willian ingawa ndio best attacking midfielders alionao lakini defensive hawako vizuri

Kama umegundua hata Wenger amebadilisha mfumo wake baada ya ule wa kwanza kufeli,Arsenal siku hizi wanafunga magoli ya krosi mengi hawapiti katikati.

Liverpool,Dortmund,PSG,Man City msimu huu wamefanya vibaya sababu kubwa defence zao ni mbovu

Tatizo la United wachezaji wetu wamekuwa wanapoteza nafasi za kufunga kipindi muhimu sana,ukiwa unacheza huo mfumo unapaswa na wachezaji ambao hawafanyi makosa mengi.Hawa Celta Vigo mechi ya kwanza first half tulipaswa kuwafunga goli si chini ya 3 Rashford,Lingard na Mikhitaryan walikosa nafasi za wazi nyingi

Ile droo against Swansea ndio ilimaliza ndoto za top 4 so game ya Arsenal haikuwa na umuhimu hata tungeshinda isingetusaidia kama kushinda game ya Celta
 
Ukweli mtupu
Yaani roho zinatudunda kama vyura!!!!
 
Uchambuzi murua kabisa
Tatizo letu kubwa lililotucost msimu huu ni ubutu wa kutupia magoli/kuua mechi kutokana na kutokuwa na washambuliaji wenye njaa/uiwango
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…