Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ukiulizwa maswali jitahidi kuyajibu,

1.Tutajie striker namba moja wa United na England tangu Ferguson amestaafu ?
2.Unafikiri kwa nini makocha wa England/United waliamua kumchezesha Rooney kama kiungo badala ya striker?
Hilo lote ni swali moja tu, ni kwasababu timu zilikua na washamuliaji wengi na upungufu wa viungo, kwa kuwa rooney ni kiraka waliamua kumpanga yeye kama kiungo, kwa sasa viungo wapo wengi utd ila washambuliaji hakuna, sioni sababu ya kumieka benchi captain kwa kulichezesha lile zee
 
Mimi Si Mshabiki Wa Man U lakini to be honest Ziwezi Kumueka Benchi Ibra nikamchezesha Rooney Hata Siku Moja!
Ubovu wa Chui si Uzima Wa Paka! Na Uzee wa Ibra si Uzima Wa Rooney
Word,, Ibra ni bora ingawa Rooney pia alikuwa bora sana
 
Utamlinganishaje wakati kwa muda mwingi rooney kachezeshwa kama kiungo? Hakua mshambuliaji wa mwisho, alitumika kama daraja la kuwalisha washambuliaji, au hamna kumbukumbu? Laiti kama angechezeshwa kama mshambuliaji wa mwisho, hiyo rikodi ya mabao 250 angekwishaiweka miaka 3 iliopita
Rooney ni mzuri behind the striker Mkuu, kuna mechi kadha wa kadha kacheza kama main striker anashindwa kutimiza majukumu yake na kujikuta ameshuka 10,
Ibra hata kujiposition tu anajua kama alivyosema mdau mwenzangu tuache kum underrate kwa mechi ya juzi kwasababu hata stats zinaonyesha Ibra ndio striker aliyefanya vizuri tangu SAF aondoke.
 
hata stats zinaonyesha Ibra ndio striker aliyefanya vizuri tangu SAF aondoke.
Pia ndie mchezaji aliye poteza nafasi nyingi Sana za wazi ligi kuu England (17) anaemfuatia kapoteza 8

EDIT: anaemfuatia ni afobe kakosa nafasi 9 (1v1)
 
Kimsingi rooney muda wake umeisha man utd.Alipewa nafasi nyingi tu mwanzoni mwa msimu na Mau lakini haikusaidia.Ni muda wa rashford sasa kuaminiwa na kupewa nafasi.
 
4bad302deb1d454450ea32175cff245a.jpg

5cd0b80eb6682959dd4c45d182f0b65c.jpg
 
Bado naamn Anthony martial ndo mtu anayeweza kuamniwa na kupewa nafas anayocheza ibra na akafanya yale yanayokosekana kwa ibra
 
Back
Top Bottom