Tumemaliza msimu huu nafasi ya tano,maana yake hatutashiriki ECL hii si habari nzuri hata kidogo kwasababu timu inaweza kukosa target nyingi sana.Wachezaji wengi wanapenda kushiriki ECL huo ndio wasi wasi wangu.
Team imeonyesha inaweza kufanya vizuri msimu ujao iwapo itasajili baki wa kati (established) kuumia kwa Jones karibu msimu mzima ilichangia sana kuifanya sehemu ya ulinzi hasa katikati kupwaya kwa muda mrefu.Ningependa tusajili wachezaji wawili wa kiungo (established) kwakuwa Carrick kafikia mwisho wake hasa ukizingatia umri umetembea sana.Sehemu ya mchezaji wa kiungo wa pembeni mwenye speed ni muhimu pia wakatafua mchezaji wa aina hiyo kama watakosekana si vibaya tukamchukua Andros wa Newcastle.Man United inahitaji mshambuliaji wa kati (Proven) mwenye kiwango cha juu,tumekosa ECL kwasababu tumefunga magoli machache sana laiti tungekuwa na magoli mengi yamkini tungemwondoa Man City nafasi ya nne.