Mkuu van gaal naweza kusema kinacho mbeba kwa sasa ni historia na sio uwezo, Huyu mzee kila kila sehemu anapoenda lazima atokee mchezaji ambae atazinguana nae, lakini kwetu imekua too much, jaribu kuangalia kuanzia RvP, Rafael, cleverly (juzi kafunguka), chicharito, wote jinsi wanapoondoka lazima wafunguke kwamba tatzo ni van gaal, kagombana na rojo, valdes, pia kuna tetesi kwamba Herrera nae hana furaha pale ot, hyo ni kwa upande wa wachezaji,
fergie kagombana na Keane,van nistelrooy, beckham etc.
LVG kaletwa man u ili atoe watu waliochoka na kueka damu mpya kuitengeneza timu mpya na ukiangalia sasa hivi duniani sidhani kama kuna timu ina potential kama man u. nakumbuka man u na barcelona kipindi cha pilli ilikuwa ni show off kati ya watoto wa barca na man u na kina januzaj/wilson/lingard/perreira waliwakamata watoto wa barcelona na kuwafanya wawe average kabisa. ongeza watoto wengine kama depay, martial, shaw, mc nair etc. hio ndio kazi ya van gaal kueka foundation ili kocha mwengine wa kudumu akija akute kikosi kizuri.
Msimu uliopita tuliingia top four sababu livapuli nae hakuwa vizuri ( kumbuka mwishoni tulivopoteza point ilikua ni rahisi sana liva Ku take advantage)
kiwango cha round ya pili kilikuwa ni kikubwa usiseme hayo tu kumbuka tulitoa dozi mfululizo kwa timu kubwa tulianza na spurs 3-0 tukaja liver nae akala 2 akaja city nae akala 4 yote kafanya LVG haya na 4-1-4-1, tulianza kupoteza baada ya kuwa tushafuzu UEFA sababu tulivyompiga liver na man city tayari ilikuwa imposible liver kutukamata tulimuacha point kama 7
Makosa mengine niliyo yaona kwa van gaal toka amefika
1: kukomaa na mfumo wa 3-5-2 msimu uliopita wakati ilikua wazi hauna matunda kwa ligi ya England, ikapelekea kupoteza point nyingi mwanzoni mwa msimu, hadi kupigwa tano na Leicester wakati tulikua tunaongoza tatu moja.
una uhakika mechi na leicester tulitumia 3-5-2? mechi naikumbuka kabisa tulitumia 4-4-2 (4-1-2-1-2) aka diamond na ushahidi huu hapa
Starting Lineups - Leicester vs Man Utd | 21 Sep 2014
baada ya kufungwa ndio tukashift kwenda 3-5-2 tukacheza mechi 11 unbeaten tukiwapiga liver na arsenal humo ndani, japo ilikuwa na droo nyingi ila 3-5-2 ndio iliotumika hizo mechi 11
2: kumtumia sana Rooney kama mid na namba kumi ( hasa kwa msimu uliopita)
3: kutuaminisha kwamba Rooney anaweza kufunga goli 20+ kwa msimu huu wakati ye mwenyewe alimuaharibu msimu uliopita.
nakubaliana na wewe sina cha kusema
4: kuna baadhi ya mechi alimchezesha di maria kama striker
di maria toka mwanzo haipendi man u, huyu jamaa alikuja kwetu sababu ya FFP psg walikuwa hawawez mnunua hivyo akawa hana ujanja. sipendi kumuongelea sana ila mashabiki wengi wa man u wanamuita snake maria
5: kumuuza RvP, chicha na Wilson kumpeleka kwa mkopo huku akituachia Rooney na martial kama striker pekee tulionao
6: kutosajili winga ya kulia, CB, richa ya kwamba alipewa fungu la kutosha
chicha na rvp walifeli mfumo wa lvg wote tuliona mi kuondoka kwao naona sawa tu ila tulitakiwa tusajili na i hope january atasajili striker. kuhusu beki sidhani kama kuna beki anapatikana kirahisi na wanaopatikana viwango vyao ni vya kawaida.
angalia mangala na otamendi wale wote tuliambiwa tuwasajili na lvg akaachana nao na ukiangalia yupo sahihi wao ndio uchochoro asipokuwepo kompany na huwezi mlimgamisha mangala u otamendi na smalling. hivyo sometime kusajili tu sio solution ya matatizo. kama tunasajili beki basi awe beki kiongozi mtu kama Ramos au godin na sio bora kusajili tu.
7: kumchezesha Bastian na carrick mechi na arsenal huku akiwaacha Herrera na Morgan nje.
nakubaliana na wewe mechi zote 3 ya psg, arsenal na wolfsburg tumefungwa na hawa jamaa wameanza pamoja
8: sub zake ndio zinaniua kabisaaaa, unamtoa mata unamuingiza Powell
powell ni bonge la player japo mechi ya uefa ilikuwa ni kubwa kwake ila inatakiwa jamaa apewe game time, usisahau fergie alimsajili powell kama mrithi wa rooney ni majeruhi tu yamemrudisha nyuma. hope aanze mechi na norwich ili umuone vizuri, one day atakuwa ni star wetu.
9: eti fellain ndio m-badilisha matokeo wetu
msimu uliopita fellaini ndio katuleta uefa na mi natamani turudishe mfumo wetu wa 4-1-4-1 ambao umetengenezwa around fellaini. jamaa ni ngumu kumkaba japo pasi zake ovyo ila akichez atleast kunakuwa na mishe mishe za goli. na akicheza fellaini inamaana young atarudi kuwa winger sababu now hapangwi kutokana na depay/mata/rooney ni vi anduje hivyo cross za young hazina madhara sana.
fellaini ndio mchezaji pekee man u ambao timu pinzani wanafanya mazoezi ya kumkaba
10: possession, possession, possession, possession mwisho wa Siku matokeo ni 0-0
so far tumefanikiwa nyuma beki na katikati papo vizuri, ila ukiangalia mechi kama ya westham tumefanya attempt 21 na goli 0 hivyo sio possesion inayofanya tusifunge bali ni watu hawapo makini mbele na wanapoteza chance kijinga. kwa kifupi hatuna quality mbele tukipata striker mzuri mmoja au wawili tutakuwa tishio sana. just angalia mechi kama vs man city tumewashika kila idara ila hakuna tu anaeweza kumalizia mpira nyavuni. ndio kama lvg anavyosema hatuna suarez au aguero ila tungekuwa nao wangefunga.
hope atamleta hata mario gomez au cavani maana tunahitaji sana forward mpiga vichwa.