Ngoja nikwambie kuhusu United na kwann tunasema tutakupiga?
1. Sisi sio favorite wa kuchukua kombe, so hatuna cha kupoteza. Kwanza tulianza league kama underdogs mkisema united ataishia nafasi ya saba kama kawaida yetu. Management ya united ikamwambia Van Gaal kuwa ili tusipoteze 30% ya deal ya addidas basi mwaka huu tuingie top 4 kwanza. Na hili ndo lengo letu toka mwanzo.
2. Mechi yenyewe: nyie mtakuja na tension na panic kwenye hii mechi ambayo mtataka kwa udi na uvumba mshinde, so hakutakuwa na umakini hapo ninaona watu wa kucheza kwa kupanic wakati sisi tunakuja kucheza mpira, tutatulia tuchukue ushindi.
3. Nafasi ya kuchukua kombe: sisi tuna 30% ya kuchukua kombe endapo tukashinda mechi zote. Huku tukitegemea wa juu wapoteze na kudraw mechi nyingi sana. Arsenal ana nafasi ya 50% na Chelsea ana 70% percent. Mechi ya sisi na nyie ndo itapunguza au kuongeza nafasi yenu ya kuchukua ubingwa. Kwahyo mjipange sana.
4. Nafasi ya wachezaji, mna wachezaji sana ambao ni very average, na wachache ni wale world class. Benchi lenu lipp very narrow for choices wakati sisi tumejaza wachezaji lukuki ambao ukawachukua na wakafanya kitu uwanjani.
Ntuzu usijiamini sana kwanza kushinda mechi yetu na kuchukua ubingwa. Sasa hivi race imekuwa too tight my bro si kama unavyosema na mbaya zaidi siku hizi kadiri mnavyokwenda mnazidi kuchuja na kuvurunda. Sijui wachezaji wanachoka? Au tatizo ni nini brother!?
Usishangae mwisho wa siku akachukua hata man city au arsenal. Unakumbuka ule mwaka ambao man city walichukua ubingwa dakika ya 93? Kwa bao la aguero? Wakati tulikuwa tumewapita almost points 10 na wakaja kutupita almost points 10 mwisho wa siku wakaja kubalance.