Ukiacha sisi washabiki wa man utd, wewe peke yako ndio ulikuwa unasema tutawafunga hawa Liverpool......wengine wote walijua jana ni kukamilisha ratiba tu mechi walishacheza midomoni mwao!
Mkuu mimi napenda mpira hasa....na mara nyingi hua siangalii tu timu yangu peke hua nafatilia na timu zingie kuweza kuona ni namna gani zinacheza na uimara wao uko wapi na je kiwango chao kinapanda na wanapata kujiamini kutokana na matokeo yao au vp....haya ni baadhi ya mambo ambayo hua naangalia sn mkuu.....Sasa ukija kwa timu yenu, hapa ningependa kuzungumzia michezo km miwili ya hivi karibu ambayo timu yenu ilicheza, Ukianzia ule wa Arsenal pamoja na kua mlipoteza ule mchezo mimi naweza kusema kua ni makosa ya uwanjani ambayo ndio yalisababisha hayo matokeo lkn km sio makosa basi mngerudiana na hawa Gunners tena. Pamoja na kupoteza ule mchezo timu iliendelea kuimarika na kucheza vzr tena katika idara zote...kuanzia kipa na mabeki na viungo na ata wafungajia pia ingawa wakati mwingine Van Gaal hua anakosea kupnga kikosi lkn hili nafikirk kwa sasa amekwisha kupata kikosi chake cha kuanza nacho kila mechi.....
Mchezo wenu na Spurs ulikua ni mchezo mzuri sn na ManU walirekebisha makosa yao yote yale waliofanya dhidi ya Arsenal na kuzidi kuimarika ktk kila idara wakati huo kwa LFC mambo hayakua hivo ingawa wao LFC walishinda lkn ushindi wao ulikua wa tabu sn tena walicheza ktk kiwango kibovu sn nakumbuka kabla ya mchezo wenu jana niliwahi kumuuliza
Malafyale juu ya kiwango kibovu siku hiyo majibu aliojibu alisema lazima ManU wafungwe tu...Unajua mkuu Brendan Rodgers amekua anafanya makosa sn mara nyingi hasa anapoona kua ana mchezo mkubwa mbeleni, mara nyingi ata km ana mchezo mmoja kabla ya big game mbele basi timu yake itacheza chini ya kiwango sn huku wakiwa wanaifikiria hio big game, kuna rejea nyingi sn juu ya hili. Na pia huyu BR anapenda sn kuzifunga timu kubwa kitu ambacho anashindwa kuwaandaa wachezaji ktk hizo big game wacheze vzr na matokeo yake wanaambulia kupigwa tu....
Kitu ngine kurudi kwa Carrick kumeifanya ngome ya ManU kua imara sn na sasaivi anavopangwa na Herrera na juu kidogo Fellain basi pale kati panakua pagumu km wakati wa nguli Kean na Schols...nilimwambia jamaa yangu Malafyale kua Carrick atawapoteza watoto wako akaniambia Carrick mzee hana kitu, Anasahau kuishi kwingi ndio kuona/kujua mengi ata mvinyo unapokua na umri mkubwa ndio unazidi kua mtamu zaidi....kwa wale wazee wa bwaah wanajua hili...Lkn kz yake Carrick na Herrera imeonekana jana. Wale sijui kina Coutinho, Hendrson, Allen wooote walichemka....na kwa mara ingine jana ManU walicheza kitimu sn hasa ktk swala la ukabaji nakumbuka mpk Young alikua anashuka kuja kukaba na kumuacha Rooney na Mata tu kule mbele.....kwa kifupi mliwatawala sn hawa jamaa tangu mpira kuanza mpk kuisha....mlicheza vzr tena kwa kujiamini sn....na pia Blind naona yuko vzr sn pamoja na Valencia ila shida bado iko kwa beki za kati zina makosa kidogo na bado hawajajua nani awe mtokaji na nani abaki....
Na pia kocha wenu ana nidhamu sn anapokutana na timu kubwa approach yake mara nyingi ktk hizi timu kubwa anapokutana nazo amekua anafanya vzr sn ata km anapoteza hua ni makosa madogo tu, ni tofauti na kocha wa LFC yeye ana papara...hii inaisaidia sn ManU
Ni hayo tu kwa uchache yalinifanya nione kua hawa LFC mtawapiga tu.