Kwa mnaongalia kupitia BBC, M'kiti wa FA kakwepa kujibu swali juu ya kudorora kwa mashindano ya FA Cup.
Mtangazaji kamwuliza ni kwanini FA isibadilishe utaratibu wa mashindano kwa kuondoa replays? Maana replays kwa mtazamo wa wadau unafanya baadhi ya timu kucheza kwa nia ya kupata replay. Hivyo, kupelekea baadhi ya mechi hata kushindwa kuvutia mashabiki na kwa namna fulani kupunguza mapato.
Ila nakubaliana na wadau, nafikiri kuanzia msimu ujao, kusiwe na replays ili timu zikiingia uwanjani zijue kwamba mshindi lazima apatikane.