Luis van gaal a.k.a master plan kama tupendavyo wengi kumwita hivyo kutokana na kufanikiwa kwa plan zake katika mechi ya mexico kufanya mabadiliko na kupata ushindi wa goli mbili baada ya kusawazisha,,mbali na hapo pia alifanya supersub baada ya kumtoa kumuingiza golikipa ambaye alidaka penalt mbili na kupelekea ushindi uliowapeleka nusu fainali ambapo inaonekana mashabiki wengi wa Manchester united kupata afuheni kwa kudhani kwamba ule mzimu ulioikumba timu katika msimu uliopita hautokuwepo tena na itabaki stori..
Lakini kuna mambo ya msingi kabisa nadhani hayakuzingatiwa na hofu yangu kwamba yanaweza kutokea yale yaliyojitokeza msimu uliopita kwa sababu zifuatazao-:
1)Kocha sio ndo atakayeingia uwanjani kucheza bali benchi na ufundi alionao kuweza kuliorganize vizuri ikiwemo maelewano mazuri na wachezaji vikapatana ndo hupelekea mafanikio.
2)Kikosi cha uholanzi kina wachezaji wazuri waliosheheni uzoefu na waliokaa kwa muda mrefu pamoja na morale waliyokuanayo baada ya mechi yakwanza kumfunga bingwa mtetezi kwa kipigo cha aibu kimewapelekea hamasa kubwa ya kujiona wanaweza hivyo organization yake imekua ni rahisi sana
3)Tukija kwenye uwezo binafsi wa wachezaji,,Manchester imebaki na wachezaji ambao ili kocha yoyote aweze kufanikiwa ni lazima wafungashe safari kwani uwezo walionao na mafanikio ya timu ni vitu ambavyo havimatch..mfano Ashley young,tom clavery,Chriss smalling,moroune fellain,lous nani,michael carrick etc pasi na Ferdinand na nemanja ambao walijiona tayari hawapo katika mfumo wa ushindani kutokana na umri wao.
4)Uongozi mzima wa klabu unaonekana kuyumba sana katika kipindi cha karibuni baada ya sir Alex kustahafu nadhani wale wazoefu kuanzia benchi la ufundi mpaka management wengi walijiuzuru na kutafuta shughuli nyingine na kuondokewa kwa bosi baadae(kufariki)nadhani kutakua na impact kubwa katika uongozi kwenye maamuzi.
5)Anakuja ligi ambayo inaushindani mkubwa sana na anasafari ndefu kwani mechi saba za kombe la dunia mpaka unaingia fainali haziwezi kufananisha premier league,fa cup ingawa uefa na Europa league nadhani hawatakuepo lakini kiwastani anatakiwa kucheza mechi nyingi tofauti...
Nini nataka kusema kwamba tusije tukaexpect too high kwa mafanikio ambayo kocha ameyapata mpaka sasa kupitia timu ya taifa na baadae inaweza kua tofauti sana kwani ni mazingira mawili tofauti tukaja kushikana mashati kutokana na sababu chache ambazo mie binafsi nimeziona na kuzielezea hapo juu ingawa tunategemea atafanya vizuri kwa imani hiyo...
#Man u forever#