Manabii wauza Mafuta ya upako hili neno hamlijui?

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
991
1,000
Mathayo 10:8 inasema,
,"Pozeni wagonjwa,fufueni wafu,takaseni wenye ukoma,toeni pepo,mmepata BURE,toeni BURE".

Hivi kama kweli maono yenu ya unabii na utume mlipewa na Mungu, je mlimlipa Mungu Sh. ngapi? Ni dhahiri mlipewa bure kabisa, sasa kwanini nyie mnawauzia hao aliowatuma kuwaponya na kuwaokoa? Ni wazi kuwa huyu Mungu wa Mathayo 10:8 sio aliewatuma. Km angekua yeye ndo kawatuma mngelitii neno lake.

Huku Iringa Nabii Boaz anauza keki ya upako. Mwamposa anauza mafuta ya upako, Nabii Suguye anauza Stika za picha yake, n.k Nawaambia hata kama mnalitaja neno la Mungu namna gani,hata km mnafungisha watu ndoa,hata km mnaombea na kuponya watu kwa nguvu zenu, siku ya mwisho mtachomwa moto kwa kuenenda kinyume na maagizo yake. Mathayo 10:8 itawahukumu. Endeleeni kujifanya wajanja Mungu anawaona!!Sent using Jamii Forums mobile app
 

The Spit

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
451
250
Wajinga ndio waliwao. Yeyote anayejiita Nabii sijuhi mtume sijuhi nini ni tapeli tu.
Tatizo ujinga umejaza watu. Watu hawajitambui kabisa.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,433
2,000
Mathayo 10:8 inasema,
,"Pozeni wagonjwa,fufueni wafu,takaseni wenye ukoma,toeni pepo,mmepata BURE,toeni BURE".
YESU hajawahi toza ada kuwafunza mitume huduma
inakuwaje makanisa mnatoza pesa kuwafunza watu kuwa wainjilisti,wachungaji na mapadri kwenye seminary,shule za Biblia na vyuo vya theolojia? huko si kuuza uijilisti,uchungaji na upadri?
UINJILISTI ,UPADRI NA UCHUNGAJI UNAUZWA DUKA LA SEMINARI,VYUO VYA BIBLIA NA VYUO VYA THEOLOJIA VYA MAKANISA

Muuza mafuta na maji ya upako na muuza uinjilisti,uchungaji na upadri nani zaidi?
Watumishi wengi wapingaji kuuza humu wao wenyewe huduma walizonazo walinunua kwa kulipa ada kuwa wainjilisti,wachungaji au mapadri ,

Mafarisayo wakubwa nyie.Yesu wapi aliuza au ku chaji ada kuwafunza?

Hilo andiko hamlioni au hamlijui?

Hata mitume wapi wali chaji ada? Kweli nyani haoni kundule
 

Laptop001

JF-Expert Member
Jan 18, 2020
205
250
Eneo hilo hawasomi na kama wanasoma wanajifanya hawaelewi.na waumini kinawaponza kutaka utajiri wa haraka,kutosoma biblia na kutafakari.
 

Zabron Hamis

Verified Member
Dec 19, 2016
3,381
2,000
YEHODAYA,
Tumia akili kidogo tu kama punje ya haradali. Ukienda kusoma bure hapo chuoni, anayekufundisha awe ombaomba? Majengo yatajengwa bure, au unataka wasomee chini ya mienmbe? MANABII WA SASA NI MATAPELI WA KIWANGO CHA LAMI, HAWAFAI HATA KUWA VIONGOZI WA FAMILIA.
 

nitonye

JF-Expert Member
Dec 18, 2011
7,274
2,000
Biblia inasema tutawaona kwa matendo yao lakini pia inatuambia tusihukumu kwa maana hatujui siri ya mioyo yao ili na sisi tusije tukahukumiwa. Kwa maana siku ya mwisho atavuna ngano na yale magugu yaliyopandwa na shetani yatatupwa kwenye tanuru la moto uwakao

Sent using Jamii Forums mobile app
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,433
2,000
Tumia akili kidogo tu kama punje ya haradali. Ukienda kusoma bure hapo chuoni, anayekufundisha awe ombaomba? Majengo yatajengwa bure, au unataka wasomee chini ya miembe?.
Yale yale.Kwa hiyo hizo huduma zingine hazina gharama?

kwa hiyo mnauza uinjilisti.uchungaji na upadri ili mpige pesa za kumlipa mfundishaji na mjenge majengo? MUMEGEUZA ajira .NI NJIA YA KUKUSANYA PESA PIA?
 

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
991
1,000
Mungu alipokua anagiza alijua tv zipo na kumbi zipo. Lakini pia hakusema ni lazma kuhubiri kupitia redio na Tv. Mungu angeruhusu visingizio hakuna mtu ambae angetenda zambi kwani hata changudoa anasababu ya kujitetea.
Na Mwamposya gharama za kukodi kumbi na viwanja na miundo mbinu unataka alipe nani ikiwemo Gharama za TV na radio?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,433
2,000
Mungu alipokua anagiza alijua tv zipo na kumbi zipo. Lakini pia hakusema ni lazma kuhubiri kupitia redio na Tv. Mungu angeruhusu visingizio hakuna mtu ambae angetenda zambi kwani hata changudoa anasababu ya kujitetea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwamposya mwache kwanza karibu upokee baraka kwa padri huyu mzungu
 

Rwankomezi

JF-Expert Member
Sep 5, 2013
2,041
2,000
Mwamposya mwache kwanza karibu upokee baraka kwa padri huyu mzungu

Hivi huyu mzungu kama sio ushirikina wa kuwachapa wenzie fimbo,Namanisha yeye kajiamlia tu kama njia ya utaratibu wake kanisani kwake,anajisikiaje pale anapokaa zake home na kuaitazama hii video na kuwaona anaowachapa Bakora watu weusiiii?
 

Kikwajuni One

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
9,679
2,000
Umenena kweli
Mathayo 10:8 inasema,
,"Pozeni wagonjwa,fufueni wafu,takaseni wenye ukoma,toeni pepo,mmepata BURE,toeni BURE".

Hv km kweli maono yenu ya unabii na utume mlipewa na Mungu,je mlimlipa Mungu Sh. ngapi? Ni dhahiri mlipewa bure kabisa, sasa kwanini nyie mnawauzia hao aliowatuma kuwaponya na kuwaokoa? Ni wazi kuwa huyu Mungu wa Mathayo 10:8 sio aliewatuma. Km angekua yeye ndo kawatuma mngelitii neno lake.

Huku Iringa Nabii Boaz anauza keki ya upako,Mwamposa anauza mafuta ya upako, Nabii Suguye anauza Stika za picha yake, n.k Nawaambia hata km mnalitaja neno la Mungu namna gani,hata km mnafungisha watu ndoa,hata km mnaombea na kuponya watu kwa nguvu zenu, siku ya mwisho mtachomwa moto kwa kuenenda kinyume na maagizo yake. Mathayo 10:8 itawahukumu. Endeleeni kujifanya wajanja Mungu anawaona!!Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mcqueenen

JF-Expert Member
Nov 2, 2019
1,309
2,000
Tatizo hao manabii hawajapewa bure unakuta na wao walinunua kwa gharama uko Nigeria
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom