Manabii wauza Mafuta ya upako hili neno hamlijui?

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
1,865
3,798
Mathayo 10:8 inasema,
,"Pozeni wagonjwa,fufueni wafu,takaseni wenye ukoma,toeni pepo,mmepata BURE,toeni BURE".

Hivi kama kweli maono yenu ya unabii na utume mlipewa na Mungu, je mlimlipa Mungu Sh. ngapi? Ni dhahiri mlipewa bure kabisa, sasa kwanini nyie mnawauzia hao aliowatuma kuwaponya na kuwaokoa? Ni wazi kuwa huyu Mungu wa Mathayo 10:8 sio aliewatuma. Km angekua yeye ndo kawatuma mngelitii neno lake.

Huku Iringa Nabii Boaz anauza keki ya upako. Mwamposa anauza mafuta ya upako, Nabii Suguye anauza Stika za picha yake, n.k Nawaambia hata kama mnalitaja neno la Mungu namna gani,hata km mnafungisha watu ndoa,hata km mnaombea na kuponya watu kwa nguvu zenu, siku ya mwisho mtachomwa moto kwa kuenenda kinyume na maagizo yake. Mathayo 10:8 itawahukumu. Endeleeni kujifanya wajanja Mungu anawaona!!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wajinga ndio waliwao. Yeyote anayejiita Nabii sijuhi mtume sijuhi nini ni tapeli tu.
Tatizo ujinga umejaza watu. Watu hawajitambui kabisa.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mathayo 10:8 inasema,
,"Pozeni wagonjwa,fufueni wafu,takaseni wenye ukoma,toeni pepo,mmepata BURE,toeni BURE".
YESU hajawahi toza ada kuwafunza mitume huduma
inakuwaje makanisa mnatoza pesa kuwafunza watu kuwa wainjilisti,wachungaji na mapadri kwenye seminary,shule za Biblia na vyuo vya theolojia? huko si kuuza uijilisti,uchungaji na upadri?
UINJILISTI ,UPADRI NA UCHUNGAJI UNAUZWA DUKA LA SEMINARI,VYUO VYA BIBLIA NA VYUO VYA THEOLOJIA VYA MAKANISA

Muuza mafuta na maji ya upako na muuza uinjilisti,uchungaji na upadri nani zaidi?
Watumishi wengi wapingaji kuuza humu wao wenyewe huduma walizonazo walinunua kwa kulipa ada kuwa wainjilisti,wachungaji au mapadri ,

Mafarisayo wakubwa nyie.Yesu wapi aliuza au ku chaji ada kuwafunza?

Hilo andiko hamlioni au hamlijui?

Hata mitume wapi wali chaji ada? Kweli nyani haoni kundule
 
Eneo hilo hawasomi na kama wanasoma wanajifanya hawaelewi.na waumini kinawaponza kutaka utajiri wa haraka,kutosoma biblia na kutafakari.
 
YEHODAYA,
Tumia akili kidogo tu kama punje ya haradali. Ukienda kusoma bure hapo chuoni, anayekufundisha awe ombaomba? Majengo yatajengwa bure, au unataka wasomee chini ya mienmbe? MANABII WA SASA NI MATAPELI WA KIWANGO CHA LAMI, HAWAFAI HATA KUWA VIONGOZI WA FAMILIA.
 
Biblia inasema tutawaona kwa matendo yao lakini pia inatuambia tusihukumu kwa maana hatujui siri ya mioyo yao ili na sisi tusije tukahukumiwa. Kwa maana siku ya mwisho atavuna ngano na yale magugu yaliyopandwa na shetani yatatupwa kwenye tanuru la moto uwakao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumia akili kidogo tu kama punje ya haradali. Ukienda kusoma bure hapo chuoni, anayekufundisha awe ombaomba? Majengo yatajengwa bure, au unataka wasomee chini ya miembe?.
Yale yale.Kwa hiyo hizo huduma zingine hazina gharama?

kwa hiyo mnauza uinjilisti.uchungaji na upadri ili mpige pesa za kumlipa mfundishaji na mjenge majengo? MUMEGEUZA ajira .NI NJIA YA KUKUSANYA PESA PIA?
 
Mungu alipokua anagiza alijua tv zipo na kumbi zipo. Lakini pia hakusema ni lazma kuhubiri kupitia redio na Tv. Mungu angeruhusu visingizio hakuna mtu ambae angetenda zambi kwani hata changudoa anasababu ya kujitetea.
Na Mwamposya gharama za kukodi kumbi na viwanja na miundo mbinu unataka alipe nani ikiwemo Gharama za TV na radio?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu alipokua anagiza alijua tv zipo na kumbi zipo. Lakini pia hakusema ni lazma kuhubiri kupitia redio na Tv. Mungu angeruhusu visingizio hakuna mtu ambae angetenda zambi kwani hata changudoa anasababu ya kujitetea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwamposya mwache kwanza karibu upokee baraka kwa padri huyu mzungu
 
Mwamposya mwache kwanza karibu upokee baraka kwa padri huyu mzungu


Hivi huyu mzungu kama sio ushirikina wa kuwachapa wenzie fimbo,Namanisha yeye kajiamlia tu kama njia ya utaratibu wake kanisani kwake,anajisikiaje pale anapokaa zake home na kuaitazama hii video na kuwaona anaowachapa Bakora watu weusiiii?
 
Umenena kweli
Mathayo 10:8 inasema,
,"Pozeni wagonjwa,fufueni wafu,takaseni wenye ukoma,toeni pepo,mmepata BURE,toeni BURE".

Hv km kweli maono yenu ya unabii na utume mlipewa na Mungu,je mlimlipa Mungu Sh. ngapi? Ni dhahiri mlipewa bure kabisa, sasa kwanini nyie mnawauzia hao aliowatuma kuwaponya na kuwaokoa? Ni wazi kuwa huyu Mungu wa Mathayo 10:8 sio aliewatuma. Km angekua yeye ndo kawatuma mngelitii neno lake.

Huku Iringa Nabii Boaz anauza keki ya upako,Mwamposa anauza mafuta ya upako, Nabii Suguye anauza Stika za picha yake, n.k Nawaambia hata km mnalitaja neno la Mungu namna gani,hata km mnafungisha watu ndoa,hata km mnaombea na kuponya watu kwa nguvu zenu, siku ya mwisho mtachomwa moto kwa kuenenda kinyume na maagizo yake. Mathayo 10:8 itawahukumu. Endeleeni kujifanya wajanja Mungu anawaona!!



Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo hao manabii hawajapewa bure unakuta na wao walinunua kwa gharama uko Nigeria
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom