Biashara ya upako: Utapeli unaoenea kwa kasi ya ajabu

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,693
Imeandikwa sehemu gani kwamba vitu vya ufunuo viuzwe?

Ninachofahamu mimi ni kuwa mafuta yalitumiwa na manabii na makuhani kwa ajili ya kazi maalum tu; haikuwa kuyauza wala kuyatangaza kama biashara, hapo ni kinyume kabisa na maandiko.

Sasa watumishi wa leo wamegeuza hiyo huduma ni biashara kitu ambacho si sahihi kabisa. Na mkumbuke kitu cha ufunuo kinatumika kwa muda maalum na kwa wakati maalum, na siyo kwa kila mtu, na si kila mahali. Angalia Yesu alipomwambia yule kipofu apake matope kwenye macho, hakufanya hivyo kwa kila kipofu, wengine aliwashika macho tu, wengine alitamka tu wakapona.

Tusemeje kwa Nabii Elisha kila mwenye ukoma angemwambia aende Yordan akajichovye mara 7, maana hata hivyo, kulikuwa na wakoma wengi katika Israeli zama hizo wala hapana aliyetakaswa ila Naamani, mtu wa Shamu pekee. [Luka 4:27].” Na wala Elisha hakuchukua malipo ya pesa, na mtumwa wake aliyemzunguka Elisha na kuchukua hizo pesa, alipatwa na ukoma.

Basi tungetegemea manabii watumie hiyo kanuni ya kuchovya watu kwenye maji wapone ukoma, lakini hilo hatulioni zaidi ya kuona mafunuo mengine ya uponyaji.

Lakini kinachoshangaza watumishi wa leo wamegeuza hivyo vitu vya kimafunuo kama biashara, na mbaya zaidi wanauza, Mungu akikupa kitu kwa mafunuo ukitumie kumponya mtu huwezi kukiuza, na huwezi kulinganisha eti mbona Biblia inauzwa, biblia ni kitabu kimepitia hatua nyingi sana mpaka kuandikwa, na wamishionari walioleta injili Afrika enzi hizo walikuwa wanagawa bure, hata leo maeneo ambayo injili haijawafikia watu Biblia inagawiwa bure mfano huko Korea Kaskazini na China na sehemu mbalimbali za dunia. Hata mimi mda mwingine nagawa Biblia bure sehemu zile ambazo Injili haijafika na kwa baadhi ya watu wasio na uwezo wa kununua na wengine nawapa kama zawadi. Mtume Paulo anasema hivi:

“Basi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nihubiripo, nitaitoa Injili bila GHARAMA, bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili. [1 Wakorintho 9:18].”

NITAITOA INJILI BILA GHARAMA: Huu msingi Mtume Paulo alipokea kutoka kwa Bwana, kuwa, “Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; MMEPATA BURE, TOENI BURE. [Mathayo 10:8].”

Hivyo wanajitetea ya kwamba, sasa bila kufanya hivyo hatutaweza kulipa umeme, kununua vyombo, kulipia kumbi na mavitu mengi. Rafiki kwani Luku/stima mnalipia bei gani? Maana tunaona ibada ya wazi mnafanya Jumapili tu tena kwenye uwanja wa wazi, na hivyo vyombo vya muziki mnavinunua kila siku?

Kwahiyo mnauza mafuta, maji, chumvi kwa vigezo hivyo? Kama ndicho kigezo nawaambia iliyo kweli acheni uongo, semeni tu mnapiga dili la upako. Kwani hamna matolea na sadaka, mbona waumini wanatoa sadaka na zaka! Au hazitoshi mpaka uanze kuuza na chumvi na mafuta? Halafu ni wewe tu ndio unapokea, na kudai ni huduma yako isiyo na kamati ya fedha, isiyohojiwa. Wenzenu wa zama za Yesu walikuwa wanauza njiwa za upako hekaluni, walifukuzwa na Yesu na meza zao kupinduliwa na kukemewa kwamba, “Je! Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi. [Marko 11:17].”

Hukumu ya Mungu itakuwa juu yenu enyi wapotoshaji. Imeandikwa kwamba, “Na ye yote atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake, na kutupwa baharini. [Marko 9:42].”

Mungu akufumbue macho utambue upo wakati gani na nini sasa unachopaswa kufanya kwa habari ya wokovu wako.

View attachment 1304985
FB_IMG_1577460242775.jpeg
 
Kwa Wakatoliki ni imani yako tu, nunua mafuta nenda nayo kanisani. Wakati wa mageuzo ukiyaombea mafuta ule uwezo unao geuza mkate kuwa mwili utayagusa mafuta yako.

Kumbuka kutoa zaka ya kanisa
Kwa wajasiriadini hawataki hivo.
 
Aaron Arsenal,
2kings4: 1 to 7

For Swahili audience: Wafalme wa 2 sura ya 4 mstari wa Kwanza Hadi wa Saba.
VIPI NDUGU , ELISHA ALIFANYA BIASHARA HAPA?

2 Wafalme 4

1 Basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha, akasema, Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha Bwana; na aliyemwia amekuja ili ajitwalie wana wangu wawili kuwa watumwa.

2 Elisha akamwambia, Nikufanyie nini? Niambie; una kitu gani nyumbani? Akasema, Mimi mjakazi wako sina kitu nyumbani, ila chupa ya mafuta.

3 Akasema, Nenda, ukatake vyombo huko nje kwa jirani zako wote, vyombo vitupu; wala usitake vichache.

4 Kisha uingie ndani, ukajifungie mlango wewe na wanao, ukavimiminie mafuta vyombo vile vyote; navyo vilivyojaa ukavitenge.

5 Basi akamwacha, akajifungia mlango yeye na wanawe; hao wakamletea vile vyombo, na yeye akamimina.

6 Ikawa, vilipokwisha kujaa vile vyombo, akamwambia mwanawe, Niletee tena chombo. Akamwambia, Hakuna tena chombo. Mafuta yakakoma.

7 Ndipo akaja akamwambia yule mtu wa Mungu. Naye akasema, Enenda ukayauze mafuta haya, uilipe deni yako; nayo yaliyosalia uyatumie wewe na watoto wako.
 
Imeandikwa sehemu gani kwamba vitu vya ufunuo viuzwe?

Ninachofahamu mimi ni kuwa mafuta yalitumiwa na manabii na makuhani, kwa ajili ya kazi maalum tu, haikuwa kuyauza wala kuyatangaza kama biashara hapo ni kinyume kabisa na maandiko.

Sasa watumishi wa leo wamegeuza hiyo huduma ni biashara kitu ambacho si sahihi kabisa; Na mkumbuke kitu cha ufunuo kinatumika kwa muda maalum na kwa wakati maalum, na siyo kwa kila mtu, na si kila mahali, angalia Yesu alipomwambia yule kipofu apake matope kwenye macho, hakufanya hivyo kwa kila kipofu, wengine aliwashika macho tu, wengine alitamka tu wakapona.

Tusemeje kwa Nabii Elisha kila mwenye ukoma angemwambia aende Yordan akajichovye mara 7, maana hata hivyo, kulikuwa na wakoma wengi katika Israeli zama hizo wala hapana aliyetakaswa ila Naamani, mtu wa Shamu pekee. [Luka 4:27].” Na wala Elisha hakuchukua malipo ya pesa, na mtumwa wake aliyemzunguka Elisha na kuchukua hizo pesa, alipatwa na ukoma. Basi tungetegemea manabii watumie hiyo kanuni ya kuchovya watu kwenye maji wapone ukoma, lakini hilo hatulioni zaidi ya kuona mafunuo mengine ya uponyaji.

Lakini kinachoshangaza watumishi wa leo wamegeuza hivyo vitu vya kimafunuo kama biashara, na mbaya zaidi wanauza, Mungu akikupa kitu kwa mafunuo ukitumie kumponya mtu huwezi kukiuza, na huwezi kulinganisha eti mbona Biblia inauzwa, biblia ni kitabu kimepitia hatua nyingi sana mpaka kuandikwa, na wamishionari walio leta injili Africa enzi hizo walikuwa wanagawa bure, hata leo maeneo ambayo injili haijawafikia watu Biblia inagawiwa bure mfano huko Korea Kaskazini na China na sehemu mbalimbali za dunia. Hata mimi mda mwingine nagawa Biblia bure sehemu zile ambazo Injili haijafika na kwa baadhi ya watu wasio na uwezo wa kununua na wengine nawapa kama zawadi. Mtume Paulo anasema hivi,

“Basi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nihubiripo, nitaitoa Injili bila GHARAMA, bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili. [1 Wakorintho 9:18].”

NITAITOA INJILI BILA GHARAMA: Huu msingi Mtume Paulo alipokea kutoka kwa Bwana, kuwa, “Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; MMEPATA BURE, TOENI BURE. [Mathayo 10:8].”

Hivyo wanajitetea ya kwamba, sasa bila kufanya hivyo hatutaweza kulipa umeme, kununua vyombo, kulipia kumbi na mavitu mengi. Rafiki kwani Luku/stima mnalipia bei gani? Maana tunaona ibada ya wazi mnafanya jumapili tu tena kwenye uwanja wa wazi, na hivyo vyombo vya muziki mnavinunua kila siku?. Kwahiyo mnauza mafuta, maji, chumvi kwa vigezo hivyo? Kama ndicho kigezo nawaambia iliyo kweli acheni uongo, semeni tu mnapiga dili la upako. Kwani hamna matolea na sadaka, mbona waumini wanatoa sadaka na zaka! Au hazitoshi mpaka uanze kuuza na chumvi na mafuta? Halafu ni wewe tu ndio unapokea, na kudai ni huduma yako isiyo na kamati ya fedha, isiyohojiwa. Wenzenu wa zama za Yesu walikuwa wanauza Njiwa za upako hekaluni, Walifukuzwa na Yesu na meza zao kupinduliwa na kukemewa kwamba, “Je! Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi. [Marko 11:17].” Hukumu ya Mungu itakuwa juu yenu enyi wapotoshaji. Imeandikwa kwamba, “Na ye yote atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake, na kutupwa baharini. [Marko 9:42].”

Mungu akufumbue macho utambue upo wakati gani na nini sasa unachopaswa kufanya kwa habari ya wokovu wako.

View attachment 1304985View attachment 1304986
Mkuu, umenena vema. Ni muhimu sana wakristo wakaomba sana kupewa karama ya kuzipambanua roho. Nikueleze tu, nimeshangaa sana pale nilipokuja kufahamu kuwa asilimia kubwa ya manabii na mitume walikuwa waislamu kisha wakaokoka na moja kwq moja wakaja na karama ya miujiza.

Ukiwa mtu wa kusoma neno, utagundua wazi kwamba wachawi wamevamia kqnisa, na sasa kwa sababu tunatafuta miujiza, wameboresha hilo na kuwateka wajinga.

Biashara za vifaa vya upako ni eneo jipya ambalo linakua kwa kasi na kuwaingiza wengi kwenye lindi la umaskini na ujinga wa kupitiliza. Bibloa imesema wazi KAENI NA WAKE ZENU KWA AKILI KWA KUWA NI VIUMBE DHAIFU. Sasa najua wanawake wengi watanichukia kwa kusema andiko hilo, lakini dalili ziko wazi. Wahanga wakubwa wa mafundisho haya yatokayo kuzimu ni wanawake. Kundi hilo limekuwa likisombwa na kila aina ya mafundisho mapya kwa sababu hawana roho ya kupambanua. Wengi wao hupima matokeo kuliko kutazama yamepatikanaje, na hivyo kutekwa na roho zidanganyazo.

Mnisamehe mama zangu, imewapasa kuwatii waume zenu, utii ikiwa ni pamoja na kusikiliza maonyo yao, wakisema huku hapana, msiwasikilize hao wachungaji na manabii ambao wanataka utii kuliko kumtii mume. Hii ni dhambi ya uasi mbele za Mungu kwani hakuna nabii ama mtume katikati yako na mumeo. Hii ni MIND CONTOL na ndio inatumiwa zaidi kuwaweka mateka wale wasiolitii neno.

Kristu akikuweka huru unakuwa huru kweli kweli, lakini haya madhehebu pendwa yanakutoa utumwani mwa waganga yanakuingiza utumwani mwa wachawi.

Kwenu wanaume mnaokwenda kama misukule, mnapoteza sifa muhimu ya kuwa kiongozi wa familia na kusombwa na kila aina ya mafundisho. Mungu amekuweka kuwa mwakilishi wake kwenye familia yako, iweje uwe unayumbishwa hovyo kwa kutamani vya kuonekana? Unatekwa na miujiza? Mwanamke ni VISUAL, hutamani kila akionacho, mwanamume ni mu wa fikra, huchuja kila jambo kuona kama lina manufaa, iweje leo tujiweke kama wanawake? Kwa hiyo Mungu alituumba kuwa wanaume bure? Tunawezaje kulilia uongozi na utii toka kwa wake zetu kama sisi wenyewe vichwa vyetu vinaongozwa kama misukule? Tujitafakari.

Amina

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Enenda
VIPI NDUGU , ELISHA ALIFANYA BIASHARA HAPA?

2 Wafalme 4

1 Basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha, akasema, Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha Bwana; na aliyemwia amekuja ili ajitwalie wana wangu wawili kuwa watumwa.

2 Elisha akamwambia, Nikufanyie nini? Niambie; una kitu gani nyumbani? Akasema, Mimi mjakazi wako sina kitu nyumbani, ila chupa ya mafuta.

3 Akasema, Nenda, ukatake vyombo huko nje kwa jirani zako wote, vyombo vitupu; wala usitake vichache.

4 Kisha uingie ndani, ukajifungie mlango wewe na wanao, ukavimiminie mafuta vyombo vile vyote; navyo vilivyojaa ukavitenge.

5 Basi akamwacha, akajifungia mlango yeye na wanawe; hao wakamletea vile vyombo, na yeye akamimina.

6 Ikawa, vilipokwisha kujaa vile vyombo, akamwambia mwanawe, Niletee tena chombo. Akamwambia, Hakuna tena chombo. Mafuta yakakoma.

7 Ndipo akaja akamwambia yule mtu wa Mungu. Naye akasema, Enenda ukayauze mafuta haya, uilipe deni yako; nayo yaliyosalia uyatumie wewe na watoto wako.
So ukayauze mafuta haya nawe ulipe Deni lako. Mafuta yalikua ya mzeutuni. Yalikuwa na upako kwa sababu aliyaombea na kuyatakasa Kisha akamwambia nenda ukayauze.

Mpira uishie hapa
 
Umeandika nini hapa?huo upako ulitokea wapi kwenye hayo mafuta?maana huyo mama alikuwa anadaiwa,na hana chochote cha kumlipa anayemdai,ndipo nabii Elisha alipomwambia akusanye vyombo vingi awezavyo,akamba kwa Mungu na vile vyombo vikajaa mafuta,akamwambia akayauze ili hela atakayoipata akalipie deni!! Hayo mauchawi yenu ya upako hayahusiani kabisa na mafuta hayo.
Enenda
So ukayauze mafuta haya nawe ulipe Deni lako. Mafuta yalikua ya mzeutuni. Yalikuwa na upako kwa sababu aliyaombea na kuyatakasa Kisha akamwambia nenda ukayauze.

Mpira uishie hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zamani walokole walikuwa wanacheka wakatoliki kuwa huwa wanaabudu sanamu. Ila sasa wao wamekuja kwa ukali zaidi, si kuabudu tu ila na kuuza tena kwa bei mbaya!
Keki za upako,sabuni za upako,vitambaa vya upako,perfume za upako,nk kuna tofauti gani na ibada za sanamu
 
Enenda
So ukayauze mafuta haya nawe ulipe Deni lako. Mafuta yalikua ya mzeutuni. Yalikuwa na upako kwa sababu aliyaombea na kuyatakasa Kisha akamwambia nenda ukayauze.

Mpira uishie hapa

rudi kasome upya..
 
Yaani manabii ni Watu wa ajabu sana na pia hata wanaofuata ni Watu wa ajabu sana

Yani kila siku ni miujiza sijui Leo tunaenda kumuangusha Goliath wako Mara mfilisti wako Mara adui wako

Hata wamesahau kazi ya miujiza miujiza yote ambayo MUNGU aliitenda ni wasio amini ili wapate kuamini ndio maana YESU alisema msipo niamini Mimi basi ziaminini kazi nizifanyazo ili baba atukukuke kupitia mwana

Lakini sasa mijuiza ni sehemu ya kupata waumini wengi walio na DHAMBI na hawataki kiziacha DHAMBI

Kama unataka ujue hawa jamaa ni waongo
Hauna mahali YESU alitabiria Watu magari ,nyumba ,wachumba Bali aliwaambia utafuteni kwanza ufalme wa mbinguni na haki yake na mengine yote mtazidishiwa

Injili yoyote inayohubiriliwa na mtu yoyote kama haingolei wewe kuacha DHAMBI na kuishi maisha matakatifu Hiyo sio injili ya Kristo
 
Naishi karibu na kanisa...ambacho hua nasikia Ni Toka pepo toka pepo...Toka pepo kwa jina la yesu. Ina maaana waumini wengi wa hi dini Wana mapepo. Niswali tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom