Naipinga Biashara ya upako , Ni Utapeli

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,693
Imeandikwa sehemu gani kwamba vitu vya ufunuo viuzwe?

Ninachofahamu mimi ni kuwa mafuta yalitumiwa na manabii na makuhani, kwa ajili ya kazi maalum tu, haikuwa kuyauza wala kuyatangaza kama biashara hapo ni kinyume kabisa na maandiko.

Sasa watumishi wa leo wamegeuza hiyo huduma ni biashara kitu ambacho si sahihi kabisa; Na mkumbuke kitu cha ufunuo kinatumika kwa muda maalum na kwa wakati maalum, na siyo kwa kila mtu, na si kila mahali, angalia Yesu alipomwambia yule kipofu apake matope kwenye macho, hakufanya hivyo kwa kila kipofu, wengine aliwashika macho tu, wengine alitamka tu wakapona.

Tusemeje kwa Nabii Elisha kila mwenye ukoma angemwambia aende Yordan akajichovye mara 7, maana hata hivyo, kulikuwa na wakoma wengi katika Israeli zama hizo wala hapana aliyetakaswa ila Naamani, mtu wa Shamu pekee. [Luka 4:27].” Na wala Elisha hakuchukua malipo ya pesa, na mtumwa wake aliyemzunguka Elisha na kuchukua hizo pesa, alipatwa na ukoma. Basi tungetegemea manabii watumie hiyo kanuni ya kuchovya watu kwenye maji wapone ukoma, lakini hilo hatulioni zaidi ya kuona mafunuo mengine ya uponyaji.

Lakini kinachoshangaza watumishi wa leo wamegeuza hivyo vitu vya kimafunuo kama biashara, na mbaya zaidi wanauza, Mungu akikupa kitu kwa mafunuo ukitumie kumponya mtu huwezi kukiuza, na huwezi kulinganisha eti mbona Biblia inauzwa, biblia ni kitabu kimepitia hatua nyingi sana mpaka kuandikwa, na wamishionari walio leta injili Africa enzi hizo walikuwa wanagawa bure, hata leo maeneo ambayo injili haijawafikia watu Biblia inagawiwa bure mfano huko Korea Kaskazini na China na sehemu mbalimbali za dunia. Hata mimi mda mwingine nagawa Biblia bure sehemu zile ambazo Injili haijafika na kwa baadhi ya watu wasio na uwezo wa kununua na wengine nawapa kama zawadi. Mtume Paulo anasema hivi,

“Basi thawabu yangu ni nini? Ni hii, ya kuwa nihubiripo, nitaitoa Injili bila GHARAMA, bila kutumia kwa utimilifu uwezo wangu nilio nao katika Injili. [1 Wakorintho 9:18].”

NITAITOA INJILI BILA GHARAMA: Huu msingi Mtume Paulo alipokea kutoka kwa Bwana, kuwa, “Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; MMEPATA BURE, TOENI BURE. [Mathayo 10:8].”

Hivyo wanajitetea ya kwamba, sasa bila kufanya hivyo hatutaweza kulipa umeme, kununua vyombo, kulipia kumbi na mavitu mengi. Rafiki kwani Luku/stima mnalipia bei gani? Maana tunaona ibada ya wazi mnafanya jumapili tu tena kwenye uwanja wa wazi, na hivyo vyombo vya muziki mnavinunua kila siku?. Kwahiyo mnauza mafuta, maji, chumvi kwa vigezo hivyo? Kama ndicho kigezo nawaambia iliyo kweli acheni uongo, semeni tu mnapiga dili la upako. Kwani hamna matolea na sadaka, mbona waumini wanatoa sadaka na zaka! Au hazitoshi mpaka uanze kuuza na chumvi na mafuta?

Halafu ni wewe tu ndio unapokea, na kudai ni huduma yako isiyo na kamati ya fedha, isiyohojiwa. Wenzenu wa zama za Yesu walikuwa wanauza Njiwa za upako hekaluni, Walifukuzwa na Yesu na meza zao kupinduliwa na kukemewa kwamba,

“Je! Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi. [Marko 11:17].”

Hukumu ya Mungu itakuwa juu yenu enyi wapotoshaji. Imeandikwa kwamba,

“Na ye yote atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, afadhali afungiwe jiwe la kusagia shingoni mwake, na kutupwa baharini. [Marko 9:42].”

Mungu akufumbue macho utambue upo wakati gani na nini sasa unachopaswa kufanya kwa habari ya wokovu wako.
 
Hiyo ni biashara kama biashara nyingine.

Siku moja nimerudi home nikakuta wife anatazama chanell ya mzee wa kukanyaga mafuta. Nikasema ok , ngoja niangalie hii misa.

Ikafika stage ati watu wanaitwa kupata baraka kwa kuwekewe madaraja ya pesa.

Eti wale wa 50k , mara 40k , mara 30k mwisho kabisa wakapewa baraka wale wa 5k , ninyi wengine wa below 5k mkapambane na hali yenu. Shubhaaamit.

At nanunua baraka 50k , kweli wajinga hawaishi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukimruhusu mkeo aende kwa hao matapeli au kuwaangalia , anaweza kuwa msukule wao

Utakuwa unaacha matumiz 10000 , 5000 anapeleka kwa hawa matapeli
 
Inakuwaje unashindwa kuwakataza watu waache kwenda huko kwa hao manabii.. ni kwa sababu huwezi kuwakataza.. Hakuna manabii bila wafuasi wake.. pambana kujua kwa nini watu hawaachi kwenda huko

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao si kama Waganga wa kienyeji wa kisasa

Wanaoenda huko hurogwa akili zao

Maana wameuamini Uongo ,na kumkataa roho MTAKATIFU ,hivo Mungu huruhusu wapotee maana wameuamini Uongo .

2 wathesalonike 2:11-12

Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo;
ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu."
 
Inakuwaje unashindwa kuwakataza watu waache kwenda huko kwa hao manabii.. ni kwa sababu huwezi kuwakataza.. Hakuna manabii bila wafuasi wake.. pambana kujua kwa nini watu hawaachi kwenda huko

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe utakuwa msambaza maji au mafuta au keki pale kwa mwamposa , na unalipwa kwa hiyo kazi

Lkn usijifanye kipofu watu wanapotapeliwa na hao matapeli

Mbona hamuendi baharini au ziwani mkayawekee upako maji ,kila mtu achote?

Acheni usanii
 
Sijui hao waumini wanarogwa..mm nawaona WAPUMBAVU..yaani wanaibiwa na bado HAWAONI.

PUMBAVU
 
Mwenye nacho anaongezewa, hata kidogo chako utanyang'anywa apewe yeye! Wataishia kwenye upako wa kukanyagana tu, na mayowe juu!
 
Sahihi, hao ni matapeli kwa asilimia kubwa. Wanatakiwa wapigwe life ban na washtakiwe na kufungwa kwa utapeli wao

Back
Top Bottom