hamis77
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,642
- 19,018
Niliambiwa na ndugu mmoja kanisani kwetu aliyetokea Zambia, kwamba nchini kwao waganga wa kienyeji huacha uchawi vijijini na kwenda kuwa wachungaji wa makanisa katika miji na majiji, nao husema eti unaweza kupata pesa nyingi ukiwa mchungaji mjini kuliko kuwa mganga wa kienyeji kijijini kwa kuwa kule mjini unatumia nguvu zile zile za kichawi kana kwamba ni nguvu za Mungu kufanya miujiza na kuponya au kuokoa!
Matendo ya mitume sura ya 8 inatufundisha kuwa tamaa ya kutumia miujiza ili kupata pesa inatokana na tamaduni za kichawi.
Simoni alikuwa mchawi, lakini mara baada ya kusikia habari njema ikihubiriwa na Filipo, alibatizwa. Lakini alipoona ya kuwa watu wanapokea karama ya Roho Mtakatifu kwa kuombewa na mtume Petro, naye alitamani kupata uwezo huo, ndipo akatoa PESA kumpa Petro akisema, “Nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu.” (Matendo 8:19).
Simoni alikuwa bado hajatubu kwa kweli, ule uchawi wake wa zamani. Alikuwa bado anataka kuwa na nguvu za kutenda miujiza ili kuwavutia watu, na kujipatia pesa!
Jibu la Petro ni onyo kwetu sote,
“Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali.” (Matendo 8:20).
Maneno haya aliambiwa nani? Aliambiwa mtu yule ambaye aliyekuwa anatenda mambo ya kichawi, na ambaye sasa alikuwa anajaribu kuingiza tamaduni na fikra za kichawi kanisani!
Iwapo muhubiri yeyote yule akijaribu KUKUUZIA wewe chumvi, maji ya upako, au kitambaa, akidai kuwa vitu hivyo ndivyo vitakuletea baraka na uponyaji au mafanikio, basi mtu huyo atakuwa anajiweka yeye mwenyewe kwenye eneo lenye hatari sana. Ikiwa na wewe utalipa pesa zako ili KUNUNUA uongo wa vituko kama hivyo, ndipo na wewe utakuwa umejiweka mwenyewe katika eneo la hatari pia. Biblia inatupatia maonyo yenye kutuokoa na yenye usalama kutokana na mwenendo mbaya huo na mtazamo wa kiuchawi kama huo pale Petro anapomwambia Simoni,
“Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali.”
Hebu basi fikiri na ujiulize wewe mwenyewe, NI SEHEMU GANI katika Agano Jipya au hata ndani ya Biblia nzima ambapo alitokea mtu kumlipa mtumishi wa Mungu pesa ili apokee uponyaji au baraka? Jawabu la swali hili ni wazi kwamba hakuna popote pale! Hakuna kitu kama hiki kinachofundishwa na Biblia. Na kwa sababu hiyo basi yakupasa moja kwa moja kukataa fundisho hili na vitendo vyake wanavyofanya!
“Na katika kutamani watajipatia faida (yaani, pesa) kwenu kwa maneno yaliyotungwa; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii.” (2 Petro 2:3).
Tayari wengi wamehamia kwenye kutukuza maji ya upako, mafuta ya upako, sabuni za upako, chumvi ya upako, vitambaa na nguo za upako na kila aina ya vitu vya upako mpaka kanisa linaonekana kama kituo cha waganga wa kienyeji maana mambo ambayo tunaelekezwa kanisani sasa hayana tofauti kabisa na mambo ambayo watu wanaambiwa wakienda kwa waganga wa kienyeji.
Yesu alisema, “Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; MMEPATA BURE, TOENI BURE.” (Mathayo 10:8).
Ushuhuda wa Paulo ulikuwa ufuatao:
“SIKUTAMANI FEDHA WALA DHAHABU, WALA MAVAZI YA MTU. Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, NI HERI KUTOA KULIKO KUPOKEA.” (Matendo 20:33,35).