Mamlaka ya Maji Tukuyu: Mgao wa maji unahusu watu wote, hadi nyumbani kwa Spika Tulia na kwa DC napo kuna mgao

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Baada ya kuibuka kwa malalamiko ya uhaba wa maji Mjini Tukuyu, Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya, ikidaiwa kuwa kuna upendeleo katika mgawo wa maji, Mamlaka ya Maji ya Tukuyu imefafanua sababu ya mgao wa maji na kuweka wazi kuwa hakuna upendeleo katika mchakato huo.

Malalamiko haya hapa - Tukuyu: Baadhi ya mitaa yenye wananchi wa kawaida inanyima maji, huku yenye viongozi ikipendelewa

Mamlaka hiyo imeeleza kuwa kuna ujenzi wa Barabara unaofanywa na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) katika baadhi ya maeneo, umesababisha uharibifu wa miundombinu ya maji na hivyo wapo kwenye matengenezo ya mabomba.

MAMLAKA YA MAJI TUKUYU
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Tukuyu, Peter Amon anafafanua kwa kusema “Mamlaka yetu inatumia vyanzo vinne vya maji na tunahudumia Kata 6 za Tukuyu Mjini.

"Katika Kata hiyo eneo ambalo linapata maji takriban muda wote au zaidi ya Asilimia 80 ni Kata ya Idigi (Katumba) kwa sababu wapo karibu na vyanzo vya maji na eneo lao lipo tambalale.

"Maeneo mengine yanapata maji kwa mgao ikiwemo Bulyaga ambapo ni nyumbani kwa Spika wa Bunge, Tulia Ackson.

"Eneo lililolalamikiwa zaidi Mtaa wa Tanesco Power Station kuna ujenzi wa Barabara unaendelea, bomba zimekatwa na tupo kwenye ukarabati, Wananchi wanaona kinachoendelea.

"Hivyo, maeneo yote ya Tukuyu kuna mgawo hadi nyumbani kwa Mkuu wa Wilaya na ofisini kwake kote kuna mgao.

"Matengenezo yanatarajiwa kukamilika ndani ya wiki hii na yakikamilka mgao pia utapungua kwa asilimia kubwa na tutawataangazia Wananchi."
 
Kwamba hapa pana mgao?

1000131005.jpg
 
Back
Top Bottom