Mamlaka za maji (Idara za maji nchini), kwanini units za maji miezi ya mgao zinakuwa kubwa zaidi ya miezi ambayo maji hayakukatika?

marcozy

New Member
Jan 29, 2021
4
2
Leo kidogo naomba kuuliza swali juu ya huduma za mamlaka za maji mikoani na wilayani, kuna kitu huwa sielewi mfano kuna miezi maji hayakatiki kabisa (yaani hakuna mgao wa maji) na kuna miezi maji yanakatikai nzima, utata unakuja namna gani bili ya maji au usomaji wenu units za maji miezi ya mgao zilizotumika zinakuwa kubwa zaidi ya miezi ambayo maji hayakukatika?

Yaani mwezi ambao maji yamekuwepo 24/7 for 30 days bili inakuwa ndogo na siku mlizokata maji kwa wiki nzima au wiki mbili units na bili inakuwa juu sana ? Je hili ni kwa Kahama tu au na kwingine napo ni hivyo hivyo?

Mnasema eti upepo, je sisi tunawajibika kulipia upepo au ninyi ni idara ya maji na upepo ?, Okay tutaanza kuja kujaza tairi za magari sasa na pikipiki huko ofsini kwenu maana ni idara ya maji na upepo.

Please hili suala likoje kitaalamu?
 
Nimeishi Peke yangu Kwa mwezi mzima wa Desemba familia ikiwa likizo kijijini. Maji yametoka mara 6 Kwa mwezi mzima. Nimeletewa bill nimetumia Unit 19.
 
Leo kidogo naomba kuuliza swali juu ya huduma za mamlaka za maji mikoani na wilayani, kuna kitu huwa sielewi mfano kuna miezi maji hayakatiki kabisa (yaani hakuna mgao wa maji) na kuna miezi maji yanakatikai nzima, utata unakuja namna gani bili ya maji au usomaji wenu units za maji miezi ya mgao zilizotumika zinakuwa kubwa zaidi ya miezi ambayo maji hayakukatika?

Yaani mwezi ambao maji yamekuwepo 24/7 for 30 days bili inakuwa ndogo na siku mlizokata maji kwa wiki nzima au wiki mbili units na bili inakuwa juu sana ? Je hili ni kwa Kahama tu au na kwingine napo ni hivyo hivyo?

Mnasema eti upepo, je sisi tunawajibika kulipia upepo au ninyi ni idara ya maji na upepo ?, Okay tutaanza kuja kujaza tairi za magari sasa na pikipiki huko ofsini kwenu maana ni idara ya maji na upepo.

Please hili suala likoje kitaalamu?
Bill wanakadiria. Hawana hasara.

Wanachofanya wanaamua kwa mwezi husika wanataka pesa kiasi gani, halafu wanagawanya kwa idadi ya wateja

Kwasababu wabongo ni mazuzu top level
 
Kwa kifupi watu wa idara ya maji 90% ni wapigaji.

Mbaya Zaidi hata ukienda kulalamika ofisini kwao hupati msaada wowote Zaidi ya kukugeuza kituko.

Mbali na hilo la kubambikiza bills za maji pia kuna hili la kukatia wateja maji ukiwa na deni kiasi kidogo unachodaiwa.

Lengo ni kukupiga kwenye FINE 15000.

Hivi DAWASA mtakataje maji kwa mteja anayedaiwa deni la 10,000 ili ulipwe FINE 15000? ndy mrudishe maji..

Tukisema DAWASA ni wahuni mnashupaza shingo kwa ubishi.

Yaani mkate maji kwa deni la 10000,halafu mteja aje alipe 25000 ndy mrudishe huduma..
 
Back
Top Bottom