Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,889
Kutokana na ugumu wa ajira kwenye nchi hii naomba Mh Rais urahisishe mchakato wa watu kwenda nje ya nchi kutafuta ajira na kazi.
Kikwazo kikubwa cha watu kwenda nje ya nchi ni passport na masharti yake. Hili limepelekea watanzania walio nje ya nchi wawe wachache sana.
Nchi kama US kuna Watanzania kama 20,000 tu lakini Wakenya ni zaidi ya 100,000. Hapo Kenya wanajipatia fedha za kutosha kupitia Remittances.
US mbali, kuna nchi kama Congo DR nchi inayohitaji wataalamu wengi na sisi tuna hadi madaktari waliokosa kazi, ikirahisishwa namna ya kwenda nje ya nchi hawa wanaweza kwenda na nchi ikajipatia pesa. Bado manesi, mainjinia, waalimu na watu wengine kibao ambao nchi haiwezi kuwaajiri lakini wanaweza kupata kazi nje ya nchi.
Nashauri kigezo cha kupata passport iwe ni kuwa na namba/kitambulisho cha NIDA tu. Yasiwepo mambo mengine ya kikwamishaji na urasimu usio na maana. Na gharama ya passport ikiwezekana ipunguzwe. Waache watu watoke. Nchi kama Mexico inahimiza kichinichini watu wake wahamie Marekani. Wamexico wanatuma nyumbani karibu USD 36 billion kwa mwaka kutoka US. Hii ni zaidi hata ya bajeti yetu.
Wacuba wanatuma madaktari duniani kote, kuna madaktari wa Cuba Kenya, Angola na kote. Wana madaktari Venezuela na wao wakilipwa mafuta.
Waethiopia wamejaa duniani kote kusaka kazi na kutuma pesa nyumbani.
Turahisihe na kuhimiza watu kutoka nchini. Tutawanye watanzania huko Msumbiji, Malawi, Zambia, Congo, Angola na kote.
Kwanza kuweka vikwazo kwa watu kutoka nje ya nchi hakuna faida wakati huna uwezo wa kuwatumia, zaidi zaidi ni kuzidi kuchochea bomu la ajira lilipuke.
Nashauri nchi ifanye hivyo sababu sisi hatuna uwezo wa kulisha wanaume elfu tano kwa samaki wawili na mikate mitano.